KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Unaonekana kuwa na uelewa mdogo au bifu kwa Askofu Dr. Malasusa

Kilichokataliwa katika Biblia Takatifu ni "ULEVI"

ULEVI hata wa Chakula kingi ni dhambi kabisa kama ilivyo Uzinzi, Wizi n.k

Unaweza kunionesha mstari wowote katika biblia unaokataza POMBE?
haupo mkuu ndio maana watu walikua wanagonga mvinyo tu kipindi cha yesu..
hata biblia inasema 1 timotheo 5:23
23.Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara
 
Mumwache Askofu wetu,kama unaona ana makosa uwe wa kwanza kwenda kumwambia na kumhukumu ila hakikisha wewe ni msafi.Matayo 15:11 inasema kimwingiacho mtu sio najisi bali kimtokacho.
Mwombee Askofu tena mwombee sana Mungu pekee ndio anayejua hakupata cheo kwa bahati mbaya.
 
Mumwache Askofu wetu,kama unaona ana makosa uwe wa kwanza kwenda kumwambia na kumhukumu ila hakikisha wewe ni msafi.Matayo 15:11 inasema kimwingiacho mtu sio najisi bali kimtokacho.
Mwombee Askofu tena mwombee sana Mungu pekee ndio anayejua hakupata cheo kwa bahati mbaya.
AMINA.
 
Unaonekana kuwa na uelewa mdogo au bifu kwa Askofu Dr. Malasusa

Kilichokataliwa katika Biblia Takatifu ni "ULEVI"

ULEVI hata wa Chakula kingi ni dhambi kabisa kama ilivyo Uzinzi, Wizi n.k

Unaweza kunionesha mstari wowote katika biblia unaokataza POMBE?
Hawa hawachoki kumsakama askofu huyu mtumishi wa Mungu.
Mafundisho ya Manisa Katholic hayakatazi pombe, mbona hawasemi. Zambi IPO kkkt tu?
Mlivowashamba, kwanini pale kwenye mkutano aliongelea habari za tuhuma za "ngono" zimekujaje hapa.
Hamshindani na Malasusa, mnashindana na Ufalme wa Mungu.
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Kwa taarifa yako hata "Yesu" anitambua pombe. Nakumbuka alienda kwenye harusi, watu wakaishiwa divai, akaagiza maji yakaletwa halaf akabariki "watu wakanywa wakalewa kweli kweli,,,,! Nuhu mwenyewe aliwahi kunywa akalewa ila sikuwahi sikia kwamba" Nuhu alitenda dhambi ya kulewa",. Asante,,,
 
Mtoa madam naomba umetengenezwa, kwangu mambo mango umetia chumvi. Mango duals la Katiba na muda wa askofu Kuala madarakani haikuwa sehemu ya agenda isitoshe kanuni ya KKKT SMP unaweza vizuri juu ya jambo hilo.
 
Kwa kuwa pombe inasabisha ULEVI na ulevi huondoa ufahamu kwa mlevi basi haifai kunywewa.Madhara ya ulevi wa pombe ni mengi na yanajulikana.HEKIMA na BUSARA haipo kabisa kwa mtu aliyelewa pombe.Zipo kampeni za kupinga ulevi wa pombe kwa jamii.
Hapo ndio mnapojitoa ufahamu. Pombe haindoi ufahamu bali ulevi. Alafu Biblia haijipingi hivyo ni vema kusoma mistari yote ili kujua kusudio la Mungu. Jiulize kwanini maandiko yanasema Askofu awe mtu wa mke mmoja na asitumie mvinyo lakini pia inasema mashemasi watumie mvinyo kidogo. Unafikiri Biblia imejipinga? Ni vyema kujipima mwenyewe ...ukiona ukipata chupa mbili tayari hujiwezi achana na pombe. Wengine wanakunywa kwa wastani kufurahia maisha then wakiwa na akili zao timamu wamevunja amri ipi? Tulishatolewa kwenye sheria za usiguse, usile, usinywe ....sasa dhambi zetu zinaandikwa mioyoni mwetu.
 
Kwa taarifa yako hata "Yesu" anatambua pombe. Nakumbuka alienda kwenye harusi, watu wakaishiwa divai, akaagiza maji yakaletwa halaf akabariki "watu wakanywa wakalewa kweli kweli,,,,! Nuhu mwenyewe aliwahi kunywa akalewa ila sikuwahi sikia kwamba" Nuhu alitenda dhambi ya kulewa",. Asante,,,
 
je soda tunayokunywa ya cocacola haina kilevi?

Je chai ya rangi?
Mkuu sio hivyo...

Tukirudi kwenye Physiology point of view pamoja na Biochemistry hasa kwenye topic ya Alcholoc metabolism...

Chakula tunachokula mpaka kiwe-converted kuwa energy yaani ATP, lazima ipite kwenye mzunguko unsitwa Creb cycle...

Sasa kwenye mwili starch inapoanza kuwa Converted kuwa Glucose then ipite kwenye Glycolysis mpaka tuje tuapate ATP, hapo katikati tuna-produce traces za Alcohol nyingi mno...

Kwakifupi ni kuwa mwili wetu kila tunapokula,mmengenyo wa chakula huwa unatengeneza pombe kila siku....

Ukila plate ya matunda mchanganyiko, ndugu pombe unayotengeneza mwilini ni balaa..

Watu waache unafiki
 
Mbona malkia wa sheba alituletea hili zao, lakini halibarikiwi.
IMG-20150724-WA0001.jpg
 
Kwa taarifa yako hata "Yesu" anitambua pombe. Nakumbuka alienda kwenye harusi, watu wakaishiwa divai, akaagiza maji yakaletwa halaf akabariki "watu wakanywa wakalewa kweli kweli,,,,! Nuhu mwenyewe aliwahi kunywa akalewa ila sikuwahi sikia kwamba" Nuhu alitenda dhambi ya kulewa",. Asante,,,
Divai ni kinywaji kinachotokana na zabibu, ukitaka unaweza kuitumia kutengeneza pombe. Ila divai aliyotoa Yesu haikuwa fermented kuwa pombe. Umesoma wapi kwamba watu waliokunywa ile divai aliyotengeneza Yesu walilewa? Usipotoshe Biblia kwa kuongeza maneno yako. Swala la Nuhu liko wazi kabisa alitenda dhambi na kitendo kilichofanyika baada ya Nuhu kunyweshwa pombe ndicho kikuonyeshe kuwa pombe ni kitu haramu na hatari maana kila aliyekitumia hata kwenye Biblia anaonyeshwa madhara gani aliyoyapata.soma Habakuki 2:15-16. Anayekunywa pombe Biblia inamtaja kama mtu asiyetahiriwa (Mpagani/ asiyemcha Mungu)
 
Ila wakuu tukiacha mambo haya ya Pombe!

Nimerejea kwa kifupi hili bandiko nikaona limeletwa kumchafua Askofu Malasusa ....Ila wametumia gia na Kanisa na pombe ili kuvuta wasomaji wengi...

Gazeti la Mwanahalisi limekuwa kinara wa kumchafua Dr. Malasusa...Sijajua ni kwanini...?
 
( مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ )

محمد (15) Muhammad

Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na magh**** kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?


Quran inasema kuna mito ya chang'aa huko peponi na inafaa kunywewa na nani?.
Huko full mipombe.
Bibles inasemaje??

Habakuki 2 : 15 - Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Biblia inakataa pombe kabisa rafiki
Mimi naona hapo Habakuki kuna "kulewa" hadi kuwa uchi! Sawa na kula hadi ukavimbiwa kiasi cha kupigwa bomba "enema" ili upumue
 
Kujiua ni dhambi itakayokutia motoni na hivyo makazi yako ni motoni. Sasa iweje ujiue kwa cirrhosis kutokana na pombe halafu ionekane ni kawaida? Au Mwenyezi Ezi Mungu anasema uongo?
 
Point moja aliyoitoa Malasusa ni hii. Wamisiomari kwa busara zao walikataza pombe baada ya kujua sisi Waafrika hatuna kiasi. Huu ndio ukweli.

Sisi Waafrica ni Walafi na kwa hivyo kiasi kwetu ni msamiati. Wazungu tunawaona wakija kwetu na kugawana BIA moja watu wawili. Sisi tukipata PESA tunataka tufie bar
 
Back
Top Bottom