KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Huku Bayern beer ni chakula hata wakati wa breakfast unapiga Weissen beer na Weiss wurst. Wakati wa kazi unaruhusiwa kwa siku beer chupa mbili.
 
HIZI NI DINI TU JAMANI....!

Bila kujali Kiongozi wa dini anasema nini!
Kuna wakati unatakiwa ufanye maamuzi kulingana na IMANI yako.
Ukiona kulingana na misingi ya Imani yako..
Unywaji wa pombe ni sawa.. Kunywa.. tu!
Ukiona sio sawa Usinywe..

Kila mtu atabeba msalaba wake.. Utakuwa peke yako hiyo siku.
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Mkuu hamna sababu ya kutokea na povu namna hiyo, unapaswa kujibu kwa reference, wapatie wadau mstari kwenye biblia unaozuia matumizi ya pombe ili hoja yako iwe na mashiko na tujue kama kweli askofu Malasusa anapotosha au kuna genge la watu wanamchafua tu
 
Malasusa amepitia mengi sana mpaka sasa kiasi kwamba akishindwa kuyamanage yanaweza kuharibu legacy yake yote. Namkumbuka Jerry Mngwamba alivyoondoka kwa aibu miaka ile ya 1999
 
Mungu Wenu mwenyewe Anawalazimisha Mnywe, Mlewe, Muanguke, Mtapike Wala Msiinuke Tena, Hiyo Ndio Amri Ya Mungu Wenu Kwenu Nyinyi Wagalatia (Wakristo)

Yeremia 25:27~28
27 Nawe utawaambia hivi, Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nyweni, na kulewa, na kutapika, na kuanguka msiinuke tena, kwa sababu ya upanga nitakaoupeleka kati yenu.
28 Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.****

Sasa mcungaji kakosea nini ?
 
Katika habari yote.nimependa jina LA askofu tu.keshomshahara.
Hilo jina mkuu design kama la kipwani kama majina mengine ya kiroboto, chausiku, dunia pembe n.k amazing majina mazuri ya kiswazi hayo
 
kama anakashfa ya ngono askofu madem wamemtoa ufaham mpaka anahalalisha pombe ambayo mwanzo ilikua haram! anatumia kitabu kipi?
 
Pombe inakatazwa!
Isaya 28:7 kileo humfanya mtu kumkosea Mungu.
Hosea 4:11 pombe huondoa fahamu,ndiyo maana wanajinyea
Hosea 4:18 pombe huchochea zinaa.
1kor 6:9-10 walevi mbinguni si kwao
waefeso 5:19-21 matendo amboyo ni dhambi ni pamoja na ulevi wa mvinyo.HUKUNA sehemu yeyote ya kuverify kwamba timotheo aliambiwa anywe pombe kwa kutibu tumbo.
 
Pombe inakatazwa!
Isaya 28:7 kileo humfanya mtu kumkosea Mungu.
Hosea 4:11 pombe huondoa fahamu,ndiyo maana wanajinyea
Hosea 4:18 pombe huchochea zinaa.
1kor 6:9-10 walevi mbinguni si kwao
waefeso 5:19-21 matendo amboyo ni dhambi ni pamoja na ulevi wa mvinyo.HUKUNA sehemu yeyote ya kuverify kwamba timotheo aliambiwa anywe pombe kwa kutibu tumbo.
 
Sio Kweli.

Pombe ni Kinywaji

Ulevi ni hali anayopata mtu baada ya kunywa pombe nyingi. Pia ni tabia.
Kwa kuwa pombe inasabisha ULEVI na ulevi huondoa ufahamu kwa mlevi basi haifai kunywewa.Madhara ya ulevi wa pombe ni mengi na yanajulikana.HEKIMA na BUSARA haipo kabisa kwa mtu aliyelewa pombe.Zipo kampeni za kupinga ulevi wa pombe kwa jamii.
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Hilo la kubariki pombe kwa wakristo ni lako mtoa mda na gazeti la udaku la MwanaHalisi.
Ukweli utabaki pale pale, pombe ni chakula kitumiwe kwa busara kama unavyo shiriki Chakula Cha Bwana kwa faida yako.
 
Kwa kuwa pombe inasabisha ULEVI na ulevi huondoa ufahamu kwa mlevi basi haifai kunywewa.Madhara ya ulevi wa pombe ni mengi na yanajulikana.HEKIMA na BUSARA haipo kabisa kwa mtu aliyelewa pombe.Zipo kampeni za kupinga ulevi wa pombe kwa jamii.
Pombe inasababisha ulevi pale inapozidishwa na mtumiaji

Pia pombe inaweza kitumiwa kidogo kama dawa na si kilevi

Unalijua hilo?
 
Back
Top Bottom