Dr.adams faida
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 1,874
- 3,305
Habari za majukumu ndugu zangu?
Nimeamua nianzishe uzi huu ilitujifunze kwa wale ambao hatufahamu mambo haya:-
Imepita siku kadhaa baada ya ndugu yangu kukamatwa na maaskari kwa kosa la kumshambulia askari ambaye alikuwa doria.
Ilikuwaje?
Ilikuwa hivi, huyu ndugu yangu mida ya saa 2 usiku alikuwa yupo kwenye baa karibu na ofisi yake akipata moja moto moja baridi na rafiki zake kadhaa,kama unavyofahamu raha ya pombe kukojoa baada ya muda ikabidi atoke pembeni kidogo kuvuka barabara akawa anakojoa pembeni ya barabara.
Mara gafla akashikwa kwa nyuma na mtu ambaye hakujitambulisha akaanza kumuhoji unafanya nini hapo? Jamaa akajibu nakojoa kwa vile pombe ilikuwa imeanza kumuingia yule askari akamkaba koo ikawa ugomvi kwa vile ilikuwa usiku yule askari alivaa sweta hivyo hakutambulika kwa uharaka yule ndugu yangu akaomba msaada wenzake aliokuwa akinywa nao wakaja wakaanza kumshambulia yule askari pasipo kujua kama ni askari hii ni kwa sababu hakujitambulisha bali alitumia ubabe kumkamata mlengwa baada ya kama dakika kama 7 gari la maaskari wenye silaha lilifika eneo la tukio na kuwabeba jamaa wanne akiwemo na ndugu zangu.
Wakafunguliwa kesi ya kumshambulia askari, baada ya kuwekwa rokapu yule askari alidai alipwe fidia ya shilingi laki 5 ndugu wakajichanga ikapatikana kama laki 3 yule askari akazikataa zile pesa akadai mpaka pesa ikamilike yote.
Kesi ikapelekwa mahakamani huko ndo mambo mengi nilienda kujifunza.
Baada ya kesi kusomwa watuhumiwa walikuwa huru kwa dhamana ila kwa kukidhi masharti kuwa wawe na kila mmoja wadhamini wawili mmoja awe mtumishi wa serikali.
Ndugu wakapambana wakapata wadhamini wote lakini kimpembe ilikuwa kupata huo mdhamana kwa maana ilikuwa kila unayemfaata anamtupia mzigo mwenzie mwisho nikamfuata KARANI mmoja nikamuuliza kwanini tunazungushwa vile alihali tumeshakamlisha vitu vyote?
Akanijibu ni vyema nionane na hakimu moja kwa moja ambaye atatoa majibu nikamfuata hakimu kwenye ofisi yake akasema nisubiri mpaka siku ya kesi iliyopangwa ndio nitamtoa mtuhumiwa kwa mdhamana.
Nikamuuliza kwa remove order taratibu zake zikoje akajibu hakuna sheria ya namna ile hivyo ni maamuzi yake yeye hakimu kumtoa kwa remove order ama laah!
Kichwa kikawaka moto baadae akasema basi inabidi nimtafute baadae ili tuzungumze tena ila nikajua hapa pesa inatakiwa nikatoka ofisini ikabidi nimfuate KARANI nikamwambia nenda uongee na mheshimiwa basi atuweke wazi kama kuna chochote kinahitajika nijue.
Yule karani akaenda dakika chache akarudi akasema mheshimiwa amesema uandae laki 4.5 afanye mchakato fasta duuh nikajisemea moyoni kweli nchi hii bila pesa haki yako hupati.
Nikasema acha nitumie akili ya kuzaliwa nikaandaa kama laki 1.5 nikamfata hakimu nikamweleza mzee nimeambiwa niandae 4.5 hakimu akashituka akasema yaani huyu dada huwa tapeli kweli kwani hapo una bei gani sikutaka kumjibu nikampa mzigo mkononi.
Akachukua ile laki moja akanikabidhi ile 50 akasema mtafute mtu flani umpatie kiasi hiki mwambie jina la ndugu yako mwenye kesi.
Nikampata yule bwana nikampa mzigo nikatambua kuwa yule bwana ni wakili ambaye anashikilia faili la mtuhumiwa wangu.
Baadae akanitoa kando akananiambia niaandae kama 40 elfu.
Shilingi 30 nimtafute PP nimpatie na shilingi elfu kumi kwa ajili ya kuwapa maaskari ya mafuta wamfuate mtuhumiwa ili aje apate mdhamana ikanibidi mzigo niutoe kwa vile niilikuwa na shida. Na mwisho mtuhumiwa akatoka kwa mdhamana.
Sasa juzi kati mlalamikaji akatufuata akituomba eti tumpatie kiasi cha pesa japo laki 2 na laki moja tumpe mkuu wa kituo tukastuka kama kesi ipo mahakamani hizi pesa tunatoa kwa ajili ya nini?
Natamani kufahamu kwa watalaamu wa sheria ili nimsaidie ndugu yangu nitumie njia zipi kumuweka huru kwa maana napata wasiwasi kama haki itatendeka kwa vile pesa imetangulizwa mbele.
Kitu kingine ambacho nimejifunza ukiwa na kesi jiandae pesa ikutoke hata kama kesi ilikuwa ndogo kiasi gani hukuzwa ili mradi pesa ipatikane.
Kama rushwa ni adui wa haki leo sehemu ya kukimbilia haki zetu ndo kumejaa rushwa tutakimbilia wapi sisi wanyonge?
Pia kazi za hawa ni zipi mahakamani?
1.KARANI
2.WAKILI
3.PP
Natamani sana kujua kazi zao na pia elimu zao.
Karibuni kwa mjadala..