Askofu Malasusa: Kuna watu jamii ikikaa kwa amani wanaumia

Askofu Malasusa: Kuna watu jamii ikikaa kwa amani wanaumia

gallow bird

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2024
Posts
14,068
Reaction score
17,502
Katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya maaskofu wa kanisa lile walioamua kuwa wanasiasa,askofu dkt malasusa amesema kuna watu hawapendezwi na jamii kukaa kwa amani
Wale wa kanisa lile wameshindwa kung'amua kuwa huwezi tafuta haki pahala pasipo amani,licha ya kusifiwa kuwa na elimu za chuo kikuu tena kuukuu, ilhali masheikh wasio hata na elimu ya a level kirahisi wameng'amua hilo
Katika Misa za noeli, viongozi hao wameonekana kusisitiza kupigania haki,wakidai kushindwa 'kutoka' na kupigania haki kwa mkiristo si sawa

===

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu, Dk. Alex Malasusa amekemea tabia za baadhi ya watu za kuchafua taswira za watu wengine, pamoja na kuichonganisha jamii.

Ameyasema hayo leo katika ibada ya Sikukuu ya krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es Salaam.

“Kuna watu wakiona jamii imekaa pamoja kwa amani wao inawakosesha raha.”

Source NIPASHE Digital
 
Katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya maaskofu wa kanisa lile walioamua kuwa wanasiasa,askofu dkt malasusa amesema kuna watu hawapendezwi na jamii kukaa kwa amani
Wale wa kanisa lile wameshindwa kung'amua kuwa huwezi tafuta haki pahala pasipo amani,licha ya kusifiwa kuwa na elimu za chuo kikuu tena kuukuu, ilhali masheikh wasio hata na elimu ya a level kirahisi wameng'amua hilo
Katika Misa za noeli, viongozi hao wameonekana kusisitiza kupigania haki,wakidai kushindwa 'kutoka' na kupigania haki kwa mkiristo si sawa
Gallow
Dunia nzima inajua watu gani ni "Source" ya watu ambao hawapendi amani duniani. No speculation, TEC of all hawana hiyo hulka, aidha tu unataka kusema uongo.

Fungua makabrasha, duniani nani ni adui wa Amani, sina haja ya kusema!!
 
Hivi kwa wale wengine wenye phD huko hakuna maofisa kipenyo? maana mnasema dola ni kubwa na pana ipo mpaka ndani ya dini. Sasa mbona kuna ligi na wale wengine?
 
Back
Top Bottom