Nimejaribu kuisoma habari hii, ila naona tatizo sio pombe au vitendo vya kitabia vya Askofu tatizo ni NAFASI YA UASKOFU, jamani wachungaji wa KKKT wengi wanafahamika wapo kweli wa kiroho lakini wapo waliowengi ambao wanajulikana fika nitashangaa kama hao ndiyo miongoni mwa wanaonyoosha vidole na kujitweza utakatifu, nafikiri kilichopo hapo ni hoja iliyopo kuhusiana na POMBE je bibilia inasemaje kuhusu pombe? Je sakrament inayotumiwa na KKKT haina kilevi? kama kipo kwanini Kanisa waruhusu kitu chenye kilevi kitumike kama sakramenti? Tupate majibu kutoka biblia ili kuanzia hapo tumuulize Askofu hicho anachosema amekipata wapi? Kilichomponza Askofu huenda ni kuwa mkweli,siamini kama Askofu hajui maandiko kwa kiasi hicho.
Nimepita tu jamani