- Nov 14, 2010
- 2,114
- 1,384
Nasikitika sana kwa hali iliyotokea.
Jumapili iliyopita nilitumia kivuko hiki kuvuka kuja DAR, kwanza nilistuka sana kuona moshi mzito uliokuwa inautoa, na nilipoangalia kenye sehemu za maboya ya abiria niligundua kwamba zaidi ya nusu ya maboya hayapo (chanja zote mbili) na inaonesha yalikuwa yamepunguzwa kwa makusudi ama kuibiwa.
Pia uholela wa kuruuhusu abiria wengi kusongamana eneo la magari ni uzembe mkubwa wa wasimamizi ambapo kule chini hakuna maboya na hata kuyafikia yale ya juu ni mziki mzito.
Nilishajiapia kutopanda tena pantooni tangia siku hiyo kwa sababu ya uzembe wa makusudi wa pande zinazohusika na usalama na usimamizi wa kivuko kile.
Naamini hakuna atakayepata madhara labda mali zipotee au kuibwa na wajanja. Ila tangu MV Bukoba hadi leo Watanzania hatujifunzi lolote na tunazidi kuishi maisha ya roho mkononi kama wazoefu wa majanga