KKKT: kufungisha ndoa mnatoza 100,000/=!

KKKT: kufungisha ndoa mnatoza 100,000/=!

Kuna rafiki yangu mmoja ameamua kubariki ndoa, hii ni baada ya kuishi katika ndoa ya Kimila kwa mwongo mmoja! Ila hasa na mashinikizo ya kidini kuwa ni lazima wafunge ndoa kanisani ili wakamilike kiroho. Sasa alipokwenda kanisani ndio kakumbana na hiyo hela kama sehemu ya masharti. Ameogopa akajua anaibiwa.

Ndio kanifuata mimi "mzee wa Kanisa " kuuliza hili ni tozo gani! Ama kweli katika ufahamu wangu wa Kanuni za KKKT hii kwangu ni mpya.

Hebu mnijuze naogopa kumpigia mchungaji kuuliza !Kam ndiyo ilivo mh....!Tafadhali tuchangie kwa staha bila jazba.

sasa kwa kanisa laki c pesa....kwani ukumbi wa kufanyia harusi mmeulipia sh ngapi??....
 
Kwenye harusi huwa unachangia double tsh ngapi? Kwanini unahoji kuhusu sadaka ya kuendeleza kazi ya Mungu? Wewe unadhani umeme, maji, petroli ya mchungaji wako itoke wapi?? Nadhani wewe uliyetoa hii thread siyo mzee wa kanisa, ni mhuni tu unayeamua kukojolea wakiristo.

KYALOSANGI hiyo ndio gharama halali kwa malipo ya cheti cha ndoa(10,000/-tsh only). Hiyo tisini kanisa litakuwa limeamua kuwapiga. Which is sad...

Kweli Mungu atakuwa anajuta kumuumba mwanadamu! Kuna siku niliketi ghorofani kanisani, wiki iliyofuata nikamuambia mchungaji nimeona buibui kwenye corners. Nataka kuita kampuni ya usafi nitailipa. Mchungaji akakataa na kusema ipo kampuni, wanahitaji guidance tu.

Ndio nikajiuliza. Hivi kila siku nakuja kanisani pako pasafi, mbele kuna fresh flowers. Sijawahi kukalia kiti kina vumbi wala sijawahi kwenda kupanga viti? Sadaka yangu inafanya kazi kwa sababu niko busy. Hata ningeombwa kufanya usafi nisingepata nafasi.

Now kwa mtoa mada. Unaenda kanisani siku ya harusi yako kanisa safi, limepambwa maalum na vitambaa na pia maua fresh. Kwaya inaimba na magitaa hapo na kinanda. Umeme ukikatika kuna generator inaunguruma! Unadhani viko pale automatic? Mtu anaelalamikia laki ya kufunga ndoa ujue hata zaka hatoi.

Mwanaume ambae hawezi kutoa laki kwa ajili ya procedure za kanisani ataweza kulisha mke na watoto kwa jasho? Sie kwetu kabla hujaoa lazma uite ndugu uwalishe na kuwaambia umekua na unataka kuoa. Kama hujaweza kulisha wazee mke si watakusaidia aisee?

Nini kilimfanya Martin Luther kulihama Kanisa Katoliki na kuanzisha hili Kanisa ?
Ni haya ambayo yanahojiwa hapa.
Kanisa kuanza kuwekeza kwenye mambo ya kidunia ndiko kunaleteleza Ukengeufu wa kuanza kuuza huduma za kiroho.
Kanisa kuongozwa na wanadamu ambao mawazo yao yamejikita kuimarisha kesho ya kidunia ndiyo msingi wa Ukengeufu.
Kanisa limepoteza dira liko kwenye ushindani wa majengo mazuri na fahari za kidunia huku likijitenga na Kweli ya Bwana Wetu Yesu Kristo.
Waamuni wanatoa sadaka na matoleo mengi mengi kila wiki ni uwekezaji mbaya na priority za kidunia zinazofanya Kanisa lionekane linapungukiwa.
Hakika Kanisa limepoteza wito imebaki kuwa kijiwe cha kufarijiana ujinga...
 
Last edited by a moderator:
Hakuna malipo hayo isipokuwa bei ya cheti. Kuhusu laki moja inaweza kuwa kweli pia hasa pale ambapo mtu anaenda kufungia ndoa usharika ambao sio wake kwa vyovyote kuna gharama fulani hasa pale Azania Front mahali ambapo wengi wanapenda. Cost lazima ziwepo kwa sehemu fulani. Maelezo zaidi njoo PM

Unataka PM kwani hizo gharama ni nyara za taifa au bangi. Ziweke hapa tuona uhalali wake Kama Kanisa siku hizi linashindana na Guest house kukamua wahudhuriaji wake.
 
Ndugu,

Nimefuatilia uzi huu tangu mwanzo na napata mashaka juu ya dhamira yako ulipokuwa unauanzisha uzi huu. Kama dhamira yako ilikuwa njema, ningetegemea ungemuuliza mchungaji wako. Kama huyo unamuogopa, hata basi wazee wenzako wawili watatu ili kuweza kutafuta majawabu kuhusiana na hili. Kwa kufanya hivi sisi huku JF wala tusingejua na pia ungekuwa umesaidia si tu kanisa basi imani ya kikristo baada ya wahusika kuacha kufanya jambo hilo kama linafanyika kimakosa.

Kwa kulileta JF, tazama wengine si tu wanadhihaki kanisa lakini hadi imani nayo haiwezi kuachwa, inadhihakiwa. Je, hili ndilo ulilolitaka toka ndani ya moyo wako, ndugu yangu?

Uzee wa kanisa ni utumishi mkubwa sana ambao kama hutokuwa mwangalifu unaweza kukuletea shida ambazo pengine usingezipata kama usingekuwa mzee wa kanisa. Kila siku kumbuka kuwa mwenye imani yake yupo na anaona yote tunayoyafanya.

Tafakari.

Kanisa lijichunguze kutokana na mjadala huh.
Hata wewe nakushauri ukiona ukengeufu kanisani usisite kuuleta hapa ili kulirudisha Kanisa kwenye mstari.
Huwezi sukuma gari lililozimika ukiwa ndani ya hilo gari inakubidi ushuke then ndipo ulisukume. Kanisa limejichafua lenyewe kwa kutenda kinyume na aliyokuwa anayapinga mwasisi wake.
Ni ujuha kusimamia ujinga na kuweka kuwa ni siri ati kulinda heshima ya kanisa. Kanisa linawezaje kutenda mambo yanayolishushia heshima ?
 
sasa kwa kanisa laki c pesa....kwani ukumbi wa kufanyia harusi mmeulipia sh ngapi??....

Fikiri japo kidogo. Usifananishe bajia na kababu...
Kanisa hutoa huduma za kiroho....
Kumbi hutoa huduma za kibiashara...
Wakristo wa kizazi hiki mnawaza kwa kutumia nini kiasi kushabikia ukengeufu wa Kanisa ?
 
sasa kwa kanisa laki c pesa....kwani ukumbi wa kufanyia harusi mmeulipia sh ngapi??....
ndugu uko sahihi mana hata fungu la kumi hajawai toa.laki imepitwa na wakati
usharikan kwetu tunataka kufanya laki mbili ili kila muumin afungie sharikani kwake.wasio na uwezo diaconia inawalipia(wanaoabudu sharikani kwetu tu)wanaotoka nje tunawafanyia harambee(baada ya kupata barua toka usharikani kwako na cheti cha safari) washarika wana walipia na unapewa risiti-kwa msaada wa watu wa ushrika
 
Masikini Martin Luther alisumbuka bureee...
 
Kanisa lijichunguze kutokana na mjadala huh.
Hata wewe nakushauri ukiona ukengeufu kanisani usisite kuuleta hapa ili kulirudisha Kanisa kwenye mstari.
Huwezi sukuma gari lililozimika ukiwa ndani ya hilo gari inakubidi ushuke then ndipo ulisukume. Kanisa limejichafua lenyewe kwa kutenda kinyume na aliyokuwa anayapinga mwasisi wake.
Ni ujuha kusimamia ujinga na kuweka kuwa ni siri ati kulinda heshima ya kanisa. Kanisa linawezaje kutenda mambo yanayolishushia heshima ?

Mkuu,

Kama una amani na ulichoandika, basi sawa.

Barikiwa.
 
Nini kilimfanya Martin Luther kulihama Kanisa Katoliki na kuanzisha hili Kanisa ?
Ni haya ambayo yanahojiwa hapa.
Kanisa kuanza kuwekeza kwenye mambo ya kidunia ndiko kunaleteleza Ukengeufu wa kuanza kuuza huduma za kiroho.
Kanisa kuongozwa na wanadamu ambao mawazo yao yamejikita kuimarisha kesho ya kidunia ndiyo msingi wa Ukengeufu.
Kanisa limepoteza dira liko kwenye ushindani wa majengo mazuri na fahari za kidunia huku likijitenga na Kweli ya Bwana Wetu Yesu Kristo.
Waamuni wanatoa sadaka na matoleo mengi mengi kila wiki ni uwekezaji mbaya na priority za kidunia zinazofanya Kanisa lionekane linapungukiwa.
Hakika Kanisa limepoteza wito imebaki kuwa kijiwe cha kufarijiana ujinga...

kuna ndoa za mafungu bure hata mia hutoi na ukumbi wa kanisa bure!chakula bure!kwaya mbili bure(vijana na kwaya kuu),tunawalipia sisi washarika,ni ww na mke na ndugu zako,tunaomba maparishiweka na wainjilist kua mc yaani buree wewe tu.matarumbeta bure na hata kwaya ya shule ya jumapi
 
Mbona laki moja pesa ndogo sana mkuu!acha kulalama bhana,kwa wanaume wa Dar kwetu hiyo pesa ndogo sana.
 
Kwa Azania front hiyo ni bei ipo tokea miaka.mingi kwa makanisa mengine ni lazima waige .

Mshauri aende kanisa ambalo hawalipii kama mfuko wake unasuasua.
 
kuna ndoa za mafungu bure hata mia hutoi na ukumbi wa kanisa bure!chakula bure!kwaya mbili bure(vijana na kwaya kuu),tunawalipia sisi washarika,ni ww na mke na ndugu zako,tunaomba maparishiweka na wainjilist kua mc yaani buree wewe tu.matarumbeta bure na hata kwaya ya shule ya jumapi

Kanisa linao wajibu wa kutoa huduma za kiroho kwa maana ya sacrament bureee...
Kama Kanisa linauhitaji ni wajibu wa waumini kutatua uhitaji huo lakini sio kuuza huduma...
 
apo sasa na mie nataka kufunga mwezi wa 10 sasa hii si dhahama jamani kanisa langu Lutheran limekumbwa na nn jamaani
 
Kwa Azania front hiyo ni bei ipo tokea miaka.mingi kwa makanisa mengine ni lazima waige .

Mshauri aende kanisa ambalo hawalipii kama mfuko wake unasuasua.

Hapo umenena!Viwango viko kutokana na dayosisi !Kwani lazima cathedral au makao makuu ya jimbo?Unataka sharika nyingine akafunge nan?Pia kuna sharika zina huduma ya mision nje ya mipaka ya dayosisi au nchi na zinabebwa na washarika!Msifikiri unapoeneza injili ni lelemama!La mwisho mjipime wenyewe mnaonekana kwenye ndoa na ubatizo na kipaimara vikao hamfiki.jimbo,dayosisi au makao makuu wanapoamu unalalamika!Ukikua wapi? Mwingine hajui hata makao makuu ya sinodi au dinari au dayosisi yake!
 
Kuna rafiki yangu mmoja ameamua kubariki ndoa, hii ni baada ya kuishi katika ndoa ya Kimila kwa mwongo mmoja! Ila hasa na mashinikizo ya kidini kuwa ni lazima wafunge ndoa kanisani ili wakamilike kiroho. Sasa alipokwenda kanisani ndio kakumbana na hiyo hela kama sehemu ya masharti. Ameogopa akajua anaibiwa.

Ndio kanifuata mimi "mzee wa Kanisa " kuuliza hili ni tozo gani! Ama kweli katika ufahamu wangu wa Kanuni za KKKT hii kwangu ni mpya.

Hebu mnijuze naogopa kumpigia mchungaji kuuliza !Kam ndiyo ilivo mh....!Tafadhali tuchangie kwa staha bila jazba.

hapo kuna gharama za umeme, mchango wa kwaya itakayokuwepo siku hiyo, cheti cha ndoa na sadaka kwa ajili ya huduma. Hela ndogo sana hiyo ukilinganisha na uzito wa jambo lenyewe......mbona mnagharamia kumbi,vinywaji,vyakula mc na music,usafiri tarumbeta nk hamji kulalamika kanisani ndo mnataka mteremko? Nyoooooooooo
 
pole sana ,na masikitiko kwa walio kuleta na akil ya aina hii!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom