KKKT labariki unywaji wa Pombe

Walutheri pombe hunyweka kama kawaida hakuna katazo wala fundisho la unywaji pombe.Wasiokunywa pombe ni wapentekoste,akitokea kiongozi wa madhehebu ya kipentekoste anashadidia unywaji pombe jamii ya wakristo wa kipentekoste watashangaa sana juu ya fundisho la kunywa pombe.
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Mazara ata chakura kina mazara
 
Wakristo na unafikisijui mtauacha lini,hivi ule mnvinyo wa chakula cha bwana si ni pombe kabisa na hata madukani ipo inaitwa altar wine?
 
Shida ni kuwa watu wanachanganya neno POMBE na neno ULEVI. Kilicho dhambi ni ulevi na sio pombe. Pombe ikitumika vizuri kwa makusudio yake ni jambo la kheri kabisa kwa mwanadamu, lakini ikitumika kama ulevi ni katazo kwa Mungu.
Hata Madaraka yaweza kutumika kama ulevi na kuleta madhara jee madaraka nayo ni dhambi? Kwa sababu Pombe na Madaraka vyote ukivitumia vibaya vinakuwa ulevi!
Kunywa pombe kistaarabu, burudisha nafsi yako. Na hasa kwa wakati huu ambao mambo ni vululu vululu kiuchumi basi ukipiga mbili tatu zako taratibu unajikuta unaburudisha ubongo na kukuepusha na ghadhabu au chuki kwa wengine.
Watu wanasahau kwamba hata kuzidisha pilau ni dhambi. Pombe kiasi kama kinywaji au chochote si dhambi!
Hao walutheri was Ujerumani wanakunywa pombe. Ndiyo waliotuletea dini yenyewe.
 
Juzi nilialikwa kwenye. Misa moja huko shinyanga,ilikuwa ikifanyikia nyumbani kwa mtu! Basi baada ya Misa ukawadia wasaa wa misosi na vinywaji,baada ya mlo vijana wakaanza kusambaza vinywaji mchanganyiko,pale mbele kwenye meza kuu alikuwepo padri,zikapelekwa kreti mbili za bia,padri akafunuliwa chupa ya Safari lager! Akaipiga paaaaap!! Ikabaki nusu! Akairudia tena paaap!! Ikawa empty!! Jamaa aliyeandaa Misa hiyo akanniita nikajumuike nao hapo mbele nikamwambia tu asante mkuu!!japo nnnnilikuwa natamani ila nisingekuwa comfortable kuchapa kinywaji na mtumishi wa Mungu.
 
Nahisi kama kuna something behind kuhusu imani ya kikristo kinafichwa. Ila naamini ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Siamini unachokisema Kw
 
Nahisi kama kuna something behind kuhusu imani ya kikristo kinafichwa. Ila naamini ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.
Naamini wale waliokuja kuleta neno ndio walikuwa wanaweka kanuni zao kulingana na eneo. Huku walijua kabisa ulabu ndio chanzo kikuu cha matendo maovu wakaona watafute njia ya kupunguza kwa kuutamka kabisa kuwa ni dhambi kwetu waafrika.
Nasikia hata wahubiri walipoenda kwa Waeskimo Kule kwenye baridi Kali ikaonekana ukiwaambia kuwa dhambi itakupeleka kwenye moto wa milele kwao ni kama unawaambia humo kuna maisha mema kwani wamechoka na baridi hivyo wakaambiwa unatupwa kwenye shimo la barafu na hadi Leo wanaiogopa dhambi kwa sababu za shimo la barafu
 
Kijana wa mudy umesemaje?
Mkuu ungejua imani yangu ,ungejishangaa kwanini umesema hivyo,miaka kadhaa nikisali ukonga hapo kanisa fulan nilienda kushiriki meza ya bwana,ile kumaliza kupiga ule mnvinyo nilipepesuka na hata nikasahau nilipokuwa nimekaa,mpka baada ya muda ndo nikagundua
 
tuendelee kufanya yetu
 

Attachments

  • beer-froth.jpg
    beer-froth.jpg
    40.8 KB · Views: 54
Yuko sawa maana hata bible imeruhusu...

1 TIMOTHEO 5:23 ‘’’ Tokea sasa usinywe maji tu
mia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.’’’

PAULO HAWAAMBIA WAKRISTO WANYWE POMBE ETI POMBE NI TIBA YA MAGONJWA.
 
Walutheri pombe hunyweka kama kawaida hakuna katazo wala fundisho la unywaji pombe.Wasiokunywa pombe ni wapentekoste,akitokea kiongozi wa madhehebu ya kipentekoste anashadidia unywaji pombe jamii ya wakristo wa kipentekoste watashangaa sana juu ya fundisho la kunywa pombe.
 
huko mi naona hawanaga msimamo wengine pombe haramu wengine
inafaa ulaya ndoa za jinsia moja zinafanyika makanisani
afrika haifai wengine kitumoto halali wengine haramu
wote mnafata biblia moja ama kila kundi lina yakwao kwa matakwa yao?
 
Yuko sawa maana hata bible imeruhusu...

1 TIMOTHEO 5:23 ‘’’ Tokea sasa usinywe maji tu
mia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.’’’

PAULO HAWAAMBIA WAKRISTO WANYWE POMBE ETI POMBE NI TIBA YA MAGONJWA.
( مَّثَلُ الْجَنَّةِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۖ فِيهَا أَنْهَارٌ مِّن مَّاءٍ غَيْرِ آسِنٍ وَأَنْهَارٌ مِّن لَّبَنٍ لَّمْ يَتَغَيَّرْ طَعْمُهُ وَأَنْهَارٌ مِّنْ خَمْرٍ لَّذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ وَأَنْهَارٌ مِّنْ عَسَلٍ مُّصَفًّى ۖ وَلَهُمْ فِيهَا مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ وَمَغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ ۖ كَمَنْ هُوَ خَالِدٌ فِي النَّارِ وَسُقُوا مَاءً حَمِيمًا فَقَطَّعَ أَمْعَاءَهُمْ )

محمد (15) Muhammad

Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?


Quran inasema kuna mito ya chang'aa huko peponi na inafaa kunywewa na nani?.
Huko full mipombe.
Bibles inasemaje??

Habakuki 2 : 15 - Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Biblia inakataa pombe kabisa rafiki
 
Back
Top Bottom