KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Cardinal Pengo aliwahi kusema anaijua biblia kuliko watu wengi nchini na haikatazi pombe.
Mbele kwa mbele.
Huko Ulaya walutheri tena wachungaji wanakunywa bila shida
Nasubiria kwa hamu na katazo la kutooa mke zaidi ya mmoja...
 
Hakuna katika Qur'an tukufu inaporuhusiwa kunywa pombe baba wa maasi! Kwani mtu huleweshwa na alcohol ndani ya pombe au ethanol?
 
waumini wa madhehebu ya ulokole hawatofautishi unywaji na ulevi. huona kunywa pombe ndio dhambi kuu, wakati kuna matendo machafu wanayafanya na kuwasumbua kwa kulia makanisani usiku kucha wanapoyakumbuka. hakuna mstari ktk biblia unaokataza unywaji, bali ulevi.
 
Divai ni kinywaji kinachotokana na zabibu, ukitaka unaweza kuitumia kutengeneza pombe. Ila divai aliyotoa Yesu haikuwa fermented kuwa pombe. Umesoma wapi kwamba watu waliokunywa ile divai aliyotengeneza Yesu walilewa? Usipotoshe Biblia kwa kuongeza maneno yako. Swala la Nuhu liko wazi kabisa alitenda dhambi na kitendo kilichofanyika baada ya Nuhu kunyweshwa pombe ndicho kikuonyeshe kuwa pombe ni kitu haramu na hatari maana kila aliyekitumia hata kwenye Biblia anaonyeshwa madhara gani aliyoyapata.soma Habakuki 2:15-16. Anayekunywa pombe Biblia inamtaja kama mtu asiyetahiriwa (Mpagani/ asiyemcha Mungu)
Kama Nuhu alitenda kosa kwa kulewa kwa nn laana ilielekezwa kwa watoto wake na siyo kwake yeye mwenyewe,,,,,,,? Maana nakumbuka walilaaniwa tu watoto kwa kosa la "kutokusitiri" baba yao. Kwa nn hakulaaniwa mlevi mwenyewe,,,,,?
 
Labda twende kimaandiko ni wapi imeandikwa kunywa pombe ni dhambi..
Namuona katika biblia bwana Yesu akibadili maji kuwa divai kwenye ile harusi ya kana.walipoionja wakasema kwanini bwana harusi ameficha mnvinyo mtamu akaleta mbaya? Maana watu huleta mnvinyo mzuri kwanza ,watu wakilewa ndiyo huleta ule mbaya.
 
Pombe na kanisa au ukristo vinaanzia mbali tangu muujiza wa kwanza kwenye harusi ya kana.
Hata hivyo, kwa kuwa washika dini wengi ni wanafiki, wakieneza dini kwa uongo wa kutunga, siyo rahisi kupata muafaka.
Wanapeana pombe yenye kilevi zaidi ya bia (divai/wine ) wakifananisha na damu ya Yesu huku bia wakiilaani kama kilevi zaidi.
 
Huku Bayern beer ni chakula hata wakati wa breakfast unapiga Weissen beer na Weiss wurst. Wakati wa kazi unaruhusiwa kwa siku beer chupa mbili.
Bayern ni mjj,mtaaa au ,,,,,msje mkasema huku chelsea na arsenal DDDDD
 
Kujiua ni dhambi itakayokutia motoni na hivyo makazi yako ni motoni. Sasa iweje ujiue kwa cirrhosis kutokana na pombe halafu ionekane ni kawaida? Au Mwenyezi Ezi Mungu anasema uongo?
Lakini katika Qur'an kuna ahadi kwamba Waumini watakaofaulu kuingia Akhera watakuta mito inayotiririsha maziwa na Mvinyo mzuri sana.

Au utabisha na hili?
Hakuna katika Qur'an tukufu inaporuhusiwa kunywa pombe baba wa maasi! Kwani mtu huleweshwa na alcohol ndani ya pombe au ethanol?
 
kwa hiyo wasiokunywa pombe hawafanyi maasi?
Haina maana hiyo. Pombe inakupelekea hata unisaidie mbele ya wanao unapokuwa an addict to it. Nipe faida moja ya pombe mbali na kukupa calories ambazo elimination yake ni shida tupo. Hata ambao hawanywi pombe hufanya pia maasi.
 
Unapata madili kwenye pombe,,,chaaaaa
 
Ndugu kumbuka utasimama peki ako mbele ya hukumu na hutamwambi Mungu niliambiwa pombe si dhambi maana wao wanajua zaidi maadii ya Ukristo kuliko sisi kumbuka adam alivojitetea lakini aliadhibiwa so hata hawa viongozi wanaweza kukuangamiza bila kujua kila mtu anapaswa kujua kwa undani anachoamini kwa kusoma neno la Mungu, binafsi maana kila mtu atajibu yake so tujiongeze.Pombe ni dhambi maana ina kilevi na walev wote moton period.
NENO
 
Hapana hapa black and white malasusa na kubenea wa ugomvi kitambo sana ko hzo ni hila za kuchafuana
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Asante baba Askofu tusaidie hata Bangi iruhusiwe maana vyote ni vya Mungu,,,,,,,,,,!
 
( مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ )

محمد (15) Muhammad

Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na magh**** kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?

Quran inasema kuna mito ya chang'aa huko peponi na inafaa kunywewa na nani?.
Huko full mipombe.
Bibles inasemaje??

Habakuki 2 : 15 - Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Biblia inakataa pombe kabisa rafiki

Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
ATAPOKE MARA MIA !

Yaani kama uliacha mke mmoja hapa duniani kwa ajili ya jina lake huko utapokea mara mia yake...

Tena baada ya kupokea vimada 100 mmeahidiwa na kugonga beer yaani...

Mark 14:25Living Bible (TLB)
25 I solemnly declare that I shall never again taste wine until the day I drink a different kind[a] in the Kingdom of God.”

Kumbe wanawake na pombe mtapata huko ?
Sasa mnazuga nini ?hamtaki tuje kufaidi huko nn ?
 
waumini wa madhehebu ya ulokole hawatofautishi unywaji na ulevi. huona kunywa pombe ndio dhambi kuu, wakati kuna matendo machafu wanayafanya na kuwasumbua kwa kulia makanisani usiku kucha wanapoyakumbuka. hakuna mstari ktk biblia unaokataza unywaji, bali ulevi.
Baadhi ya walokole wanapiga sana kelele kuhusu pombe lakini ni wezi wakubwa wa hela na wazinzi waliokubuhu.
Kipi afadhali?
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.
Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”
Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.”
Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”
Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”
Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano.
Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?”
Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.
Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe.
Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT.
Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.
Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.
Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.
Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.
Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.
Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.
Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake.
Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.
Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake.
Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Back
Top Bottom