KKKT: kufungisha ndoa mnatoza 100,000/=!

KKKT: kufungisha ndoa mnatoza 100,000/=!

Kweli wewe ni conservative ! ninachosema mimi kuwa KANISA limekengeuka ibada kama hii haistahili kulipiwa kiwango hicho! Ni kweli kueneza injili si lelelmama lakini tupime na maeneo ya kutoza hela!
Hapo umenena!Viwango viko kutokana na dayosisi !Kwani lazima cathedral au makao makuu ya jimbo?Unataka sharika nyingine akafunge nan?Pia kuna sharika zina huduma ya mision nje ya mipaka ya dayosisi au nchi na zinabebwa na washarika!Msifikiri unapoeneza injili ni lelemama!La mwisho mjipime wenyewe mnaonekana kwenye ndoa na ubatizo na kipaimara vikao hamfiki.jimbo,dayosisi au makao makuu wanapoamu unalalamika!Ukikua wapi? Mwingine hajui hata makao makuu ya sinodi au dinari au dayosisi yake!
 
aNi kweli inawezakana kwa wanaume wa D ar kama wewe ! kama watu walieba feddha kwye lumbesa unategea nini ! Lakini huwezi kuishi kwa majumisho wenzio laki moja ni kubwa sana !Kama kanisa halijui hivo basi Dini hiyo ni ya kutilia mashaka! Kumbuka kuna vijana wanalipwa elfu 80,70,100, wakikusikia unaongea haya kwao ni maneno ya kippuzi!na ndio hao wanawageuka na kuwakimbiza na vitambi vyenu hovyo wanajiita watototwa Panya! Yesu hakuleta madhehebu na taratibu hizi YESUalikuja kwa maskini ....na matajiri wanyoofu wa mioyo
Mbona laki moja pesa ndogo sana mkuu!acha kulalama bhana,kwa wanaume wa Dar kwetu hiyo pesa ndogo sana.
 
Kwa Azania front hiyo ni bei ipo tokea miaka.mingi kwa makanisa mengine ni lazima waige .

Mshauri aende kanisa ambalo hawalipii kama mfuko wake unasuasua.
Azania Front kuna tofauti gani na Manzese,Chanika au Pugu kwa Yusuph! Sakramenti ni ile ile hivi kwa nini tunalazimishwa kufikiri kinyume2 na kulifanya kanisa kuwa pango la wanya'ganyi!Ibada gani inatendek Azania !Ujinga walotuahia wakoln tunndeleza ka etuihta makania yana madaraja!
 
sasa kwa kanisa laki c pesa....kwani ukumbi wa kufanyia harusi mmeulipia sh ngapi??....
Nani kakwambia kalipaia ukumbi wa harusi aua kafanya sherehe unayoifikiria wewe! Tusiishi kwa mazoea na kuumiza wengine! Kama si uhuru binafsi ningekuletea picha na matukio ya harusi yake ungejifunza kitu ...!
 
Hapo inawezekana, kwani hata stahili yao ya kusali si ya utamaduni wa KKKT kabisa, inaonekana viongozi hapo wamejiinua na kuanzisha ka system kao. Lakini Dar sharika nyingi za KKKT ni kama zinamilikiwa na viongozi ((wachungaji viongozi) wanakoelekea watakuwa kama kina Lusekelo tu
 
Hiyo ni kweli nadhani ni KKKT wote maana hivi majuzi kuna ndugu yangu naye alifungia KKKT ukonga na tozo ilikuwa ni laki Moja,kuna kiasi kinakwenda mfuko wa kwaya,kiasi kwenye zile shahada za ndoa ukumbuke kuwa unapewa mbili ya serikali na ya kanisa, kiasi kingine kwenye shughuli nyingine za uendeshaji wa kanisa.Yeye angeuliza tuu angepewa ufafanunuzi,over !!!
 
Ni elfu 10 tu kwa hiyari.
Kama kweli huna husaidiwa,
zingatia ni gharama za fomu ya serikali,
Ina ne ''mboo'' ya bibi na bwana.
Walioshika pembe,
Wengine wanakamua.
 
jamaani sikilizeni askofu niwajibu
kila kitu na kila sehemu kunakuwa na utaratibu wake pamoja na kanuni,sijaona kama kuna umuhimu wa kuprolong maada kwani kuna tatizo gani its better mtu angeuliza palepale ufafanuzi wa gharama siyo kucomplain tu jaman.af inaonekana humu wote hawajaoa kama ndiyo bas ndoa za kipagani coz you are complaining withot rizon
 
Wewe ni Mzee wa kanisa unashindwa kuongea na mchungaji wako unatuletea huu upuuzi hapa JF. Kama huwezi kuongea nae kwa mambo muhimu kama haya si ujihuzuru au kama huduma zingine huhusiki nazo si ukae kimya yote yakikushinda si uhame dini kwani umefungiwamo kamba. Nahisi itakuwa wa kwanza kuomba bia kwenye sherehe huku uliona nongwa mtu kutoa 100,000 kanisani!

BP
 
Mkuu Mungu alikupa akili itumie vema ! mimi nimeuliza swali kama huna jibu nyamaza! Mimi ni mLuther ila sijawhi shiriki kwa karibu katika michakato hii ,pengine ni sahihi au jamaa kadanganywa ! Ndio maana umeweka utambulisho wako hivo!

Kyalosangi nina wasi wasi huyo jamaa yako hajakueleza vizuri au pengine hujamuelewa. Siku hizi wachungaji wanafundisha hasa kwenye mafundisho ya wanandoa watarajiwa.

Unapofunga ndoa unapashwa kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyokutendea hasa ktk kipindi cha uchumba mpaka ukafikia siku hiyo ya kubariki ndoa. Kuna mambo mengi yanatokea kipindi cha uchumba. Hujawahi sikia mchumba anatoroka siku ya harusi anaingia mitini. Anaenda kwa boyfriend wake wa zamani?!!! Hivi wewe ukioa salama bila mikosi kama hiyo, Mungu utamshukuru kwa namna gani??

Hivyo wana ndoa wanafundishwa kumtolea Mungu ikiwa kama ni shukrani ya ndoa lakini pia kuiweka hiyo ndoa katika ulinzi wa Mungu isijepata dhoruba kama wengine inavyowatokea. Hata Mungu mwenyewe amekubali kujaribiwa ktk matoleo ili tuone kama hatatufungulia milango ya baraka na hata ghala zetu zikafurika...

By the way huyo Bwana Harusi ameshakosea kwani Mungu anapenda tumtolee kwa moyo safi bila manung'uniko mioyoni mwetu.
Kwa kuwa Mungu wetu ni tajiri so hahitaji mali zetu bali roho zetu after all vitu vyote vilivyoko juu ya ardhi na chini ya bahari ni mali yake. Ubarikiwe sana.
 
Mimi nimefunga KKKT kwa sh 50000 niliambiwa ya vyeti,niliona ni sahihi,tumepewa vyeti vya serikali 2 na kanisa kimoja. RC na anglican ni zaidi ya kilo kuna mdogo wangu alilipa 150000 anglican church.
 
mnaona 100,000 bei ghali na ndo sehemu ambayo unapata kibali cha ndoa yako mbona ukumbi unalipa 1m mpaka 2m hulalamiki sehemu ya kuwapa watu mapombe....mshukuru MUNGU aliekupa uhai mpaka ukaamua kufunga hiyo ndoa
 
Kuna gharama nyingi mfano mimi roman.nilifunga ndoa. Kwaya 50,000. Msalaba wa ndoa 10,000 cheti viwili 30,000. Mafunzo 10,000. Mbona kawaida??
 
Kyalosangi nina wasi wasi huyo jamaa yako hajakueleza vizuri au pengine hujamuelewa. Siku hizi wachungaji wanafundisha hasa kwenye mafundisho ya wanandoa watarajiwa.

Unapofunga ndoa unapashwa kumshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyokutendea hasa ktk kipindi cha uchumba mpaka ukafikia siku hiyo ya kubariki ndoa. Kuna mambo mengi yanatokea kipindi cha uchumba. Hujawahi sikia mchumba anatoroka siku ya harusi anaingia mitini. Anaenda kwa boyfriend wake wa zamani?!!! Hivi wewe ukioa salama bila mikosi kama hiyo, Mungu utamshukuru kwa namna gani??

Hivyo wana ndoa wanafundishwa kumtolea Mungu ikiwa kama ni shukrani ya ndoa lakini pia kuiweka hiyo ndoa katika ulinzi wa Mungu isijepata dhoruba kama wengine inavyowatokea. Hata Mungu mwenyewe amekubali kujaribiwa ktk matoleo ili tuone kama hatatufungulia milango ya baraka na hata ghala zetu zikafurika...

By the way huyo Bwana Harusi ameshakosea kwani Mungu anapenda tumtolee kwa moyo safi bila manung'uniko mioyoni mwetu.
Kwa kuwa Mungu wetu ni tajiri so hahitaji mali zetu bali roho zetu after all vitu vyote vilivyoko juu ya ardhi na chini ya bahari ni mali yake. Ubarikiwe sana.

Mungu yupi huyo anayetaka 100000 na sio kwa kadri ya mtu impendezavyo kumtolea au kumjaribu Mungu.
mnatetea upotofu ama kwa kujua ama kwa unafiki.
iweje sacrament ipangiwe bei ?
nani kapofusha macho ya kiroho hata wana Mungu wakatetea uharibifu wa patakatifu ?
kanisa kuwekea bei huduma za kiroho !!!!????
 
Kweli wewe ni conservative ! ninachosema mimi kuwa KANISA limekengeuka ibada kama hii haistahili kulipiwa kiwango hicho! Ni kweli kueneza injili si lelelmama lakini tupime na maeneo ya kutoza hela!

mkuu hata wangesema ni senti moja bado mimi ningehoji hiyo price yag kwenye huduma ya kanisa, nani kawapofusha watu kiasi cha kutoliona hili ?
kuhusu cheti cha ndoa cha SERIKALI sina tatizo nacho kwa kuwa najua kanisa ni wakala wa serikali na naamini hakuna mtu atahoji lakini hili la kuweka visingizio ili kutumia huduma za kanisa tena sacrament kuwa miradi ya kiuchumi,hakika Yesu atawatenda zaidi ya wale waliokuwa wanafanya biashara ndani ya nyumba ya ibada, kwa kuwa waona Neema haikuwafikia bado.
kanisa lijiangalie upya !
 
Mkuu mrigariga.
Sasa gharama za vyeti. Msalaba. Mafunzo. Nazo bure????alipe nani??
 
Mkuu mrigariga.
Sasa gharama za vyeti. Msalaba. Mafunzo. Nazo bure????alipe nani??

kazi ya sadaka.matoleo.mafungu ya kumi etc etc ni nini ?
acheni kushabikia ukengeufu. na hii ndiyo inawavunja moyo watu wa Mungu ambao kimsingi wako tayari kutoa kadri ya Mungu alivyowajaalia...
 
Kuna gharama nyingi mfano mimi roman.nilifunga ndoa. Kwaya 50,000. Msalaba wa ndoa 10,000 cheti viwili 30,000. Mafunzo 10,000. Mbona kawaida??

yawezekema Mungu wenu sie mwenye mali yote, wenu anaishiwa inabidi achangiwe kinamna.
aibu sanaaaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom