KKKT labariki unywaji wa Pombe

KKKT labariki unywaji wa Pombe

Kama unaweza kutofautisha unywaji na ulevi wewe kunywa tu, ila kama huwezitofautisha acha kugusa hata matangazo ya pombe usisome.
 
Ila siku hizi bhana,kila mtu anatafsiri biblia kwa interests zake....mwingine alisema kuoa wake wawili sio dhambi,endeleeni tu kuhalalisha Ila Mungu hapendi
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Hiv kile Yesu alichobariki kwenye harus ya kana ninin
 
Otorong'ong'o ,
Kwanza ujue sina mpango wa kubadili mtu anachoamua kuamini juu ya jambo lolote. Kwangu mimi jukumu langu ni kuusema ukweli na kila mtu aamue yeye mwenyewe. katika miaka yangu yote ya kusoma maandiko hakuna mahali nimekutana na andiko likiongelea vizuri kuhusu pombe na ulevi. Hakuna!
1. Baada ya kupona na gharika Nuhu alilewa akakaa uchi
2. Ajali nyingi sana na maamuzi ya kijinga yanatokana na Pombe.

Najua argument yako ni pombe sio mbaya bali ulevi. Ulevi unatokana na kunywa pombe. Unasema kunywa kiasi si dhambi. Bahati mbaya Biblia haijasema hivyo na hakuna kipimi cha kiasi. Je Mungu akiwa anahukumu siku hiyo atatumia kipimo gani kujua nilipita "kiasi"? Kiasi ni kipi na ni kwa andiko gani? Ulevi ni dhambi iwe wa Chupa moja au nusu glasi.

Nimeomba maandiko yanayoruhusu kwa sababu ninajua hayapo. "Nabii" Tito wa posta naye alikuwa hivyo hivyo lakini pamoja na kuwa "nabii" naye alikosa andiko akaja na hilo hilo.

Tim 5:23 hairuhusu Pombe kwa maana ya Safari Lager, John Walker, Vodka au Sijui nini Wine. Inaruhusu Tomotheo kunywa Mvinyo kama sehemu ya dawa. Na leo tuna dawa nyingi tu zenye pombe ndani yake. Lakini hatunywi kujitafutia furaha humo, la Hasha! Tunakunywa kama dawa kama ilivyokuwa kwa Tim.

Hiyo ya Yesu hata sio ushahidi. Neno la Kigiriki lililotumika ni ambiguous kwa maana linaweza kumaanisha Divai au Mvinyo. Hatujui ni aina gani ya Divai Yesu alitengeneza kutoka katika mstari huu.

Kwa kuongezea tu Mungu anawazaje juu ya Pombe hebu tazama mistari hii:
Walawi 10:8-9 - "Kisha Bwana akanena na Haruni, na kumwambia, Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;

Hesabu 6:3 - [Mnadhiri] atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.

Waamuzi 13:4 - [Mama yake Samsoni] Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

Isaya 5:11 - Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!

Isaya 5:22 - Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;

Mingine iko kwenye Biblia yako utaipitia!

Ukweli ni kwamba kitu pekee ambacho kinawafanya watu wapende Pombe ni sawa kabisa na kile kinawafanya wengine wavute sigara au madawa ya kulevya. Nacho ni kutafuta furaha na kutosheka. Mungu anaichukia Pombe kwa sababu anataka furaha na uteshelevu wetu uwe kwake. Ndio maana andiko kama alilonukuu FaizaFoxy la Waefeso 5:18 linasema tulewe Roho Mtakatifu. Kwa maana nyingine furaha yetu inapaswa kuwa ndani ya Roho Mtakatifu na ili ujazwe na Roho Mtakatifu lazima Utubu dhambi zako ikiwemo ulevi na Kuulilia msaada na msamaha alioununua Kristo katika Msalaba wa Kalvari!

Unaweza kuutete unywaji wa pombe aka ulevi kwa nguvu zote, na ni haki yako kufanya hivyo wala sitakuzuia. Ila nikualike kwa Yesu Kristo ambaye kwake kuna pumziko na raha ya moyo ambayo walevi, wavuta unga na wengineo wanaitafuta kwa gharama hata ya maisha yao.

Ukijazwa na Roho Mtakatifu hutahitaji pombe tena.

Kumbuka kila mlevi chakari alianza kidogo kidogo. Hakuna mlevi alianza na chupa kumi!

Shalom!
Barikiwa Pastor.
Ndiyo umuhimu wa kuwepo kwako mtandaoni. Paulo alisema "kuwepo kwangu katika mwili huu yafaa sana kwa ajili yenu" . Kuna sababu ya wewe kuendelea kuishi ili wengi waijue kweli na uwe sababu ya kuwavuta wengi kwa Kristo Yesu.

Halafu habari za Roho Mtakatifu wengi hawazipendi, na ni kwa sababu hawamjui na hayumo ndani yao. Kwa wale walio naye Roho mtakatifu wanaelewa na kujua uzuri wake usioelezeka.

Barikiwa!
 
KKKT labariki unywaji wa Pombe

ASKOFU Mkuu wa zamani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amebariki rasmi unywaji wa pombe katika kanisa hilo kongwe nchini, anaripoti Mwandishi Wetu.

Akizungumza katika mkutano wa 33 wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, wiki iliyopita, huko Seminari ya Kisarawe, mkoani Pwani, Askofu Malasusa amesema, ” katazo la unywaji wa pombe lililetwa na wamisionari, lakini pombe kama pombe haina tatizo.”

Askofu Dk. Malasusa, ndiye askofu mkuu wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Askofu Dk. Malasusa alikuwa akikamilisha majibu yaliyotolewa na Askofu Keshomshahara wa kanisa hilo, Dayosisi ya Bukoba aliyoyatoa kwa swali lilioulizwa na Prof. Mjema wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Katika swali lake, Prof. Mjema alihoji, nafasi ya pombe katika dhana ya Mtume Paulo anapozungumzia kutiwa unajisi kwa vyakula na vinywaji wanavyokunywa wakristo.
Alitaka kupata ufafanuzi wa msiamo wa kanisa juu ya msemo wa “kimuingiacho mtu na kimtokacho mtu.” Awali katika majibu yake, Askofu Keshomshahara amesema, “pombe ni kinywaji tu kama vinywaji na vyakula vingine” na kwamba pombe inapaswa kutumiwa kwa kiasi na kwamba “hata sakramenti takatifu ya Meza ya Bwana inayotumika kanisani mwao ni pombe.”

Baada ya majibu hayo, ndipo Askofu Dk. Malasusa aliposisitiza kuwa makatazo ya pombe kanisani ni “busara ya wamisionari wa kwanza walioleta injili Afrika baada ya kuona Waafrika walikuwa wakilewa bila kiasi na kukosa ustaarabu.”
Aliendelea kusisitiza kuwa “pombe itumike kwa kiasi na hasa kwa wakristo wachanga.”

Majibu hayo ya maaskofu yaliwachanganya wajumbe wengi na kusababisha mijadala baada ya mkutano. Mjumbe mmoja aliyeongea na gazeti hili huku machozi yakimlenga anasema, “nimesikitika sana kuona maaskofu wetu wanalipotosha kanisa. Hivi kweli sakramenti ni pombe?” Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia katiba yake, inapiga marufuku wazee wa kanisa kutomiliki vitega uchumi vinavyouza pombe.

Aidha, sherehe zote za kanisa haziruhusiwi kuwa na pombe huku baadhi ya waumini wakipewa adhabu na wachungaji wao kwa kunywa pombe au kufanya biashara ya pombe. Msimamo wa maaskofu hawa wawili unaliweka kanisa Zima la KKKT katika njiapanda ya kulifafanua jambo hili huku waumini wengi wakitishia kuhamia makanisa ya kiroho kukimbia upotoshaji wa wazi wa maakofu wa KKKT. Mkutano huo wa 33 ulijaa vitimbi vingi vinavyoonyesha dayosisi hiyo haiko shwari.

Akiongea kwa uchungu kwenye mkutano huo, Mchungaji wa kanisa hilo usharika wa Kigogo, jijini Dar es Salaam, Richard Ananja alimtaka Askofu Dk. Malasusa kuachia kiti mara moja kwa kuwa amepoteza sifa kwa kashfa za ngono zinazomkabili.

Amesema Dk. Malasusa anakabiliwa na tuhuma nzito za matumizi ya madaraka, uvujaji wa fedha za dayosisi, hujuma kwa Benki ya Maendeleo, kugushi vyeti ya elimu, ukabila, chuki na visasi kwa wachungaji.

Hivyo basi, ili kulinda hadhi na heshima ya kanisa na yeye binafsi, ni vema Askofu Malasusa “akaachia ngazi kwa hiari, badala ya kusuburi kufukuzwa.”
Hoja hiyo ilipozwa na katibu mkuu wa Dayosisi hiyo, Godfrey Nkini aliyedai kuwa kamati ya maadili inashughulikia tuhuma hizo.

Siku moja kabla ya kufungwa kwa mkutano, mchungaji wa kanisa la KKKT, Usharika wa Kibaha, Amani Lyimo katika mahubiri ya ibada ya asubuhi, aliushambulia utendaji wa Askofu Dk. Malasusa kuwa ni wa uonevu, usijali kweli, uliojaa udhalimu, ubabe na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema uongozi wa Dk. Askofu Malasusa unakomoa watu kuliko uongozi wowote uliopita katika dayosisi hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa mkutano huo, Mwenyekiti wa kamati ya maadili wa dayosisi hiyo, Ibrahim Kaduma, alidai kuwa tuhuma juu ya Askofu Dk. Malasusa, si za kweli na zinachochewa na gazeti moja (hakulitaja) lakini akadai ni chuki ya uislamu dhidi ya kanisa.

Maelezo hayo yalipingwa na wachungaji wengi hali inayoonyesha kuwa Askofu Malasusa hayuko vizuri na wachungaji wake. Wachungaji walidai kamati imeleta “majibu mepesi” kwa tuhuma za ngono zinazomkabili Dk. Malasusa na kwamba kinachobakia sasa wao kumwaga hadharani yaliyositiriwa kulilinda kanisa, alisisitiza mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo mwenye taaluma ya sheria.

Katika hatua nyingine, ajenda ya marekebisho ya katiba ya dayosisi hiyo, iliburuzwa ili kumwepusha Askofu Malasusa na hoja ya ukomo wa madaraka yake. Siku za karibuni, Askofu Dk. Malasusa amekumbwa na tuhuma mfululizo, zikiwamo matumizi mabaya ya madaraka, ngono na ubaguzi.

Hata hivyo, Dk. Malasusa amekuwa akijibu tuhuma hizo kwa kuwanyooshea kidole waumini wanaotoka mikoa ya Kaskazini kuwa wanamsakama kwa vile katika uchaguzi mkuu uliyopita, limuunga mkono Rais Magufuli na kumsaliti swahiba wake wa miaka mingi, Edward Lowassa.

Chanzo: Mwanahalisionline
Kumbe chanzo ni Mwanahalisi
 
Barikiwa Pastor.
Ndiyo umuhimu wa kuwepo kwako mtandaoni. Paulo alisema "kuwepo kwangu katika mwili huu yafaa sana kwa ajili yenu" . Kuna sababu ya wewe kuendelea kuishi ili wengi waijue kweli na uwe sababu ya kuwavuta wengi kwa Kristo Yesu.

Halafu habari za Roho Mtakatifu wengi hawazipendi, na ni kwa sababu hawamjui na hayumo ndani yao. Kwa wale walio naye Roho mtakatifu wanaelewa na kujua uzuri wake usioelezeka.

Barikiwa!
Acheni kudanganyana nyie...Nimemwambia namrudia..Ni vyema na wewe uwe arround wakati namrudia
 
Hata shetani lazima amshangae huyo askofu. Hivi hata kwa kuangalia madhara ya pombe kijamii tu haitoshi mtu kuelewa kuwa pombe ni kitu haramu ambacho Mungu mtakatifu anayejali ustawi wa viumbe wake ansingewez kuruhusu pombe kuwa sehemu ya mpango wa chakula au kinywaji kwa viumbe wake. Hii haihitaji kuwa mtaalamu wa Biblia kulielewa bali common sense. Wanaounga mkono unywaji wa pombe ni mateka wa Shetani ambao wamepotoshwa na mafundisho potofu ya kanisa Katoliki na mabinti zake yanayohalalisha pombe kwa kutafsiri Biblia kulingana na tamaa zao.
Baba Askofu yupo sahihi Bosi wangu,On a jinsi Biblia inavyoruhusu Pombe/Mvinyo-Mhubiri 9:7-"Wewe enenda zako,ule chakula chako kwa furaha,unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka,kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubari kazi zako". Aidha Hata Mtume Paulo aliwahi kumshauri Timotheo kunywa Divai kidogo kwaajili ya Afya yake, 1Timotheo 5:23-"Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo,kwaajili ya tumbo lako,na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.";Hata Yesu Kristo Bwana wetu alibadili Maji kuwa divai ambayo inalevya,rejea Yohane 2:1-8;9-10.Mkuu zipo sehemu nyingine tens zinazoruhusu Pombe/Mvinyo,Soma Mhubiri 2:24,10:19;Yoshua bin sira 40:20;Zaburi 4:7,104:15;Waamuzi 9:13;Katika kitabu cha Mithali tunaambiwa tumpe Kileo Maskini ili asahau taabu zake,rejea Mithali 31:6-7;Kumbe usimlaumu Askofu wala Kanisa Katoliki.Ubaya sio pombe ubaya ni kichwa chako,maana kuna wengine hata wakinywa vipi hawana Shida na mtu sasa ubaya wa pombe utatoka wapi???.
 
Itabidi tu nihamie Lutheran, nimechoka kunywa gwembe kwa kujiiba. Pombe sio dhambi wala bibilia haijakataza
 
Otorong'ong'o ,
Kwanza ujue sina mpango wa kubadili mtu anachoamua kuamini juu ya jambo lolote. Kwangu mimi jukumu langu ni kuusema ukweli na kila mtu aamue yeye mwenyewe. katika miaka yangu yote ya kusoma maandiko hakuna mahali nimekutana na andiko likiongelea vizuri kuhusu pombe na ulevi. Hakuna!
1. Baada ya kupona na gharika Nuhu alilewa akakaa uchi
2. Ajali nyingi sana na maamuzi ya kijinga yanatokana na Pombe.

Najua argument yako ni pombe sio mbaya bali ulevi. Ulevi unatokana na kunywa pombe. Unasema kunywa kiasi si dhambi. Bahati mbaya Biblia haijasema hivyo na hakuna kipimi cha kiasi. Je Mungu akiwa anahukumu siku hiyo atatumia kipimo gani kujua nilipita "kiasi"? Kiasi ni kipi na ni kwa andiko gani? Ulevi ni dhambi iwe wa Chupa moja au nusu glasi.

Nimeomba maandiko yanayoruhusu kwa sababu ninajua hayapo. "Nabii" Tito wa posta naye alikuwa hivyo hivyo lakini pamoja na kuwa "nabii" naye alikosa andiko akaja na hilo hilo.

Tim 5:23 hairuhusu Pombe kwa maana ya Safari Lager, John Walker, Vodka au Sijui nini Wine. Inaruhusu Tomotheo kunywa Mvinyo kama sehemu ya dawa. Na leo tuna dawa nyingi tu zenye pombe ndani yake. Lakini hatunywi kujitafutia furaha humo, la Hasha! Tunakunywa kama dawa kama ilivyokuwa kwa Tim.

Hiyo ya Yesu hata sio ushahidi. Neno la Kigiriki lililotumika ni ambiguous kwa maana linaweza kumaanisha Divai au Mvinyo. Hatujui ni aina gani ya Divai Yesu alitengeneza kutoka katika mstari huu.

Kwa kuongezea tu Mungu anawazaje juu ya Pombe hebu tazama mistari hii:
Walawi 10:8-9 - "Kisha Bwana akanena na Haruni, na kumwambia, Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;

Hesabu 6:3 - [Mnadhiri] atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.

Waamuzi 13:4 - [Mama yake Samsoni] Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

Isaya 5:11 - Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!

Isaya 5:22 - Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;

Mingine iko kwenye Biblia yako utaipitia!

Ukweli ni kwamba kitu pekee ambacho kinawafanya watu wapende Pombe ni sawa kabisa na kile kinawafanya wengine wavute sigara au madawa ya kulevya. Nacho ni kutafuta furaha na kutosheka. Mungu anaichukia Pombe kwa sababu anataka furaha na uteshelevu wetu uwe kwake. Ndio maana andiko kama alilonukuu FaizaFoxy la Waefeso 5:18 linasema tulewe Roho Mtakatifu. Kwa maana nyingine furaha yetu inapaswa kuwa ndani ya Roho Mtakatifu na ili ujazwe na Roho Mtakatifu lazima Utubu dhambi zako ikiwemo ulevi na Kuulilia msaada na msamaha alioununua Kristo katika Msalaba wa Kalvari!

Unaweza kuutete unywaji wa pombe aka ulevi kwa nguvu zote, na ni haki yako kufanya hivyo wala sitakuzuia. Ila nikualike kwa Yesu Kristo ambaye kwake kuna pumziko na raha ya moyo ambayo walevi, wavuta unga na wengineo wanaitafuta kwa gharama hata ya maisha yao.

Ukijazwa na Roho Mtakatifu hutahitaji pombe tena.

Kumbuka kila mlevi chakari alianza kidogo kidogo. Hakuna mlevi alianza na chupa kumi!

Shalom!

Kaka nyie (Walokole/ Wasabato) huwa mna matatizo sana kwwnye maandiko matakatifu, Wakatoliki wamekaa na hiyo Biblia mamia ya miaka kabla hayo madhehebu yenu hayaja anzishwa,

Wakatoliki wanaijua sana hiyo Biblia na hawachagui kitabu cha kusoma ndani ya hiyo Biblia

Hebu tusome andiko la Luka 7:33-34,
" kwa Yohana alikuja hali Mkate wala anywi mvinyo, wakasema ana mapepo, Mwana wa Adamu (Yesu) amekuja AKILA NA KUNYWA, wakasema ni mlafi na MLEVI rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi"

Swali, Yohana alikuwa ANYWI NINI mpaka waseme ana MAPEPO?, Na Yesu ALIKUWA ANAKUNYWA NINI mpaka waseme ni MLEVI?

Cc: Otorong'ong'o , barafu , MTAZAMO , bagain
 
Bora waruhusiwe tu wanywe pombe laini kuliko kuwaacha wakija kuwa wachungaji wanakunywa konyagi aka bapa!!
 
Kaka nyie (Walokole/ Wasabato) huwa mna matatizo sana kwwnye maandiko matakatifu, Wakatoliki wamekaa na hiyo Biblia mamia ya miaka kabla hayo madhehebu yenu hayaja anzishwa,

Wakatoliki wanaijua sana hiyo Biblia na hawachagui kitabu cha kusoma ndani ya hiyo Biblia

Hebu tusome andiko la Luka 7:33-34,
" kwa Yohana alikuja hali Mkate wala anywi mvinyo, wakasema ana mapepo, Mwana wa Adamu (Yesu) amekuja AKILA NA KUNYWA, wakasema ni mlafi na MLEVI rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi"

Swali, Yohana alikuwa ANYWI NINI mpaka waseme ana MAPEPO?, Na Yesu ALIKUWA ANAKUNYWA NINI mpaka waseme ni MLEVI?

Cc: Otorong'ong'o , barafu , MTAZAMO , bagain
Hahahahahaha!!!!
 
Kaka hawa ni kwenda nao polepole wataelewa tu, shida yao ni kusoma biblia nusunusu, ukiona kitu kinafanywa na Wakatoliki basi hicho kitu kamwe HAKIKO kinyume na maandiko matakatifu
Yani mimi huwa nashangaa , miaka ya nyuma matumizi ya maji ya baraka, mafuta walikuwa wanaita ni upagani wa Wakatoliki ..ila leo hii naona na wao wanavitumia...

Mbaya zaidi kuna wale wanajaribu kuiga ekaristi ila ndio wanaharibu maana wanalishana mikate ya superloaf na juisi za Fruto..

Its a matter of time...Watakuja kuelewa tuu....
Kanisa la Methodist ni majuzi wamekuja kugundua kweli B/Maria ni mama wa Mungu..Na wanampa heshima zote...

Tuwape muda...
Ila tatizo moja hawana elimu ya Filosofia na Teolojia....
 
Back
Top Bottom