Mama amvaa mchungaji, asambaratisha ndoa ya bintiye Kanisani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
aibu.jpg
DAR ES SALAAM:
Vuta picha bibi harusi ameshavaa shela, bwana harusi ameshatinga suti yake matata kabisa, wameshaingia madhabahuni kanisani, tayari kabisa kwa kufungishwa ndoa halafu ghafla mtu anatokea na kuisambaratisha ndoa hiyo, hakika hii ni aibu ya aina yake!

Unaweza kuona ni kama filamu ya ‘Ki-Nigeria’ lakini hapana, ndivyo ilivyomtokea mubashara bwana harusi mtarajiwa, Elisha Mjuu kwa mkewe mtarajiwa, Betina Benson (pichani) ambao tayari walishaikanyaga madhabahu ya Bwana kwa ajili ya kufungishwa ndoa, ghafla akatokea mama mzazi wa bibi harusi, Roda Mtakya akaisambaratisha ndoa hiyo papo hapo!

NI JUMAMOSI ILIYOPITA
Tukio hilo lililowaacha ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamepigwa butwaa lilitokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbagala jijini Dar es Salaam lilitokea tarehe 22.06.2018

MAMA ALIFICHWA
Inadaiwa wanandoa hao walipanga kufunga ndoa hiyo bila kumshirikisha mama huyo mzazi wa bi harusi, mkazi wa Mbagala jijini Dar ambapo ghafla walimshtukia mama huyo ameibuka madhabahuni akiwa pekupeku na kutamka kuwa ndoa hiyo isifungwe.

KUMBE KUNA MGOGORO
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, Betina alikuwa na mgogoro na mama yake ambao ulimfanya ahame kwa mama yake na kwenda kuishi anakojua.
Imedaiwa kuwa, Betina aliendelea na maisha yake akampata mwenza huyo na kukubaliana wafunge ndoa ili wasitende dhambi ambapo kwa mtazamo wao wakaona waendelee na mipango yao ya harusi bila kumshirikisha mama huyo mzazi.

MAMA HAJAAMBULIA KITU
Chanzo hicho kimeendelea kudai kuwa, mipango hiyo ilisukwa bila mama wa bi harusi kujua aliyepokea mahari, mkaja wa mama na vikorombwezo vingine vya mila na desturi.

WAPAMBE WAMTONYA
Wakati mipango hiyo ikiendelea kwa siri, mama wa bi harusi aliinyaka ishu kwa wapambe wa mitaani ambao walimpa ‘ubuyu’ wote
Inadaiwa kuwa, baada ya kutonywa, mama huyo alifika kwa mchungaji na kuweka pingamizi ambapo mchungaji aliahidi kushughulikia suala lake lakini kabla hajafanya hivyo, mama akasikia ndoa inafungwa ndipo akavamia.

SIKU YA TUKIO
Mama huyo alipopenyezewa habari za kufungwa ndoa hiyo ndipo alipotinga madhabahuni kisha kupaza sauti akimtaka mchungaji aliyetajwa kwa jina la Ngaleni aliyekuwa akiifungisha ndoa hiyo kuisitisha na kusema bibi harusi huyo ni mwanaye wa kumzaa na yeye kama mama mzazi hajajulishwa ndoa na wala hajaisikia wala kuiona barua ya posa wala mahari.

Kufuatia sakata hilo mwanahabari wetu ambaye alisikia fununu za kutaka kutokea tukio hilo naye alifika kanisani na kulikuta likiendelea na kulishuhudia laivu.
Mama huyo wa bi harusi alisikika akipaza sauti madhabahuni hapo akisema ndoa hiyo ni batili na haina baraka zake. “Huyo bi harusi Betina ni mwanangu wa kumzaa mwenyewe iweje leo afungishwe ndoa tena kanisani bila kunijulisha hata kama nina umasikini gani au nina kilema gani iweje?

“Wewe mchungaji Ngaleni mimi si nimeshakuja ofisini kwako kukuletea barua za pingamizi la hiyo ndoa ya mwanangu kabla ya siku ya leo ukaniambia utalimaliza suala hilo kabla ya kuwafungisha ndoa, sasa mbona hivi?
“Hujanitendea haki, sasa mimi kama mama nasema hapa hakuna ndoa na hata kama unataka kuwafungisha kinguvu we’wafungishe lakini mimi kama mama mzazi nasema mbele ya madhabahu hii kuwa kama utawafungisha hiyo ndoa ni batili,” alisema mama huyo akiwa ndani ya kanisa.

NDOA YASITISHWA
Baada ya ndoa hiyo kutibuliwa, mchungaji huyo aliisitisha na kuwaomba wazee wa kanisa wakaongee na mama huyo kiustaarabu ili awasamehe maharusi hao wafunge ndoa takatifu kwa amani, furaha na baraka za wazazi.

AWAGOMEA…
Hata hivyo, mama huyo alishindwa kuelewana na wazee hao wa kanisa na hata alipotoka nje mchungaji aliyekuwa akiwafungisha ndoa hawakuweza kuelewana naye.
Mama huyo alikuwa akilalamikia kitendo cha mchungaji huyo kupokea shauri la pingamizi lake na kumwambia atalifanyia kazi lakini matokeo yake akamfungisha ndoa mwanaye kabla ya kuafikiana naye katika barua yake ya pingamizi.

MCHUNGAJI NA UWAZI
Mwanahabari wetu alizungumza na Mchungaji Ngaleni nje ya kanisa hilo ndoa ilipositishwa ambapo alikiri kupokea barua za pingamizi la mama huyo lakini akasema: “Kwa kimila ni lazima kuwashirikisha wazazi katika ndoa lakini kidini siyo lazima kuwashirikisha wazazi ila ni muhimu na ni vizuri.”

MCHUNGAJI ALAUMIWA
Baadhi ya waumini waliokuwa eneo la tukio walisikika wakimlaumu Mchungaji Ngaleni kwa kutaka kufungisha ndoa hiyo na kusema kama kulikuwa na mgogoro kati ya bi harusi na mama yake basi alitakiwa kushughulikia hilo kwanza na ndipo awafungishe ndoa lakini si kama alivyofanya.

“Ni kama alilipotezea tu pingamizi la huyo mama ukizingatia bwana harusi ni mwanakwaya wa hapa kanisani pengine ndio maana wameonekana kupewa upendeleo, ona sasa mchungaji ameondoka ameinamisha kichwa chini,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Kujura.

MAMA ANENA
Hata hivyo, baada ya sakata hilo Uwazi lilizungumza na mama wa bi harusi na lilipomhoji, atafanya nini baada ya ndoa kusitishwa alisema kifupi:

“Mimi nakwenda mbele zaidi kisheria ili mimi kama mama mzazi nijue nafasi na haki yangu katika sakata hilo. “Sijatendewa haki hata kidogo katika hili na hata Mungu ananiona, huyu mtoto amekaa tumboni mwangu miezi tisa, iweje nisishirikishwe katika tendo la takatifu kama hili?”

SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inasema kama kutakuwa na pingamizi ni budi itolewe kabla ya ndoa kufungwa.

Aidha, sheria hiyo inasema mwanaume au mwanamke kuolewa au kuoa lazima kuwe na idhini ya mzazi au mlezi.

Chanzo:GGLOBALSPUBLISHERS
 
Daaaah!! Sasa mwanamke mwenzangu, si ungeitisha vikao vya familia pindi uliposikia kuliko kumkomesha binti ako kwa style hio? Labda ulienda ki jazba sana ndio maana hata Mchungaji akaamua aendelee tu kumhitimishia binti agano la NDOA!
 
aibu.jpg
DAR ES SALAAM:
Vuta picha bibi harusi ameshavaa shela, bwana harusi ameshatinga suti yake matata kabisa, wameshaingia madhabahuni kanisani, tayari kabisa kwa kufungishwa ndoa halafu ghafla mtu anatokea na kuisambaratisha ndoa hiyo, hakika hii ni aibu ya aina yake!

Unaweza kuona ni kama filamu ya ‘Ki-Nigeria’ lakini hapana, ndivyo ilivyomtokea mubashara bwana harusi mtarajiwa, Elisha Mjuu kwa mkewe mtarajiwa, Betina Benson (pichani) ambao tayari walishaikanyaga madhabahu ya Bwana kwa ajili ya kufungishwa ndoa, ghafla akatokea mama mzazi wa bibi harusi, Roda Mtakya akaisambaratisha ndoa hiyo papo hapo!

NI JUMAMOSI ILIYOPITA
Tukio hilo lililowaacha ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wamepigwa butwaa lilitokea Jumamosi iliyopita katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Mbagala jijini Dar es Salaam lilitokea tarehe 22.07.2018

MAMA ALIFICHWA
Inadaiwa wanandoa hao walipanga kufunga ndoa hiyo bila kumshirikisha mama huyo mzazi wa bi harusi, mkazi wa Mbagala jijini Dar ambapo ghafla walimshtukia mama huyo ameibuka madhabahuni akiwa pekupeku na kutamka kuwa ndoa hiyo isifungwe.

KUMBE KUNA MGOGORO
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, Betina alikuwa na mgogoro na mama yake ambao ulimfanya ahame kwa mama yake na kwenda kuishi anakojua.
Imedaiwa kuwa, Betina aliendelea na maisha yake akampata mwenza huyo na kukubaliana wafunge ndoa ili wasitende dhambi ambapo kwa mtazamo wao wakaona waendelee na mipango yao ya harusi bila kumshirikisha mama huyo mzazi.

MAMA HAJAAMBULIA KITU
Chanzo hicho kimeendelea kudai kuwa, mipango hiyo ilisukwa bila mama wa bi harusi kujua aliyepokea mahari, mkaja wa mama na vikorombwezo vingine vya mila na desturi.

WAPAMBE WAMTONYA
Wakati mipango hiyo ikiendelea kwa siri, mama wa bi harusi aliinyaka ishu kwa wapambe wa mitaani ambao walimpa ‘ubuyu’ wote
Inadaiwa kuwa, baada ya kutonywa, mama huyo alifika kwa mchungaji na kuweka pingamizi ambapo mchungaji aliahidi kushughulikia suala lake lakini kabla hajafanya hivyo, mama akasikia ndoa inafungwa ndipo akavamia.

SIKU YA TUKIO
Mama huyo alipopenyezewa habari za kufungwa ndoa hiyo ndipo alipotinga madhabahuni kisha kupaza sauti akimtaka mchungaji aliyetajwa kwa jina la Ngaleni aliyekuwa akiifungisha ndoa hiyo kuisitisha na kusema bibi harusi huyo ni mwanaye wa kumzaa na yeye kama mama mzazi hajajulishwa ndoa na wala hajaisikia wala kuiona barua ya posa wala mahari.

Kufuatia sakata hilo mwanahabari wetu ambaye alisikia fununu za kutaka kutokea tukio hilo naye alifika kanisani na kulikuta likiendelea na kulishuhudia laivu.
Mama huyo wa bi harusi alisikika akipaza sauti madhabahuni hapo akisema ndoa hiyo ni batili na haina baraka zake. “Huyo bi harusi Betina ni mwanangu wa kumzaa mwenyewe iweje leo afungishwe ndoa tena kanisani bila kunijulisha hata kama nina umasikini gani au nina kilema gani iweje?

“Wewe mchungaji Ngaleni mimi si nimeshakuja ofisini kwako kukuletea barua za pingamizi la hiyo ndoa ya mwanangu kabla ya siku ya leo ukaniambia utalimaliza suala hilo kabla ya kuwafungisha ndoa, sasa mbona hivi?
“Hujanitendea haki, sasa mimi kama mama nasema hapa hakuna ndoa na hata kama unataka kuwafungisha kinguvu we’wafungishe lakini mimi kama mama mzazi nasema mbele ya madhabahu hii kuwa kama utawafungisha hiyo ndoa ni batili,” alisema mama huyo akiwa ndani ya kanisa.

NDOA YASITISHWA
Baada ya ndoa hiyo kutibuliwa, mchungaji huyo aliisitisha na kuwaomba wazee wa kanisa wakaongee na mama huyo kiustaarabu ili awasamehe maharusi hao wafunge ndoa takatifu kwa amani, furaha na baraka za wazazi.

AWAGOMEA…
Hata hivyo, mama huyo alishindwa kuelewana na wazee hao wa kanisa na hata alipotoka nje mchungaji aliyekuwa akiwafungisha ndoa hawakuweza kuelewana naye.
Mama huyo alikuwa akilalamikia kitendo cha mchungaji huyo kupokea shauri la pingamizi lake na kumwambia atalifanyia kazi lakini matokeo yake akamfungisha ndoa mwanaye kabla ya kuafikiana naye katika barua yake ya pingamizi.

MCHUNGAJI NA UWAZI
Mwanahabari wetu alizungumza na Mchungaji Ngaleni nje ya kanisa hilo ndoa ilipositishwa ambapo alikiri kupokea barua za pingamizi la mama huyo lakini akasema: “Kwa kimila ni lazima kuwashirikisha wazazi katika ndoa lakini kidini siyo lazima kuwashirikisha wazazi ila ni muhimu na ni vizuri.”

MCHUNGAJI ALAUMIWA
Baadhi ya waumini waliokuwa eneo la tukio walisikika wakimlaumu Mchungaji Ngaleni kwa kutaka kufungisha ndoa hiyo na kusema kama kulikuwa na mgogoro kati ya bi harusi na mama yake basi alitakiwa kushughulikia hilo kwanza na ndipo awafungishe ndoa lakini si kama alivyofanya.

“Ni kama alilipotezea tu pingamizi la huyo mama ukizingatia bwana harusi ni mwanakwaya wa hapa kanisani pengine ndio maana wameonekana kupewa upendeleo, ona sasa mchungaji ameondoka ameinamisha kichwa chini,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Kujura.

MAMA ANENA
Hata hivyo, baada ya sakata hilo Uwazi lilizungumza na mama wa bi harusi na lilipomhoji, atafanya nini baada ya ndoa kusitishwa alisema kifupi:

“Mimi nakwenda mbele zaidi kisheria ili mimi kama mama mzazi nijue nafasi na haki yangu katika sakata hilo. “Sijatendewa haki hata kidogo katika hili na hata Mungu ananiona, huyu mtoto amekaa tumboni mwangu miezi tisa, iweje nisishirikishwe katika tendo la takatifu kama hili?”

SHERIA INASEMAJE?
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inasema kama kutakuwa na pingamizi ni budi itolewe kabla ya ndoa kufungwa.

Aidha, sheria hiyo inasema mwanaume au mwanamke kuolewa au kuoa lazima kuwe na idhini ya mzazi au mlezi.

Chanzo:GGLOBALSPUBLISHERS
Hiyo tarehe ya tukio mbona hatujaifikia?!.
 
We bwana harusi acha ujanja, kata mapene kwa mama mzaa chema, acha ujanja ujanja - mbona sisi wenzako tulitoa na tunaendelea kutoa mara kwa mara???

acha hizo sheikh, hata laki tano tu kumpoza bi mkubwa umekosa wakati kakuzalia tunda zuri ivo....
 
kuna ulazima ganu wa kuwa na idhini ya wazazi ilhali wanaoona wamepita miaka 18?. Hiyo sheria ni ya kizembe sana.
 
We bwana harusi acha ujanja, kata mapene kwa mama mzaa chema, acha ujanja ujanja - mbona sisi wenzako tulitoa na tunaendelea kutoa mara kwa mara???

acha hizo sheikh, hata laki tano tu kumpoza bi mkubwa umekosa wakati kakuzalia tunda zuri ivo....
Kabisa
Ampe mama Kifuta jasho chake.Ingawa mama na Mwana they need to work on their relationship.Hata akipewa million 10 kama mahusiano yake na mwanaye yapo impaired beyond repair hawezi kuona utamu wake.Naona hapa anataka kumkomoa binti yake.
 
Watu tupo tofauti sana yaani ninavyompenda mama yangu mtu ufanye tukio kubwa kama hilo usimshirikishe?
 
Mbagala kuna waswahili sana,huyo mama wa bibi harusi hana tofauti na mama Diamond!
 
Watu tupo tofauti sana yaani ninavyompenda mama yangu mtu ufanye tukio kubwa kama hilo usimshirikishe?
ni kitu si cha kawaida, ila nafikiri tungepata chance a kupata comment ya bibi harusi tungejua undani zaidi. Mama ndiye msiri mkubwa, yawezekana kijana anayetaka kumwoa ni kaka yake.....who knows

Thats why kwenye issue nzima hatujaona comment ya baba mzazi wa bibi harusi.....
 
Jaman kuna watu wanadharau kwa mama zao daah . ila sie hatuwez fahamu ugomvi halisi wa mama na mwana
 
si ajabu bwana harusi alikuwa anakula huyo mama ndo maana binti akakimbia nyumbani.
hapo kuna wivu wa kimapenzi si bure
 
Back
Top Bottom