Kiwanja cha meter 11x15 naweza jenga vyumba 3 na sehemu ya Parking?

kumbe maisha yanenda poa kuanza kumiliki gari then mjengo
Hiyo kawaida sana inategemea na mishe zako,Kuna mishe mtu inatakiwa uwahi afu ndo inakuingizia pesa so unaanza na usafir ili usave time kipato kiongozeke upate hela ya kujenga. Ila kama hela yako kupata kwa mwaka mara moja lazima utaanza kujenga.
 
nikiwa kwa kitanda peni na karatasi uwa havikosekani karibu yangu, na hii ndo wazo langu la haraka baada ya kuona hili bandiko. mchoro rahisi lkn wenye faragha kulingana na ukubwa wa kiwanja ambacho ni 11x15m. note: sijazingatia location ya kiwanja sbb sikijui

View attachment 1846543
Hivyo vyoo vije kati ya master na room ya mwisho
 
Hivyo vyoo vije kati ya master na room ya mwisho
yah inawezekana kabisa, lkn binfsi uwa napenda kuangalia faragha ya nyumba, ukiweka vyoo kama ulivyoshauri ina maana mgeni akitaka kwenda chooni atakua ameitembelea almost nyumba nzima sbb atapita dinning, master, kitchen na kwa karibu sana atakua amevikaribia vyumba vyote. nyumba nzur ni kwamba kama mgeni anataka kwenda toilet aishie mitaa hiyo hiyo ya sebuleni na sio kukross kwenye makorido ya kwendea vyumbani. pia ukiweka choo mbali kitawachanganya wageni na nirahisi kuingia vyumbani badala ya chooni labda uweka kibao kinachoonyesha toilet 🚻. sidhan kama utapenda!!!
 
Itakufa hii inafiti na parking unapata
Screenshot_20210717-210324_Xodo%20Docs.jpg
 
Ingia juiwaa la ujenzi na ramani huko mafundi tuko wengi, tatizo lako litaisha.
 
Good try but dinning ya mita mbili ni ndogo sana. Nyumba ndogo huwa haziwekwi dinning.

yeah kuna ka ukweli ikiwa standard ya dining table ya viti vinne tena umeibana meza inakuwa na upana na marefu wa 1m , hapo viti vyenyewe standard ni 40cm upana na bado hujaweka clearance ya kiti na kiti pia kati ya meza na kiti

aweke busati tu chini watu wakunje goti.. 🤪kiarabu zaid
 
Good try but dinning ya mita mbili ni ndogo sana. Nyumba ndogo huwa haziwekwi dinning.
Dinning ingeunganishwa na jiko au afanye open space design. Hicho kiwanja ukijenga ghorofa unapata nyumba na parking ya gari mbili na sehemu ya kuanikia nguo nyuma ya nyumba ndio unaweka mashimo ya majitaka. Ingia google tafuta nyumba za wafilipini check you tube AV properties utaona watu wanavyo shusha vitu kwenye space ndogo
 
nikiwa kwa kitanda peni na karatasi uwa havikosekani karibu yangu, na hii ndo wazo langu la haraka baada ya kuona hili bandiko. mchoro rahisi lkn wenye faragha kulingana na ukubwa wa kiwanja ambacho ni 11x15m. note: sijazingatia location ya kiwanja sbb sikijui

View attachment 1846543
Jiko limekosa hata mlango mkuu? Ila umeweka vizuri.
 
Hii hapa, size 9m×7.5m, ikikuvutia waweza nitafuta nikakupa full documents na maelezo zaidi kuhusu site plan

View attachment 1846963
Duuh! Hiyo kitchen umeiweka mkabala na sebule tena jirani kabisa na mlango wa mbele?
Nyumba yenyewe haina hata exit door.
Sasa moto ukizuka kwa hiyo kitchen na kukamata chakula ya moto (furniture), si utachomeka humo ndani kama ndafu?
 
Design hufanyika kulingana na nature ya eneo, ushaambiwa eneo ni dogo, huko nyuma anatokea wapi, kuhusu suala la usalama, nafikiri umekalili, dirisha linaweza tumika kufanya exit, huwa zinaachwa sehemu zinazofunguka. Tafuta wataalam wakushauri vizuri kabla ya kuanza ujenzi.
 
Back
Top Bottom