Kiukweli huwa sipendi usafiri wa ndege basi tu

Kiukweli huwa sipendi usafiri wa ndege basi tu

Aiseee........basi sawa........

Mwaka Jana nimequotiwa sama na mamen tu. 2015 nimeanza poa preta wasalimie huko afu ukipanda ndege tena utupie picha bila kusahau kale ka dirisha ka mviringo kaonekane
 
 
Last edited by a moderator:
Pilot ukipata nafasi angalia post # 85 kwa kweli kuna vitu vingine nimevijua kupitia hii link (50 minutes duration) wala sikuvidhania kama vinaweza kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege. Kuna mfano wametoa wa ile Concorde iliyoanguka pale Paris mwaka 2000, lakini usiogope unaweza ukajifunza mawili matatu ambayo yatakuwa na manufaa makubwa siku za usoni.

Hii thread inanipa huzuni kweli ...
 
Mie sijawahi panda ndege hivyo siwezi sema lolote. Ila kitakwimu aviation inaongoza kwa usalama.
 
Sijui lini na mie nitapanda nijionee tofauti

endelea kumuomba mungu usilazimike kuipanda....isingekuwa hii ajira nisingekubali kupanda ndege...usafiri gani roho mkononi!jk ana roho ngumu mzee yule!!!!
 
Hapa kila mtu atasema amepanda ndege jamiiforum bwana jaman waliokuwa hawajapanda pandeni hata vichater mkienda kwenu mm nikipandaga ndege nakula dawa za mafu za vichenga kwisha habar kulala mwanzo mwishoo

Unalala mwanzo mwisho afu nawewe unajihesabu umepanda ndege!? Lakn kweli,maana hata vifurushi navyo vilivyopanda ndege huongezeka ubora wake!
 
Unalala mwanzo mwisho afu nawewe unajihesabu umepanda ndege!? Lakn kweli,maana hata vifurushi navyo vilivyopanda ndege huongezeka ubora wake!

Inamaana ukipanda ndege alafu ukalala ww hujapanda ndege duu, ww Baba yake madenge itakuwa na ukipanda meli alafu ukalala baadae ww hujapanda meli na gari pia ukipanda baadae ukilala utakuwa hujapanda haya kaka mkubwa wa madenge unadhan kila alalae hulala kwenye sita kwa sita
 
Pandeni tu. Maana kifo popote hata mwenda kwa mguu nae hufa. Siku yako ikifika hata ukijifungia ndani ya safe utatoka tu.
 
Huwa nasikia kuwa usafiri wa ndege ndio wa usalama kuliko usafiri mwingine wowote (sijui kama ni kweli), lakini binafsi kati ya usafiri sipendi ni wa ndege na sababu kubwa huwa ninakuwa na hofu muda wote tangu ndege inapaa mpaka inashuka, na kama ni masaa mengi ndio kabisaa. Itokee sasa mmepita kwenye mawingu au hali mbaya ya hewa na ndege inayumba mpaka pilot anawaambia fungeni mikanda, halafu ukute ndio kwanza hata kufika bado labda kuna masaa kama manne mbele ndio mfike. Huwa nasali sana kila ninapoanza safari lakini kusema na ule ukweli nikiwa angani huwa sina amani kabisa mpaka pale ndege inapotua. R.I.P wote mliopoteza maisha katika ajali za ndege na nyinginezo.

Ni salama sana sema issue kidogo ipo kwenye kuinuka (dakika tatu baada ya kuachia ardhi) na kushuka (dakika nane kabla ya touch down). Hii kitu wenyewe wanaita 11 minutes ni very critical moment, na hapa ndipo hata crew members hawatembei!!

The Plane Crash - Articles - Improve Your Chances of Survival - Channel 4

Kwa nini ni salama sana? 1. care ni ya hali ya juu sana, 2. waongozaji ni wengi - marubani, control tower, technology kama vile transponder, 3. uko juu angani nako kuna highways yaani kila ndege inapewa njia yake.

Shida utokea pale human anapoingiza error aidha kutokuzingatia vigezo au kuondoa focus kuanzia yule anayetakiwa kuikagua, mkagua running way, control tower, rubani. Kitu kingine nafikiri baadhi ya marubani wanapuuzia vigezo hasa wa nchi zisizokuwa za western ingawaje nako huwa na ajali, mfano, AirAsia issue ni bad weather na rubani alilijua hilo; juzi huko UK Virgin ilikuwa inaenda Las Vegas, imeruka tu rubani akashtukia landing gear ina issue, akamwaga mafuta, akarudi chini faster! BBC News - Virgin Atlantic jet lands safely with landing gear problem

Hapa hakuna ile ya kibongo kichwa kinauma unasema ngoja nione kesho taamkaje.

Na ukitaka maisha yako yawe ya mafanikio fuata principle hii ya hakuna kusikilizia!!!
 
Kumbe hata wewe........mi nautumia sana kuja huko TZ kuangalia vitunguu vyangu Yaeda........

Preta From Mongolia.......

kule angani hakuzoeleki mpnz ni basi tu. bi mkubwa huwa analia tukiagana akifikiria masaa 10 angani
 
Back
Top Bottom