Bombabomba
JF-Expert Member
- Dec 23, 2017
- 1,725
- 2,008
Nikiwa Mwanafunzi wa SM miaka ya 80s nilianza kupata adha ya kodi hii kwa kushuhudia watu wazima wakibaki ndani ya nyumba siku nzima kujificha. Msimu wa maembe mwezi Desemba walikuwa wakishinda mashambani/mafichoni wakila maembe siku nzima. Nilijiuliza kwa nini wakamatwe?
Nilivyomaliza form VI nilitumia kitambulisho changu miaka 3 mbele kujiokoa dhidi ya ulipaji kodi lakini Juni 30, 2001 mgambo walinivizia home saa 9 usiku nikijipanga kutorokea vijijini kukusanya mazao nikakamatwa. Nikalazimika kulipa kodi na adhabu pia na kipande cha baiskeli na kuishiwa mtaji.
Julai Rais Mkapa aliifuta kodi hii sumbufu. Kulikuwa na Migambo wababe sana kizazi kile. Kiukweli sitasahau adha hii maishani mwangu.
Karibuni wahenga tujikumbushe Maisha yale ya kukamatwa na Migambo kwa kushindwa lipa kodi.