Nilipoingia mahabusu kwa kubambikwa kesi ya kuiba na kuvunja

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
771
1,000
Siku hiyo kulikuwa na mechi ya Simba na Yanga, mechi hiyo iliisha kwa Simba kushinda goli 1 kwa nunge goli la MK14.

Ilikuwa ni mida ya saa kumi ndio kulikuwa na hiyo mechi hapo palikuwa ni lodge na bar ya mshua na Mimi ndio msimamizi au meneja wa hapo.

Wakati nipo bize nikitazama mpira huo walikuja wageni fulani na gari mimi sikuwaona ilo nilijua baadae nilikuwa bize na mpira mpaka wanachukua vyumba wahudumu ndio walishughulika nao.

Mechi ikaisha nipo na furaha kwa Simba chama langu kushinda na siku ikapita saaafi.

Sasa siku fulani mida ya saa moja jioni ilikuwa kama mwezi wa 11 au 12 ilipita karibu miezi mitatu hivi toka hilo tukio, nimetoka saloon naelekea apo lodge hiyo ni tarehe 7 tarehe ambayo wasimamizi wa guest inakuwa ni tarehe ya mwisho kwenda kulipia kodi ya mapato ya mwezi uliopita.

Na siku hiyo nilitoka kulipia kitabu manispaa ila tulikuwa na guest 2 zote hizo mimi ndio huwa naenda kulipia lazima ubebe kitabu cha wageni, wakati nimetoka kulipia pale manispaa ya Songea Mjini nilipoondoka guest ya kwanza ipo bombambili inabidi nipite hapo niache kitabu mi sikupita nikaona ntakileta baadae nikanyosha kuelekea ambako ndio hua nashinda

vitabu vipo kwenye begi ile kufika nikaacha begi kaunta nikasepa na mizunguko yangu.

Jioni iyo saa moja ndio natoka saloon kunyoa narudi nakuta gari tatu zipo pale ndani Toyota mayai nyeupe 2 na moja ni IST kijivu.

Nikapita zangu huwani sina ili wala lile nikaona kupitia dirisha muhudumu kabananishwa anaulizwa iki kitabu cha wapi mbona namba tofauti mnatumia vitabu viwili sio??
Kakosa jibu ameduwaa tu yule askari mkali kinyama jina lake maarufu LUKUBA sijui muhehe sjui mbena
Basi bana nikaona kumbe ishu ni kitabu ngoja niende nikawaelekeze nikajua wakaguzi tu wa vitabu nikaingia pale akamuuliza muhudumu
Meneja yupo wapi aliponiona akasema uyu hapa akaniuliza
Kitabu cha gest kipo wapi?? iki sio na manatumia vitabu viwili

Kumbe muhudumu alipoenda kwenye beg langu akachukua tu kitabu bila kuangalia na kuwaletea alafu beg lilikua na kitabu kingne cha gest iyo nyingne sasa ye alijua cha pale ndio akaleta.

Mi nikamwambia afande kitabu iki kakosea iki sio cha hapa mim nilijisahau Leo siku ya kulipia iki kitabu ilibdi nipitishe gest flani

akahamaki we brother mpumbavu acha ujanja brother Sawa kabla ya kuja uku unapita pale kivipi usahau acha masihara cha hapa kikwapi nikaenda kuchukua bana nipo na askari yupo na mtutu ananifata nyuma yule askari aliniambia dogo kua mkweli na usiseme uongo Sawa usiogope nikamwambia aina shida bro apo sijui tatizo kubwa ni nini mpaka mitutu.

nikaleta kitabu wakaangalia majina ya watu wao yalikuapo ila ya uongo sio ya ukwli na muda ule wateja walioingia awakuandikwa, na wahudumu usipokuepo wanapiga kwa mtindo huu awaandiki jina pesa kapuni mpaka ufatilie sasa iyo siku ndio ukawa msala.

Afande akasema meneja mzembe, we Dada bahati yako tungeondoka na wewe ila kaja uyu tunaondoka nae we utabaki du mungu wangu nakwenda selo,
saa moja jioni iyo nikajipa moyo sina kosa ntarudi bana.
Nikaingizwa kwenye IST tulikua na afande mmoja anaitwa victor pande la mtu black ivi kaenda hewani akasema meneja usihofu bana wala akuna shida.
yule afande mkali wakaingia gari nyingne nikawaona na jamaa flani ivi wamepigwa pingu wapo wawili usoni sikuwaona vizuri, safari mpaka kituo kikuu songea nikaingizwa kaunta pale nikawekwa chini nika ambiwa nivue viatu mkanda nikabizi na simu na kila kitu kilichopo mfukoni mwangu nikafanya ivyo nikaa kaa pale chini nilivaa soksi azikukakuka vizuri bana harufu iliyotoka hapo ilisamba pale pote nasikia askari nini hiki sijui mmoja akasema mhm kuna dogo kavua kiatu kachafua hewa.....ilikua balaa

Tuendelee kwenye point nika andika majina yangu pale kaunta afande yule aliuliza uyu ana kesi gani yule afande mnoko akajbu kuiba na kuvunja nikashangaa Mimi kuiba na kuvunja lini,
then nikapelekwa mahabusu for the first time katika maisha yangu jamaa walinipokea oya umekula msosi hapana sijala wakaniletea msosi bana
Ulikua ugali na dagaa bwana uo ugali ata bodingi school sikuwai ona wakati nasoma kummmke uji maunga unga tupu mboga dagaa maji chumvi mchuzi kibao aise ulinishinda kula nikasema hapana nimeshiba bana si ulisema ujala nikajbu Amna shida.

Ndani mahabusu nilimkuta bro wangu mtoto wa mama mkubwa upande mwingine wa uko kama unavyojua ndugu sometimes mkionana ndio apo apo alikua ana kesi yake ila sikuijua baadae niliijua.

nae ananishangaa dogo vipi umekula mtaji nini wa louge nikamwambia hapana bro ila nime andikiwa kesi ya kuiba na kuvunja
Sielewi chochote hapa,

tukatulia pale piga stori kidogo wanaletwa wazurulaji ma boda boda mpaka kukajaa mule ndani kuna muda watu wakamaindi ahaa umu tumejaa afande tunajibana
afande akasema sogeeni chooni uko watu wakagoma,
bana afande akasema msinizoee Sawa akaingia akatandika mtu kofi paaaa watu wakanywea wakasogea vile vichumba vimejaa.

naiti iyo, sasa nikajilaza sakafuni kichwa ukutani naangalia bati usingiz Amna jamaa wengne wapo na story tu kusogeza masaa pale ukutani nilipoweka kichwa walinipanda kunguni kichwani uzuri sikua na nywele kubwa nikawatoa wote nikalala katikati kwa kujibana ukuta nikauacha mbali yule bro wangu alinipa kopo la maji lina maji ndani ndio kama mto unaweka kichwani,
Apo nawaza watakuja sasa ivi kunitoa kimya.

Tumelala tupo ka biskuti ivi
Kumbe mshua alifika kunifata kituoni, uyu ni mshua wangu mkubwa ila sio baba mzazi na awajatoka tumbo moja na dingi ye kamuoa mama yangu mkubwa ambae ndio toka nitoke na mama yangu mzazi.

Alivyofika pale kaunta akauliza jina langu ibrahim akatajiwa ila Mimi niliandika jina la pili la babu na sio la baba hua najichanganya sana na uyu dingi nafikir alikua analijua jina la mzee wangu la kwanza tu akauliza ana kesi gani wakamwambia kuvunja na kuiba akaona haaaa sio yeye uyu kuiba na kuvunja wapi na wapi akasepa kwenda vituo vingine kunisaka.
Tena siku iyo usiku kulikua na mpira wa uefa juve na Manchester united afande baadae akaja akasema oya nyie wale wa mpira Manchester wamesinda 2-1 apo nikajua saa sita sasa ndio muda mpira unaisha ulianza SAA 4...............
Pause kidogo Ntarudi kuimaliza
 
IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
771
1,000
Madongo ka yote Mara malinda yalikua salama ? Mara mambo mengi story zenye part2 zisitishwe OK fine
Tuendelee mida iyo ya usiku tukiwa tumelala na wengne wapo na story nikaamka nikajiunga kwenye story nilikua msikilizaji tu mladi muda uende lakini usingiz sio mchezo ukatupitia kuna muda watu wote kimya kabisa

Apo natamani kukuche waje wanitoe mida ya saa kumi na moja alafajiri ile azana akaja askari akauliza nani anataka kutoka jamaa flani wawili wakawai fasta mlangoni pale akasema nyie ndio wajanja akawatoa akafunga mlango.

Tukajiuliza unatokaje kirahisi ivi baadae wakarudishwa kumbe walienda kudekishwa na kufagia nje
asubhi kabisa purukushani zikaanza ndugu wanakuja kutoa jamaa zao mule
Majina yanaitwa kama ni kunywa chai utarudi kama kutoka ndio aurudi.

Ghafla nikasikia jina langu ibu bin flani fasta nikasogea mlangoni nikatolewa nikakuta mother yupo na mam mkubwa na yule dingi, dingi akauliza kwa askari sasa uyu ndio kesi ya kuiba na kuvunja afande akajibu mzee sio Mimi hii kesi ina wenyewe wakti nimesimama pale yule afande akasema dogo kesi yako ngumu
Mhmm nikashtuka ngumu kivipi

Akasema kuiba na kuvunja kesi kubwa na palipoibwa hapo sio poa nikaitwa kwa mmama mmoja ivi mwana sheria nikaongea nae nae nikawa simuelewi wala nini baada ya kumuelezea nae akaguna tu na kusema mungu atakusaidia usiwe na was wasi nikarudi lumande nikapewa na chai mule ndani kampani yote tunapunguziana kidogo kidogo fresh.

Nilikaa mule watu wengine wanatoka wengne wanabaki kuna jamaa mmoja dereva wa superfeo sijui alifanya nni kakaa wiki nzima akielewki akasema Leo sikubali
Akajitupa chini akaanza kugalagala kwamba anaumwa ila alikua anakojoa damu, mule ndani mazingira ni machafu sana aligaragara pale chini mpaka anaitwa askari akaja
Yule askari akasema mengne yatajifia humu yashaoza wakambeba mpaka nje wakampeleka hospital.

Sasa 7 azana sioni dalil ya kutoka saa kumi nayo azana kimya mhm nikaona hapa kuna hatari ya kulala tena itakuaje,nikawaza ikivuka Leo sijatoka kesho lazima niumwe nikalazwe hosptali uko potelea mbali ata nikifungwa pingu poa tu
Wale majambazi waliofungwa pingu na kuja nao kule gest nikawaona sasa walikua chumba kingne nikajua kabisa hawa ndio wamesababisha mim kulala humu kudadeki apo nipo kimya nawaza siku ya pili tena inikute humu ahaa kudadeki,

Akaja afande victor akaita Yale majamabaz ya kuvunja wakatoka wale jamaa wapo na pingu yao mkononi akaita na meneja nikatoka pale kaunta nikapewa simu yangu na vitu vyangu vyote tukaingizwa kwenye gari wote safari tena mhm sikujua tunaenda wapi pamoja na ma mother wangu na mzee nikaona akuna shida na hawa wapo sio ishu.

Tukaenda makao makuu ofisi ya upelelez karibu na kwa mkuu wa mkoa ghorofani mahojiano yakaanza askari anawauliza wale jamaa uyu mnamjua mmoja alikua mzee ivi sio sana mwngne kijana, mzee alikua mkaidi anapewa vitasa mhm yule mshkaji akasema mzee tuseme ukweli tutaumia hapa tukiulizwa tuanchojua tuseme

Ndio akawauliza uyu mnamjua wakasema atumjui nikasema afazali siku mlioenda pale gest mlimuona wakajbu atukumuona uyu.
Akaniuliza Mimi kwann unashirikiana na majambazi nikasema afande sijashirikiana na majambazi na si wajui hawa si umewasikia mwenyewe akasema kama wanakulinda si tutajuaje mmoja wao akasema uyu afande atumjui ile siku tumelala pale ni wahudumu tu ndio tunawakumbuka sio uyu atukumuona

Afande akasema kelele hapa nikatolewa nikapelekwa chumba kingne kutoa maelezo nikaanza kuhojiwa
iyo usiku ulikua wapi mpaka wanakuja nikawapa
A to Z maelezo yangu yaka andikwa yote karatasi mbili badae jioni saa kumi na mbili ndio nikatolewa kwa zamana na kupewa maagizo wahudumu waje watoe maelezo ili kusaidia ushahidi kwa polisi.

Nikaambiwa na nianze kuripoti kila baada ya siku tatu bila kukosa
Nikatoka mpaka home nikaoga kutoa nuksi wenyewe wanasema na nguo kufua.
Siku ya pili wahudumu nao walienda kuhojiwa sasa maelezo ya wahudumu ndio yalikua safi kwao polisi ila yangu ayakua na msaada sababu sikuwaona na ata wao awanijui.

Jama kesi yao walivunja stoo ya bia ya kampun ya breweries songea ipo maeneo ya masamala karibu na stendi kuu ya zamani na kuiba pesa kuna mtu aliwachoreshea mchongo inasemekana ni mlinzi.

Sababu za Mimi kuambiwa kesi ngumu ni bosi alimwaga pesa hao watu walio husika washikiliwe na bosi uyo ni boss STRAM anaitwa mi namjua kwa jina ilo hata zile gari zao za bia zimeandkiwa stram
Na jamaa Walishikwa kwa njia ya simu waliwakamatia shinyanga uko kitu kama icho kushikwa kwao ilikua ni mlinzi ambae anasema alipigwa na kufungwa kamba mikono nyuma ila sasa akatuma meseji kwa mtu kupitia simu yake

kavamiwa ndipo akashikwa unatumaje mesj mikono ipo nyuma ndio akataja wenzake na namba yao waka wa track na kuwashka wawili mmoja walimkosa alikua tandahimba nafikir maeneo ya mtwara baadae awakumuona tena kwnye trace zao nahisi alishtuka.

Sijui ikawaje kama walimshika au vipi nikaanza kuripoti siku ya kwanza wakasema uje tena siku flani
Ikawadia iyo siku nikaenda wanauliza we nan na una kesi gani nawajbu Sawa tumekuona ondoka nasepa bila kusahini wala chochote ila wengne wakawa wakija kuripoti wanasaini.
Baadae ikawa wiki na hatimae kila mwezi ila sasa kwanin kila nikiifika sisaini na wengne wote wanasaini kingne mimi wanashangaa una kesi gani ukiwaambia wanasema Sawa ondoka siku nyingne wanasema afande wako ayupo Mara we ulipoti kwangu nenda kwa flani ukienda uko nako wanasema we nenda zako unatuletea kiwingu uje siku nyingne.

Nikaona hapa naonaekana msukule na sijulikani kwanza kesi sio yangu wenye kesi wapo nikaacha kuripoti
Nikimuona afande victor mitaani uku nalala mbele namkwepa ivyo ivyo

Kuna siku njian tukakutana uso kwa uso niakaona hapa Leo kimbembe akauliza meneja upo mbona uonekani nikamwambia nipo afande vipi ujaleta majamabz mengine nikamwambia nipo makini saiz tukapiga story akasepa apo ndio nikapata kibali cha kua huru sasa kumbe swala la kulipoti lilisha sahaulika.

Mwaka 2020 wale wahudumu waliitwa mahakamani kwenda kutoa ushahidi mi sikuitwa kama nilivyosema maelezo yangu ayakua na msaada ila ya wahudumu ndio yalikua sahihi sana wao ndio waliwauhudumia siku iyo kesi ilihairishwa na kupangwa tarehe nyingne

Siku waliokuja gesti kulala wale majambazi walitoka usiku na ndio walienda kufanya tukio la kuiba pesa.
Na kuna mtu alikua kama ndio mfazili wao aliwalipia chumba na kila kitu pale gest na vyumba walivyo lala vilifatana namba 9 na 10.

Hao wahudumu mmoja ni mtu mzima kidogo mwingine binti alihetimia yupo vizuri kweli wale maafande bana karatasi ya uyu muhudumu binti ilikua inachunguzwa sana kumbe kuchukua namba bana na walikua wana msumbua sana mala njoo kituoni kuna maelezo inabidi utoe amna kitu wanataka mzigo tu ila aliniambia kati yao kuna mzee alimpitia na aliniambia uyo mzee ana puling ya hatari sijui alimnywea viaga alisema arudii tena kwake na mpaka pale lodge akawa anakuja kumbembeleza ampe mzigo tena.

Uyu mzee nikikutana nae njiani lazima aniulizie yule muhudumu wako yupo lazma tu
na pia afande mwngne na yeye alipita sema uyu Dada nae achengeshi swala ni mpunga tu.

Kashaulo
Upande wa malinda wakuu mahabusu swala la kuondoana malinda halipo kwa nijuavyo Mimi sijui wengne aya yanakua uko magerezani kwa wafungwa ndio ninavyo elewa.
Mwisho
 
Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,675
2,000
Story nzuri na ni experience mbaya kwa kweli.
Selo pasikie tu lakini si kulala humo. Ni hatari hasa kama kesi yako haieleweki. Maana hujui utatoka ama la!

Ila pia polisi ni watu wanaojua sana kumtingisha mtu kisaikolojia. Kama hauko imara unaweza kujiharishia.
 
sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,038
2,000
Nilikuwa naogopa sero ila nilipoingia mwaka 2016 kulinipa uzoefu mkubwa sana.

Ni sehem ambayo iko vizuri tu wala haina shida, Shida ni kupelekwa mahabusu huko unaweza kukaa hata miaka kesi haijasikilizwa.

Ni vyema ukiingia selo uhakikishe unasaidiwa na watu wako wa karibu kuyamaliza hapo hapo fasta utembee zako urudi mtaani.

Kiufupi selo haina tatizo kabisa, hata ukae wiki poa tu, kimbembe upandishwe kwenye defender upelekwe mahabusu, aisee huko ukienda nafasi yako ya kurudi uraiani inakua ndogo zaidi, ukifika mahabusu ni l unaweza kusubiria kwenda mahakamani muda mrefu sana na hata ukienda mahakamani utaskia kesi imeahirishwa inabidi tena urudi mahabusu, ponapona yako usomewe kesi uhukumiwe tu uanze kifungo chako mapema ama wanaokushtaki watulize munkari waseme hawana ushhidi ili urudi uraiani.

Sero ni kama sebleni tu, hakuna noma wala nini, wewe tulia tu fanya ujanja upate simu ya kumpigia mwanafamilia, ndugu, rafiki waje kukutoa endapo kosa ulilofanya sio serios sana, Nakumbuka waliichukua simu yangu na wallet yangu ya vitambulisho waliniambia niwe naripoti kila siku asubuhi, kila nikienda naulizwa nina kesi gani 😂 siku ya 3 nikaambiwa nawajazia kiwingu tu hapo wakanipa simu na waletina mimi ndio nikatokomea sikwenda tena.

Ila nilivyokuwa naenda kuripoti hio saa moja asubuhi daah, Maafande sio watu wale, kuna mzee mlinzi wa duka flani lililoibiwa alikuwa kakamatwa tulikuwa nae sero bosi wake alimpeleka polisi anadai yeye ndio karuhusu wezi waibe, bosi wake alikuwa anawapa pesa mpolisi wawe wamkamue ukweli (kipigo), basi nikifika pale polisi asubuhi nasubiria nje ya mlango wa ofisi ya kuripoti humo ndani sasa kuna miguno mhh mhhh ahh afandeee unaniuaa!!, afande alikuwa anatumia kufuli kubwa kumpiga yule mlinzi kwenye ugoko, yani kuanzia siku ile niliapa mimi na maafande hatuwezi kuwa marafiki
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
61,201
2,000
Siku iyo kulikua na mechi ya simba na yanga, mechi iyo iliisha kwa simba kushinda goli 1 kwa nunge goli la mk14 kagere.

Ilikua ni mida ya saa kumi ndio kulikua na iyo mechi apo palikua ni louge na bar ya mshua na Mimi ndio msimamizi au meneja wa hapo.

Wakati nipo bize nikitazama mpira huo walikuja wageni flani na gari mi sikuwaona ilo nilijua baadae nilikua bize na mpira mpaka wanachukua vyumba wahudumu ndio walishughulika nao,
Mechi ikaisha nipo na furaha kwa simba chama langu kushinda na siku ikapita saaafi.

Sasa siku flani mida ya saa moja jion ilikua kama mwezi wa 11 au 12 ilipita karibu miez mitatu ivi toka ilo tukio, nimetoka saloon naelekea apo louge iyo ni tarehe 7 tarehe ambayo wasimamizi wa gest inakua ni tarehe ya mwisho kwenda kulipia kodi ya mapato ya mwezi uliopita.
Na siku iyo nilitoka kulipia kitabu manispaa ila tulikua na gest 2 zote izo mi ndio huo naenda kulipia lazima ubebe kitabu cha wageni, wakati nimetoka kulipia pale manispaa ya songea mjini nilipo ondoka gest ya kwanza ipo bombambili inabidi nipite hapo niache kitabu mi sikupita nikaona ntakileta baadae nikanyosha kuelekea ambako ndio hua nashinda

vitabu vipo kwenye begi ile kufika nikaacha begi kaunta nikasepa na mizunguko yangu.

Jioni iyo saa moja ndio natoka saloon kunyoa narudi nakuta gari tatu zipo pale ndani Toyota mayai nyeupe 2 na moja ni IST kijivu.

Nikapita zangu huwani sina ili wala lile nikaona kupitia dirisha muhudumu kabananishwa anaulizwa iki kitabu cha wapi mbona namba tofauti mnatumia vitabu viwili sio??
Kakosa jibu ameduwaa tu yule askari mkali kinyama jina lake maarufu LUKUBA sijui muhehe sjui mbena
Basi bana nikaona kumbe ishu ni kitabu ngoja niende nikawaelekeze nikajua wakaguzi tu wa vitabu nikaingia pale akamuuliza muhudumu
Meneja yupo wapi aliponiona akasema uyu hapa akaniuliza
Kitabu cha gest kipo wapi?? iki sio na manatumia vitabu viwili

Kumbe muhudumu alipoenda kwenye beg langu akachukua tu kitabu bila kuangalia na kuwaletea alafu beg lilikua na kitabu kingne cha gest iyo nyingne sasa ye alijua cha pale ndio akaleta.

Mi nikamwambia afande kitabu iki kakosea iki sio cha hapa mim nilijisahau Leo siku ya kulipia iki kitabu ilibdi nipitishe gest flani

akahamaki we brother mpumbavu acha ujanja brother Sawa kabla ya kuja uku unapita pale kivipi usahau acha masihara cha hapa kikwapi nikaenda kuchukua bana nipo na askari yupo na mtutu ananifata nyuma yule askari aliniambia dogo kua mkweli na usiseme uongo Sawa usiogope nikamwambia aina shida bro apo sijui tatizo kubwa ni nini mpaka mitutu.

nikaleta kitabu wakaangalia majina ya watu wao yalikuapo ila ya uongo sio ya ukwli na muda ule wateja walioingia awakuandikwa, na wahudumu usipokuepo wanapiga kwa mtindo huu awaandiki jina pesa kapuni mpaka ufatilie sasa iyo siku ndio ukawa msala.

Afande akasema meneja mzembe, we Dada bahati yako tungeondoka na wewe ila kaja uyu tunaondoka nae we utabaki du mungu wangu nakwenda selo,
saa moja jioni iyo nikajipa moyo sina kosa ntarudi bana.
Nikaingizwa kwenye IST tulikua na afande mmoja anaitwa victor pande la mtu black ivi kaenda hewani akasema meneja usihofu bana wala akuna shida.
yule afande mkali wakaingia gari nyingne nikawaona na jamaa flani ivi wamepigwa pingu wapo wawili usoni sikuwaona vizuri, safari mpaka kituo kikuu songea nikaingizwa kaunta pale nikawekwa chini nika ambiwa nivue viatu mkanda nikabizi na simu na kila kitu kilichopo mfukoni mwangu nikafanya ivyo nikaa kaa pale chini nilivaa soksi azikukakuka vizuri bana harufu iliyotoka hapo ilisamba pale pote nasikia askari nini hiki sijui mmoja akasema mhm kuna dogo kavua kiatu kachafua hewa.....ilikua balaa

Tuendelee kwenye point nika andika majina yangu pale kaunta afande yule aliuliza uyu ana kesi gani yule afande mnoko akajbu kuiba na kuvunja nikashangaa Mimi kuiba na kuvunja lini,
then nikapelekwa mahabusu for the first time katika maisha yangu jamaa walinipokea oya umekula msosi hapana sijala wakaniletea msosi bana
Ulikua ugali na dagaa bwana uo ugali ata bodingi school sikuwai ona wakati nasoma kummmke uji maunga unga tupu mboga dagaa maji chumvi mchuzi kibao aise ulinishinda kula nikasema hapana nimeshiba bana si ulisema ujala nikajbu Amna shida.

Ndani mahabusu nilimkuta bro wangu mtoto wa mama mkubwa upande mwingine wa uko kama unavyojua ndugu sometimes mkionana ndio apo apo alikua ana kesi yake ila sikuijua baadae niliijua.

nae ananishangaa dogo vipi umekula mtaji nini wa louge nikamwambia hapana bro ila nime andikiwa kesi ya kuiba na kuvunja
Sielewi chochote hapa,

tukatulia pale piga stori kidogo wanaletwa wazurulaji ma boda boda mpaka kukajaa mule ndani kuna muda watu wakamaindi ahaa umu tumejaa afande tunajibana
afande akasema sogeeni chooni uko watu wakagoma,
bana afande akasema msinizoee Sawa akaingia akatandika mtu kofi paaaa watu wakanywea wakasogea vile vichumba vimejaa.

naiti iyo, sasa nikajilaza sakafuni kichwa ukutani naangalia bati usingiz Amna jamaa wengne wapo na story tu kusogeza masaa pale ukutani nilipoweka kichwa walinipanda kunguni kichwani uzuri sikua na nywele kubwa nikawatoa wote nikalala katikati kwa kujibana ukuta nikauacha mbali yule bro wangu alinipa kopo la maji lina maji ndani ndio kama mto unaweka kichwani,
Apo nawaza watakuja sasa ivi kunitoa kimya.

Tumelala tupo ka biskuti ivi
Kumbe mshua alifika kunifata kituoni, uyu ni mshua wangu mkubwa ila sio baba mzazi na awajatoka tumbo moja na dingi ye kamuoa mama yangu mkubwa ambae ndio toka nitoke na mama yangu mzazi.

Alivyofika pale kaunta akauliza jina langu ibrahim akatajiwa ila Mimi niliandika jina la pili la babu na sio la baba hua najichanganya sana na uyu dingi nafikir alikua analijua jina la mzee wangu la kwanza tu akauliza ana kesi gani wakamwambia kuvunja na kuiba akaona haaaa sio yeye uyu kuiba na kuvunja wapi na wapi akasepa kwenda vituo vingine kunisaka.
Tena siku iyo usiku kulikua na mpira wa uefa juve na Manchester united afande baadae akaja akasema oya nyie wale wa mpira Manchester wamesinda 2-1 apo nikajua saa sita sasa ndio muda mpira unaisha ulianza SAA 4...............
Pause kidogo Ntarudi kuimaliza
Ukirudi boresha aina yako ya uandishi
 
IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
771
1,000
Nilikuwa naogopa sero ila nilipoingia mwaka 2016 kulinipa uzoefu mkubwa sana.

Ni sehem ambayo iko vizuri tu wala haina shida, Shida ni kupelekwa mahabusu huko unaweza kukaa hata miaka kesi haijasikilizwa.

Ni vyema ukiingia selo uhakikishe unasaidiwa na watu wako wa karibu kuyamaliza hapo hapo fasta utembee zako urudi mtaani.

Kiufupi selo haina tatizo kabisa, hata ujae wiki poa tu, kimbembe kwenda kule mahabusu aisee, huko ukienda unasubiria kwenda mahakamani na mahakamani ukifika unasomewa hukumu unaenda jela.

Sero ni kama sebleni tu, hakuna noma wala nini, Nakumbuka waliichukua simu yangu na wallet yangu ya vitambulisho waliniambia niwe naripoti kila siku asubuhi, kila nikienda naulizwa nina kesi gani 😂 siku ya 3 nikaambiwa nawajazia kiwingu tu hapo wakanipa simu na waleti sikwenda tena.

Ila nilivyokuwa naenda kuripoti hio saa moja asubuhi daah, Maafande sio watu wale, kuna mzee mlinzi wa duka flani lililoibiwa alikuwa kakamatwa wanadai yeye ndio karuhusu wezi waibe, bosi wake ni kijana alikuwa anawapa pesa wapelelezi wamkamue ukweli, basi nikifika pale nasubiria nje ya mlango humo ndani sasa kuna miguno, afande alikuwa anatumia kufuli kubwa kumpiga yule mlinzi, yani kuanzia siku ile niliapa mimi na maafande hatuwezi kuwa marafiki
Kuna wengne niliwakuta wana mwaka wapo mahabusu wanaenda mahakamani kesi ina hairishwa wanarudi mahabusu du
 
SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,726
2,000
Jana nilikuwa natokea maeneo flani Hivi mashambani huko wakati napita asubuhi kipande kile cha fukayosi niliwaona jamaa wakiwa wamevaa sare rangi ya fanta, mda narudi dar kupita pale masaa ya kumi na moja jioni hivi nikawakuta pale pale wakiwa wamepika mihogo kwenye jungu kubwa wamewekwa chini ya ulinzi wanakula, kuna jamaa ndani ya gari alisikika akisikitika jamaa wamepiga kazi mshahara ndio ile mihogo wanayokula pole sana mkuu jela au mahabusu sio kuzuri
 
sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,038
2,000
Kuna wengne niliwakuta wana mwaka wapo mahabusu wanaenda mahakamani kesi ina hairishwa wanarudi mahabusu du
Ndio umuhimu wa ndugu na familia unapoonekana, Kama huna ndugu ama uligombana ama kukata mawasiliano na ndugu zako au familia ulikotoka ndio umeshakwenda hivyo.

Binafsi nlitoka baada ya ndugu zangu kunipambania, niliingia sero jioni ila saa 12 asubuhi walifika kituoni, Saa tano nikatolewa.

Alafu mtu ukiingia mara ya kwanza mule unajipa matumaini kwamba utatoka sio mda kumbe waweza kukaa sero mule wiki na baada ya hapo ni mahabusu waweza kusota mwaka na hapo bado sijahesabia hukumu ya miaka kadhaa jela.

Kwa ambao tumewahi kuingia sero na kulala sakafuni angalau tunajua umuhimu wa kujinasua haraka pindi unspokamatwa, yani hakikisha unatumia pesa yako pale pale unapokamatwa wakuachie au kama wamekukamata wakiwa hawana bunduki we kimbia tu.
 
Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,316
2,000
Siku hiyo kulikuwa na mechi ya Simba na Yanga, mechi hiyo iliisha kwa Simba kushinda goli 1 kwa nunge goli la MK14.

Ilikuwa ni mida ya saa kumi ndio kulikuwa na hiyo mechi hapo palikuwa ni lodge na bar ya mshua na Mimi ndio msimamizi au meneja wa hapo.

Wakati nipo bize nikitazama mpira huo walikuja wageni fulani na gari mimi sikuwaona ilo nilijua baadae nilikuwa bize na mpira mpaka wanachukua vyumba wahudumu ndio walishughulika nao.

Mechi ikaisha nipo na furaha kwa Simba chama langu kushinda na siku ikapita saaafi.

Sasa siku fulani mida ya saa moja jioni ilikuwa kama mwezi wa 11 au 12 ilipita karibu miezi mitatu hivi toka hilo tukio, nimetoka saloon naelekea apo lodge hiyo ni tarehe 7 tarehe ambayo wasimamizi wa guest inakuwa ni tarehe ya mwisho kwenda kulipia kodi ya mapato ya mwezi uliopita.

Na siku hiyo nilitoka kulipia kitabu manispaa ila tulikuwa na guest 2 zote hizo mimi ndio huwa naenda kulipia lazima ubebe kitabu cha wageni, wakati nimetoka kulipia pale manispaa ya Songea Mjini nilipoondoka guest ya kwanza ipo bombambili inabidi nipite hapo niache kitabu mi sikupita nikaona ntakileta baadae nikanyosha kuelekea ambako ndio hua nashinda

vitabu vipo kwenye begi ile kufika nikaacha begi kaunta nikasepa na mizunguko yangu.

Jioni iyo saa moja ndio natoka saloon kunyoa narudi nakuta gari tatu zipo pale ndani Toyota mayai nyeupe 2 na moja ni IST kijivu.

Nikapita zangu huwani sina ili wala lile nikaona kupitia dirisha muhudumu kabananishwa anaulizwa iki kitabu cha wapi mbona namba tofauti mnatumia vitabu viwili sio??
Kakosa jibu ameduwaa tu yule askari mkali kinyama jina lake maarufu LUKUBA sijui muhehe sjui mbena
Basi bana nikaona kumbe ishu ni kitabu ngoja niende nikawaelekeze nikajua wakaguzi tu wa vitabu nikaingia pale akamuuliza muhudumu
Meneja yupo wapi aliponiona akasema uyu hapa akaniuliza
Kitabu cha gest kipo wapi?? iki sio na manatumia vitabu viwili

Kumbe muhudumu alipoenda kwenye beg langu akachukua tu kitabu bila kuangalia na kuwaletea alafu beg lilikua na kitabu kingne cha gest iyo nyingne sasa ye alijua cha pale ndio akaleta.

Mi nikamwambia afande kitabu iki kakosea iki sio cha hapa mim nilijisahau Leo siku ya kulipia iki kitabu ilibdi nipitishe gest flani

akahamaki we brother mpumbavu acha ujanja brother Sawa kabla ya kuja uku unapita pale kivipi usahau acha masihara cha hapa kikwapi nikaenda kuchukua bana nipo na askari yupo na mtutu ananifata nyuma yule askari aliniambia dogo kua mkweli na usiseme uongo Sawa usiogope nikamwambia aina shida bro apo sijui tatizo kubwa ni nini mpaka mitutu.

nikaleta kitabu wakaangalia majina ya watu wao yalikuapo ila ya uongo sio ya ukwli na muda ule wateja walioingia awakuandikwa, na wahudumu usipokuepo wanapiga kwa mtindo huu awaandiki jina pesa kapuni mpaka ufatilie sasa iyo siku ndio ukawa msala.

Afande akasema meneja mzembe, we Dada bahati yako tungeondoka na wewe ila kaja uyu tunaondoka nae we utabaki du mungu wangu nakwenda selo,
saa moja jioni iyo nikajipa moyo sina kosa ntarudi bana.
Nikaingizwa kwenye IST tulikua na afande mmoja anaitwa victor pande la mtu black ivi kaenda hewani akasema meneja usihofu bana wala akuna shida.
yule afande mkali wakaingia gari nyingne nikawaona na jamaa flani ivi wamepigwa pingu wapo wawili usoni sikuwaona vizuri, safari mpaka kituo kikuu songea nikaingizwa kaunta pale nikawekwa chini nika ambiwa nivue viatu mkanda nikabizi na simu na kila kitu kilichopo mfukoni mwangu nikafanya ivyo nikaa kaa pale chini nilivaa soksi azikukakuka vizuri bana harufu iliyotoka hapo ilisamba pale pote nasikia askari nini hiki sijui mmoja akasema mhm kuna dogo kavua kiatu kachafua hewa.....ilikua balaa

Tuendelee kwenye point nika andika majina yangu pale kaunta afande yule aliuliza uyu ana kesi gani yule afande mnoko akajbu kuiba na kuvunja nikashangaa Mimi kuiba na kuvunja lini,
then nikapelekwa mahabusu for the first time katika maisha yangu jamaa walinipokea oya umekula msosi hapana sijala wakaniletea msosi bana
Ulikua ugali na dagaa bwana uo ugali ata bodingi school sikuwai ona wakati nasoma kummmke uji maunga unga tupu mboga dagaa maji chumvi mchuzi kibao aise ulinishinda kula nikasema hapana nimeshiba bana si ulisema ujala nikajbu Amna shida.

Ndani mahabusu nilimkuta bro wangu mtoto wa mama mkubwa upande mwingine wa uko kama unavyojua ndugu sometimes mkionana ndio apo apo alikua ana kesi yake ila sikuijua baadae niliijua.

nae ananishangaa dogo vipi umekula mtaji nini wa louge nikamwambia hapana bro ila nime andikiwa kesi ya kuiba na kuvunja
Sielewi chochote hapa,

tukatulia pale piga stori kidogo wanaletwa wazurulaji ma boda boda mpaka kukajaa mule ndani kuna muda watu wakamaindi ahaa umu tumejaa afande tunajibana
afande akasema sogeeni chooni uko watu wakagoma,
bana afande akasema msinizoee Sawa akaingia akatandika mtu kofi paaaa watu wakanywea wakasogea vile vichumba vimejaa.

naiti iyo, sasa nikajilaza sakafuni kichwa ukutani naangalia bati usingiz Amna jamaa wengne wapo na story tu kusogeza masaa pale ukutani nilipoweka kichwa walinipanda kunguni kichwani uzuri sikua na nywele kubwa nikawatoa wote nikalala katikati kwa kujibana ukuta nikauacha mbali yule bro wangu alinipa kopo la maji lina maji ndani ndio kama mto unaweka kichwani,
Apo nawaza watakuja sasa ivi kunitoa kimya.

Tumelala tupo ka biskuti ivi
Kumbe mshua alifika kunifata kituoni, uyu ni mshua wangu mkubwa ila sio baba mzazi na awajatoka tumbo moja na dingi ye kamuoa mama yangu mkubwa ambae ndio toka nitoke na mama yangu mzazi.

Alivyofika pale kaunta akauliza jina langu ibrahim akatajiwa ila Mimi niliandika jina la pili la babu na sio la baba hua najichanganya sana na uyu dingi nafikir alikua analijua jina la mzee wangu la kwanza tu akauliza ana kesi gani wakamwambia kuvunja na kuiba akaona haaaa sio yeye uyu kuiba na kuvunja wapi na wapi akasepa kwenda vituo vingine kunisaka.
Tena siku iyo usiku kulikua na mpira wa uefa juve na Manchester united afande baadae akaja akasema oya nyie wale wa mpira Manchester wamesinda 2-1 apo nikajua saa sita sasa ndio muda mpira unaisha ulianza SAA 4...............
Pause kidogo Ntarudi kuimaliza
Meneja mzembe!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom