Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kufunguliwa

Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kufunguliwa

tutawatoa hawa ccm,wanakula bata mpk wanakufuru wanatuona sisi wajinga
 
Hizo 75% ya hisa za serikali zimeshindwa nini kuifufua hiyo kampuni?

Wakipewa hiyo 25% zilizobaki zitasaidia nini?
100% kuwa chini ya serikali ni matumaini yangu ile notion ya mali ya uma haipo vichwani mwa watanzania.
Maana hii ilichangia kuua viwanda vingi Tz.
Kwa upande mwengine serikali kama majority shareholder sijajua why walikuwa wanangojea kununua izo 26 share zilizobaki.
Ntafuatilia undani wake nijue shida nini
 
lowasa alisema akianza kampeni atatoa ufafanuzi wa kiwanda hiki.apa wameamua kuwai
 
lowassa ni jemedari hodari.Ndugu zangu tumpe uraisi huyu mtu
 
Leo serikali ya chama tawala imeamua kutangaza kuwa Kampuni ya General Tyre ilyopo Arusha itaanza kufanya kazi ndani ya muda mfupi baada ya kumlipa muwekezaji hisa zake na Kampuni ya ndege ya ATC ikisema itaanza safari zake za kwenda Mwanza siku chache zijazo hii ni jambo la kawaida je ni bunge lipi lilijadili na kuyapitisha haya?

Wakati wote serikali ilisema haina pesa hata ya kuendesha kampuni ya ndege pesa hizi zimepatikana wapi? Si ajabu mkasikia madeni yote ya waalimu na stahiki zao zimelipwa.

Naomba tujiulize pesa zote hizi wamezipata wapi, wanasema wanataka kutuondolea umasikini sisi watanzania haraka iwezekanavyo Lol kuna umaskini wakuondoa haraka haraka namna hiyo? Au kuna siri kubwa, walikuwa wanafanya makusudi?

Kumbe serikali ya tanzania ina uwezo wa kumfanyia mtanzania chochote kile, sasa nimeamini nchi ililiwa miaka na walitaka waendelee kuila hivyo hivyo kisa Lowasa alipokuwa arusha alisema atairudisha General tyre na kampuni ya ndege kwa vile wanamfaham ana siri zote za kuziua hizi kampuni ndio wameshtuka kabla hajasanua duh wana Jf it's too late kufanya yote haya mnasemaje ndio swali langu kwenu.
 
leo kwenye taarifa ya habari ya channel 10, katibu mkuu kiongozi balozi seif ametangaza kwamba serikali itakifufua kiwanda cha general tyre cha arusha mapema iwezekanavyo. Tunajua kwamba mh lowasa alipoenda kutafuta wadhamini mkoani arusha alitangaza vipau mbele vyake kimoja wapo ni kukifufua kiwanda cha matairi kilichokufa kwa muda mrefu, arusha general tyre. Sasa naona serikali ya ccm imeamka na kusema kwamba watakifufua kiwanda hichi. Sasa namwomba mh lowasa aendelee kutoa vipau mbele vyake kwenye kila mkoa, serikali inamsikiliza sana na wanajua anachosema ni kweli atafanya, sasa wanaamua kuamka. Bravoo lowasa, na serikali pia kwa kumsikiliza mzee wa maamuzi
lowasa ni kichwa bwana, tunakuombea afya baba, tuko pamoja, ulipo tupo.
 
Bunge la katiba limepitisha.....wanarusharusha miguu wakikata roho
 
Katika kikao cha Bunge aliyekuwa Waziri wa Viwanda natumaini Mhe. Nagu alidanganya wananchi katika hotuba yake kwenye Bunge kuwa Serikali itakifufua Kiwanda cha General Tyre mpaka leo ni danganya toto mpaka Mhe. Lowassa alipoibua wazo hili na hivyo imekuwa hoja ya CCM. WANANCHI KATAENI CCM ni walaghai Maji hakuna, Hakuna miradi inayoendelea mwaka huu na Halmashauri hazipelekewi fedha, Madawa ya kununua, wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo, watoto wanakaa chini. OGOPEMI CCM kama UKOMA.
 
Daganya Toto hyo ili wapate kura walikua wapi siku zote hizo kufanya hivo. Na kura hawapewi hata wakifufua viwanda vyote. Wakipata kura bungeni ni mipasho tu na kusema ndiooo hata kwa ujinga
 
Ccm Haiwezi Kutupeleka Popote Zaidi Tuwatoe Oktoba 25
 
Hawa ccm wanakumbuka shuka kumeshakucha hatudanganyiki lengo la kuiondoa ccm madarakani bado lipo pale pale mwaka huu lazima ccm iondoke .
 
Nina hakika sisi wazee wa( east africa )tutapata mafao yetu kupitia rais mtarajiwa edward lowassa
 
Back
Top Bottom