Kodi ya Maendeleo(kichwa), Uzembe na Uzururaji...

Ili kukabiliana na aibu ya rais wetu kuzunguka kwenye mataifa za watesi wetu kuomba omba na pia kuiwezesha serikali yetu kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni kwanini serikali isirudishe kodi ya kichwa kwa kila mwananchi kuanzia at least miaka 25?
 
..mie nafkiri kodi ya tumbo inge sound zaid.. si ajua ndo kila kitu
 
cheap idea hizi mkuu, kama serikali isingezikabidhi resources zote kwa makampuni ya kigeni na kufanya effective utilization of resources mi nadhani kusingekuwa na hata kodi ya sigara wala pombe licha ya kichwa unayoiwadhia, mi nadhani tunaweza kuwa kila siku tunasema raisi dhaifu bila kuangalia huu udhaifu umeanzia kwetu wananchi kumdekeza huyu raisi wetu dhaifu. Ni hayo tu mkuu
 
Kwa taarifa yako, madhara ya watanzania kutokulipa kodi ni makubwa kulinganisha na madhara ya makampuni kutokulipa kodi, unapokuwa na wananchi ambao hawalipi kodi maana yake ni kwamba wananchi hao wanakuwa hawana interest ya kuidai serikali yao uwajibikaji.

Na ndio maana napendekeza kodi ya kichwa, natambua kila mwananchi analipa VAT, lakini kodi hii ni indirect na haina nguvu ya kutriger wananchi kuhoji matumizi ya kodi zao.

Hata tukisitisha uchimbaji wa madini nchini mwetu leo, lakini tukawa na serikali inayowajibika kwa wananchi tunaweza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
 
hivi mwajua kuwa 60% ya kodi inalipwa na na wafanyakazi na walaji wa mwisho? (final consumer). Mimi mshahara wangu nakatwa kodi karibu laki 7 kwa mwezi. Nikinunua kitu dukani nalipia vat. Walahi wakileta hiyo kodi ya kichwa huyo atakeye kuja nidai namkata kichwa.
 
cheap idea hizi mkuu, kama serikali isingezikabidhi resources zote kwa makampuni ya kigeni na kufanya effective utilization of resources mi nadhani kusingekuwa na hata kodi ya sigara wala pombe licha ya kichwa unayoiwadhia, mi nadhani tunaweza kuwa kila siku tunasema raisi dhaifu bila kuangalia huu udhaifu umeanzia kwetu wananchi kumdekeza huyu raisi wetu dhaifu. Ni hayo tu mkuu
Mimi sijui watu wengine wanafikiria kwa kutumia kitu gani. Kodi ya kichwa iliwahi kuleta maendeeo gani Tanzania? ...na huyo raisi unayesema anahangaika kututafutia misaada , ni misaada ipi hiyo ? Misaada aliyopewa hapa ya vyandarua vya mmbu, ndio misaada watanzania wanayoitaka? . Trilioni 11.3 zimeibiwa au kutumiwa vibaya na wafanyakazi wa serikali, wewe badala kuhoji hilo na hatua zilizochukuliwa, unataka watu wetu masikini ,fukara wa kutupwa waendelee kukamuliwa. Fikiri kabla ya kupost kitu hapa.
 
kodi ya kichwa ili iweje? wameshindwa kukusanya VAT 18% na PAYE 14-30 wataweza kukimbizana na fedha za walalahoi?
 
Ili kukabiliana na aibu ya rais wetu kuzunguka kwenye mataifa za watesi wetu kuomba omba na pia kuiwezesha serikali yetu kukusanya mapato ya kutosha kwa ajili ya shughuli za maendeleo ni kwanini serikali isirudishe kodi ya kichwa kwa kila mwananchi kuanzia at most miaka 25?

kweli wewe SANGARARA...huna upeo wa kufikiri.TANZANIA SI YA KUWA MASIKINI KAMA UNAVYODHANI.
 
Kwa taarifa yako, madhara ya watanzania kutokulipa kodi ni makubwa kulinganisha na madhara ya makampuni kutokulipa kodi, unapokuwa na wananchi ambao hawalipi kodi maana yake ni kwamba wananchi hao wanakuwa hawana interest ya kuidai serikali yao uwajibikaji.Na ndio maana napendekeza kodi ya kichwa, natambua kila mwananchi analipa VAT, lakini kodi hii ni indirect na haina nguvu ya kutriger wananchi kuhoji matumizi ya kodi zao.Hata tukisitisha uchimbaji wa madini nchini mwetu leo, lakini tukawa na serikali inayowajibika kwa wananchi tunaweza kupiga hatua kubwa sana kimaendeleo.
hivi wewe umeshawahi kusikia kuwa huku nyuma hii kodi ilikuwepo? Na kama unajua, je umeshawahi kufanya analysis yoyote kujua ni nini kilifanya wakaifuta au ikaondolewa? Ukishakuja na jibu sahihi ya swali hili naweza kuja na hoja kukufafanulia kwa nini nakwambia umeleta hoja dhaifu kama hii kwa wakati kama huu
 
Mimi naona irudishwe ili wananchi wawe na uchungu na fedha zao zikiliwa na mafsadi wa nchi hii na wawe tayari kufanya mapinduzi.
 
Rais dhaifu, Serikali dhaifu, Bunge dhaifu, wananchi dhaifu! Kazi tunayo!
 
Maendeleo hayaletwi na shilingi ya Tanzania. Ni fedha za kigeni ndizo zinazoleta maendeleo. Hata ukikusanya trilion elfu kumi, mshahara utakuwa mzuri lakini mafuta,magari, mashine na vitu vingine utavitoa wapi? Utajengaje madaraja na miundombinu mingine kama reli, bandari, usafiri wa anga, silaha bila kusahau viti vya ikulu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom