Kivuko cha MV Magogoni chaelea baada ya injini kuzima

Kivuko cha MV Magogoni chaelea baada ya injini kuzima

Poleni sana, vipi lakini mkulu wa kaya hakuwepo? magufuli nenda kapige mbizi uwaokoe.
 
Wanakusanya Milioni sio chini ya 18 kwa siku!!!! wafanyakazi wa pale 97% ni vibarua na hulipwa Tzs.100,000 kwa mwezi!! Pesa yoooote hiyo huendesha kivuko kibovu!! Hii serikali imelaanika!
 
Kishawekwa pembeni watu wameshushwa ma matechnician wamevaa diving suit na gesi mgongoni wanazama chini yake

Hizo zoooote ni sarakasi za kijinga!! Kivuko kina matatizo kwa takribani wiki sasa kinatoa moshi kama vile wanachoma matairi! diving wanakwenda kumwokoa nani??
 
Ufumbuzi wa kudumu ni daraja lililo mbioni kukamilika.
Sina amani na mapantoni haya siku zote.
Yana engine 4 lakini kila moja ni engine 2 tu ndo zinafanya kazi
na hamna linalo fanyika kuhusu engine zingine.
 
sixgates,faizafoxy na ritz1 na huyu lizaboni hapa watakimbia kuwa hayawahusu
 
Dar leo yaani kuna wengine walishaanza kugawa mirathi kwenye simu nawasikia live.
 
Na mwanzoni nilidhani wanafanya grill kumbe nikaja kugundua kweli kulikuwa na hitlafu..
Na nimeshangaa sana mana siku zote wanatumia engine mbili na ku-preserve mbili kwa kuhofia kufell zote,sijui imekuwaje zote zikazingua.
 
Mv magogoni imeanza kufanya kazi kama kawaida baada ya kufanyiwa matengenezo madogo.
 
Kwaiyo maboya yamekuwa dili,,,akipatikana mmachinga mmoja kujitolea kuuza maboya xmass kwake itakuwa nzuri,,kweli mjini shule

Hahha! Nimecheka sana ndugu.

Naamini kuna Wachaga washawahi Fursa Hiyo na sasa watakuwa wanauza hata Maputo.
 
Ufumbuzi wa kudumu ni daraja lililo mbioni kukamilika.
Sina amani na mapantoni haya siku zote.
Yana engine 4 lakini kila moja ni engine 2 tu ndo zinafanya kazi
na hamna linalo fanyika kuhusu engine zingine.

Ndugu embu piga hesabu ili kupanda daraja inabidi uende Kurasini kwa sister kule bandarini kutoka posta au KKO na ukivuka inabidi uje huku kigamboni maana wakazi wengi wanakaa kule.
 
Chezeya nchi inayoendeshwa kisayansi ya Wakwere weye!!!
CC: faizafoxy
 
Back
Top Bottom