Barakaeli174
Senior Member
- Aug 2, 2015
- 171
- 142
Leo serikali ya chama tawala imeamua kutangaza kuwa Kampuni ya General Tyre ilyopo Arusha itaanza kufanya kazi ndani ya muda mfupi baada ya kumlipa muwekezaji hisa zake na Kampuni ya ndege ya ATC ikisema itaanza safari zake za kwenda Mwanza siku chache zijazo hii ni jambo la kawaida je ni bunge lipi lilijadili na kuyapitisha haya? Wakati wote serikali ilisema haina pesa hata ya kuendesha kampuni ya ndege pesa hizi zimepatikana wapi? Si ajabu mkasikia madeni yote ya waalimu na stahiki zao zimelipwa. Naomba tujiulize pesa zote hizi wamezipata wapi, wanasema wanataka kutuondolea umasikini sisi watanzania haraka iwezekanavyo Lol kuna umaskini wakuondoa haraka haraka namna hiyo? Au kuna siri kubwa, walikuwa wanafanya makusudi? Kumbe serikali ya tanzania ina uwezo wa kumfanyia mtanzania chochote kile, sasa nimeamini nchi ililiwa miaka na walitaka waendelee kuila hivyo hivyo kisa Lowasa alipokuwa arusha alisema atairudisha General tyre na kampuni ya ndege kwa vile wanamfaham ana siri zote za kuziua hizi kampuni ndio wameshtuka kabla hajasanua duh wana Jf it's too late kufanya yote haya mnasemaje ndio swali langu kwenu.