Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Kizazi cha vijana cha leo ni tofauti na cha miaka ya 1980 kutudi nyuma hadi 1961
Uwezo wa kufikiri wa vijana wakileo ni mdogo tena nimdogo kiasi cha kuhatarisha usalama wa nchi yetu!
Kuna njia nyingi za kurejesha ushupavu, uzalendo, na uwezo kifikra wa vijana wa leo na kesho, mfano kuboresha mfumo wa elimu yetu, kurejesha mafunzo ya mgambo yawe ni lazima kwa kila kijana, kuweka utaratibu wa kuitisha mikutano ya vijana kila mwaka kwa kila mkoa na wilaya,
Lakini yote hayo yanaweza kuwa msaada mbalada tu, mimi napendekeza KODI ya kichwa irejeshwe,
Iwekwe katika makundi, vijana waishio mjini watozwe kodi stahiki kama ni 10000 (elfu kumi)
Wale wa vijijini walipe nusu 5000 (elfu tano)
Hili litasaidia kuwafanya vijana kujituma/kuchakarika/kupigana kusaka pesa!
Licha ya kusaka pesa, vijana watakuwa na uchungu na nchi yao hasa wakisikia kuwa KODI yao inaibwa na kufichwa USWISI na kikundi kidogo mufilisi kilichopewa dhamani ya kuwaongoza!
Napendekeza Kodi ya kichwa irejeshweeee!
Yericho
Kimsingi serikali imeondoa direct tax kwa ajiri ya kuzima nguvu ya wananchi kuihoji juu ya matumizi na utendaji wake, ndio maana leo watu wachache sana tunalazimika kuilalamikia serikali na kuipush kutueleza kwa nini tunaendelea kuwa masikini wakati tuna rasilimali nyingi mwisho wa siku kwa sababu wengi wengi hatujawahi kuona dhahabu,almasi, wala kutembea mbuga za wanyama na hatujui thamani yake sokoni ni kiasi gani ukizingatia vitu hivyo haviko karibu hata kidogo na maisha yetu ya kila siku, baada ya muda mfupi tunasahau na tunakuwa wepesi sana kubadirishiwa sinema.
kama tutalipa kodi ya kichwa (kwa jina lolote lile) swali litakuwa where is our money going?? pasingetosha hapa