Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kufunguliwa

Kiwanda cha General Tyre cha Arusha kufunguliwa

NI Lowassa yupi unaemzungumzia? Kama ni huyu mamvi basi umeumia huyu jamaa kwanza mwizi tena fisadi isitoshe ni mtu wa visasi kumbuka Kilichomtokea mwakyembe Lowassa afai hata kuongaza nyumba kumi ikulu atisikia kwenye radio tu

Do you have evidence for all this allegations??? Or you are just provoking?? Cyber crime law is near the corner.
 
Huyo Lowasa ana ilani yake ya uchaguzi mfukoni or? Maana anayoyasema hatujui huwa ni ilani ya chama gani ndani ya ukawa. Au kuna ilani ya ukawa nini?

MKUU, kiongozi bora ni yule mwenye maono, unataka hata mambo madogo kama kufufua viwanda mpaka asubiri ilani..... yeye siyo kiraza kam kufuli la ccm
 
Ufufuaji wa hicho kiwanda kiko kwenye ajenda ya serekali, kilichochelewesha kuna kesi za madeni ambayo hayajamalizwa kati ya serekali na mbia wa mwanzo

Sio kweli. Serikali ilishatoa shilingi bilioni kumi miaka mingi iliyopita za kulipa hilo madeni na kufufua kiwanda. Mbia (Continental/General Tyre) alikuwa anadai dollar 2.4 million na HSBC walikuwa wanadai 2 million dollars. Deni likalipwa pesa iliyobaki Mramba, Shelukindo na mafisadi wenzao huko CCM wakazitia ndani kiwanda kikatelekezwa.
 
Kiwanda cha General Tyre kufunguliwa muda wowote kuanzia hivi sasa.Leo wajerumani wamekabidhi shares 26% kwa serikali hivyo 100% GT iko kwa serikali ambapo balozi Ombeni Sefue alishuhudia hilo tukio.
Hii kiwanda haifufuliki, kwanza kiwanda siyo kama nyumba unapakaa rangi nakuwekawa
Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara anasema muda wowote wanaweza kufanya trial run wanamalizia kurekebisha mifumo ya umeme, malighafi zipo za kutosha.

Chanzo: Channel Ten habari leo
Tatizo lililoko GT ni ushindani ulioko sasa hivi kwenye soko la tairi, ili kiwanda kiweze kujiendesha lazima uuze bidhaa bora na kwa bei ya ushindani hii ndiyo changamoto hata kampuni ya samir tyres ya Kenya ilikutananae hata baada ya moi kuzuia kwa muda tairi kutoka nje alivyo ingia kibaki mambo yakawa magumu tena,kwanza kipindi cha nyuma GT ilkua inapata mpira kutoka mashamba ya mpira nchini kwa bei nafuu leo mashamba yamebinafsishwa,hivyo itabidi uanze kuagiza mpira nje,halafu ushindane na hao wenye kukuuzia mpira kwenye soko la Tairi,wenye Viwanda karne ya 21 wamejipanga kuanzia upatikanaji wa malighafi kwa bei nafuu ili waweze kushika soko, ndiyo maana Dangote yuko mtwara mahali penye gesi na choka na malighafi mengine leo hii makampuni makubwa ya tyre zimejenga Viwanda vya matairi china na Vietnam siyo bure wanafuata malighafi,kwa hiyo Kama atafufua anaweza, lakini je litadumu muda gani?
 
Kiwanda cha General Tyre kufunguliwa muda wowote kuanzia hivi sasa.Leo wajerumani wamekabidhi shares 26% kwa serikali hivyo 100% GT iko kwa serikali ambapo balozi Ombeni Sefue alishuhudia hilo tukio.

Katibu wa Wizara ya Viwanda na Biashara anasema muda wowote wanaweza kufanya trial run wanamalizia kurekebisha mifumo ya umeme, malighafi zipo za kutosha.

Chanzo: Channel Ten habari leo

Kiwanda hakikufungwa kwa sababu ya 26% of shares; kilifungwa kwa sababu ya mtaji mdogo (working capital) na kuelemewa na madeni. Continental kuachia hizo 26% shares ni kwa vile hizo shares hazina thamani tena (worthless)
 
mtafufua vitu vingi sana mwaka huu..kama vipi mfufueni na komba aje awasaidie kwenye kampeni.kushindwa kubaya.....
 
Leo kwenye taarifa ya habari ya Channel 10, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Seif ametangaza kwamba serikali itakifufua kiwanda cha General Tyre cha Arusha mapema iwezekanavyo.

Tunajua kwamba Mh Lowasa alipoenda kutafuta wadhamini Mkoani Arusha alitangaza vipau mbele vyake kimoja wapo ni kukifufua kiwanda cha matairi kilichokufa kwa muda mrefu, Arusha General Tyre.

Sasa naona serikali ya CCM imeamka na kusema kwamba watakifufua kiwanda hichi. Sasa Namwomba Mh. Lowasa aendelee kutoa vipau mbele vyake kwenye kila mkoa, serikali inamsikiliza sana na wanajua anachosema ni kweli atafanya, sasa wanaamua kuamka.

Bravoo Lowassa, na serikali pia kwa kumsikiliza mzee wa maamuzi
Mleta habari anazungumzia mambo ya uchumi wewe unatumbukiza mambo ya SIASA!
 
Aliyekiua hicho kiwanda cha General Tyre ni nani? Na amechukuliwa hatua gani?
 
It's working. CCM hawakumtaka Lowassa kwa sababu wanajua rekodi ya uchapakazi wake! Yeye sio msanii akisema kitu anamaanisha.
Hongera sirikali

Ccm waliokuwa na sababu kuu tatu za kumkataa Lowasa 1)fisadi na mwizi 2) Mgonjwa 3, mbinafsi
 
JF inahitaji pongezi sana kwani imekuwa source ya habari nyingi sana nadhani hadi waandishi wa habari huwa wanashinda huku wakipita kila jukwaa kutafuta habari maana imetokea mara mingi kwenye taarifa habari naangalia taarifa ambayo nimeshaipata hapa Jukwaani na hata juzi serikali imeeamka nakwenda kufanyia kazi matatizo kwenye mgodi wa Tanzaniate one na mmoja wa mtu mkubwa sana ndani ya wizara hiyo nilipiga nae story akaniambia anaelekea Arusha migodon kuna shida wamepata kutoka mitandao ya kijamii...Na specific alitaja JF....BIG UP JF.
 
Sie wengine jamani...tunaomba na sisi mtupe hiyo habari
 
Na viwanda vilivyokua mkoa wa Tanga vikafa wamevikumbuka???? Kama kuna mkoa ulikuwa na viwanda vingi vikafa ni Tanga jamani uwiii...
 
Wafufue na viwanda vya nguo Mwatex,Mbeyatex,Sunguratex,Urafiki,bila kusahau vya zana za kilimo kv ZZK zana zetu kali UFI mbeya,viwanda vya kusindika nyama,Kiwanda cha Pareto Mafinga,nk
 
Back
Top Bottom