Kwenye Dini ya Kikristo hasa kwa viongozi wakuu kama maaskofu. Matamko yao yana leta adhali sana katika ustawi au kutokustawi kwa kanisa.
Watu hawajui Theolojia ya dini ya kikristo(Elimu) ni kitu kizuri sana lakini pia ni kibaya sana.
wachungaji wanaoenda nje kusomea elimu ya dini (theolojia) ukiwauliza watakwamba kwamba wanapata wakati mgumu sana kuhusu baadhi ya mafundisho katika Biblia.
Kunywa Pombe sio dhambi ila ni maadili ya kanisa waliyojiwekea. Yesu alipo tengeneza Divai SIO juice Bali Ilikuwa POMBE. WENGI wachungaji wanahangaika bure na hili kwa kukwepesha kwepesha ilikuwa ni pombe.
Kunywa Pombe kwa waamini sio dhambi na bado huyu mtu atakwenda mbinguni. shida ni kwamba pale mtu anapoitumikia pombe inapochukua nafasi ya Mungu.(kwa kutokufanya mapenzi ya Mungu kwa sababu ya Pombe).
Katika Biblia hauna sehemu palipokatazwa kunywa pombe isipokuwa kuna maangalizo tu kwa watu maalum kama viongozi wa kanisa wasitumie pombe kwa maana hawatakuwa sahihi katika kutoa maamuzi (Si unakumbuka Mzee wa Upako angekuwa mtu mwingine ambaye hana cheo au si kiongozi wa dini lilikuwa ni jambo dogo sana).
Hata hivyo waamini ndiyo wanaharibu kanisa. Siku moja Askofu mmoja aliwahi kusema ushoga ni dhambi lakini si tofauti na dhambi zingine kama uongo, ugomvi,uuaji nk, kwa hiyo waacheni mashoga wawe makanisani watabadirika kama waongo na wafiraji na waasherati na wazinzi wanavyobadilika wakiwa makanisani" Huyo askofu alisuswa mpaka alipofariki wakimshutumu ni mwenye dhambi kwa kutamka hivyo.
u
Nilitaka kusema tangu. Tuwasililize viongozi wetu wa dini, kwa maana wao wanajua zaidi maadii ya Ukristo kuliko sisi.
NB: Sishangai kabisa nikiona kanisa la KKKT likikatika vipande vipandi kwa sababu viongozi wao wote wanapelekwa kusoma elimu ya Dini Ujerumani ambapo hao ualimu wao hawamwamini Mungu, inaamini ushoga na haki za binadamu.