Wanawake mnaona ujinga wenu hapa! Hebu jaribuni kuchunguza kama kuna la maana mlilomwambia mwenzenu haapa, pamoja na kuwaambia kuwa alishatendwa miezi minane iliyopita na ukiangalia hapa anawaambia anaenda kukutana na njemba nyingine. Woooote kwa umoja wenu hakuna hata mmoja aliyemshauri la maana zaidi ya kumwambia avaeji sijui apendeze. Mimi nilitegemea mumshauri mambo ya msingi pengine ni vitu gani akienda kuonana na huyo mdunguaji anayeenda kuonana nae. Hii ingemsaidia mwnzenu ambaye mpaka sasa ameshasema sijui ana mshawasha wa kuonana naye jamaa maa leo ndo mara ya kwanza anatoka naye.
Yaani wengi wenu huwa hamuwazi nini vya kwenda ku speculate from a man when you meet the first day. Kwa taarifa yenu huyu mwenzenu ingawa leo ndiyo mara ya kwanza anatoka na jamaa msishangae kama leo hii hii anadunguliwa huyu maana hata nyie hamjamshauri la maana zaidi ya kumpandisha 'mori' mwenzenu namna anavyotakiwa avae, akisha fanya hivyo atakapoonana naye akisifiwa kapendeza basi kwisha habari yake, na kweli nawaambia huyu anaenda kutoa mzigo.
Mi hata sielewi, hivi woooooote nyie kubwa la kumwambia kweli ktk hili la dating yake, mmeona ni mavazi kweli? Hata kama hilo ndo alowauliza, ni kweli mmeshindwa hata kumshauri aka speculate mambo ya msingi, yaani mmeishia kumshauri mavazi pekeee, loh! Kweli wanawake wengi mwalimu wao ni mmoja.
Kwa wewe mdada ambaye umepagawa mpaka huji nini cha kuvaa, wenzio ndo wameshakushauri nini cha kuvaa ili uendane na umbo lako la Lulu......jamani kwa nini Mungu asingetuumba kimawazo tufanane maana hii gender nyingine inapata taabu sana kukabiliana na changamoto zilizo mbele yao.....mweeeeeeeee!