Amani na iwe kwenu wanajamvi!
Basi hata ilipotimia miaka mitatu baada ya vita vya Kagera,uchumi ulikuwa bado haujatengamaa! vijana wakawa wanakimbia vijiji vyao na kwenda mijini.Basi, mwalimu akaona namna ya kuwaondo mijini na kujenga uwajibikaji hasa miongoni mwa vijana, akatangaza bajeti chokonozi.kodi zikaongezeka maradufu na kodi iliyo kuwa maarufu enzi za mkoloni ikafufuliwa.iliitwa KODI YA KICHWA. Wakati ule ilikuwa ni shs 1500 kwa kichwa! yaani kila raia aliye timiza miaka 18 na ambae hayuko shule alitakiwa kulipa hiyo kodi.
Basi shs 1500 ya wakati ule ilikuwa ni kubwa sana na mbaya zaidi hata ukiwa na baiskeli ulitakiwa kuilipia kodi ya shs 500 kwa mwaka.Mijini ilikuwa ukikamatwa kwa koso lolote, kitu cha kwanza ungeulizwa umelipa kodi ya kichwa?Kama umelipa basi unaanza kuonekana kama raia mwema vile.mijini kulikuwa hakukaliki, vijijini hakukuwa na usumbufu sana, hivyo vijana wakitaka kuja mjini walitafakari mara mbili kabla ya kufanya uamuzi wowote.
Ikaja majira ya joto ya mwaka 1984, nasafiri kutoka shule kwenda likizo fupi ya mwezi Septemba, nikashuka kwenye gari nikajisogeza kwenye hoteli ya karibu nipate chai,Mara Mgambo kama watano wakanikamata, haya tuoneshe chiti chako kama umelipa kodi! nikawajibu sina.Kwa spidi ya umeme nikaingizwa kwenye gari lao,wakasema, twende wahujumu wa Nchi nyie.
Njiani nikawa nawasikia vijana wanasikitika, mmoja akasema aah tena nilikuwa sitaki kuja mjini mie, sasa ona nitaenda limishwa vibarua mie mpaka nipate kodi yao.Hawkuwa na namna ilibidi kodi ilipwe.
Mkubwa wa wale mgambo akanisogelea na kuniuliza, na wewe ni nani? nikamwambia jina langu na kwamba mimi ni mwanafunzi nasoma kidato cha tatu Malangali sekondari.Akamwita mkusanyaji kodi aniulize maswali kwa kiingereza ili athibitishe kama kweli ninasoma.Kumbe wamejiroga,Nikamwambia before you ask me anything let me tell you my history in brief! niliongea kwa tornation ya kimarekani kabisa, basi yule mkubwa wao akasema kumbe kweli anasoma, mpeni begi lake aende.
Hali ile ingeendelea na kiwango cha kodi ya kichwa ikaongezwa, unafikiri kuna mtu angecheza pool asubuhi? unadhani watu wanekimbilia kuja mijini bila kujipanga? Karibu tena kodi ya kichwa!!!