Mimi pia ndege zinanikosesha amani
nawaonea wivu walevi.....wanakunywa tu hawajui kinachotokea
Hapa kila mtu atasema amepanda ndege jamiiforum bwana jaman waliokuwa hawajapanda pandeni hata vichater mkienda kwenu mm nikipandaga ndege nakula dawa za mafu za vichenga kwisha habar kulala mwanzo mwishoo
Vichater ndio aina gani ya ndege?
Nilishawahi kuwa kwenye chatter ya watu wanne halafu wote tuna mabegi... ile safari ingekuwa angalau ni ya saa mbili; nadhani ningefika wakati pumzi zimekata kabisa!!Malia usingizi kwanza ndege zinasafirisha abiria mikoani via visawani vingi vinakuwa vichater namaanisha ndogo sio zile kubwa zinazootoka nje ya nchii
Kama usafiri wa majini ingekuwa umesambaa kama wa ndege au magari/mabasi basi my best option kwangu wakati wote ingekuwa ni usafiri wa maji... very safe, next airway. Usafiri wa gari ndo hivyo tena, hamna jinsi lakini hakuna usafiri ambao ninauogopa kama usafiri wa barabara... hususani kama barabara zenyewe ni hizi za kwetu ambazo regional roads zote ni single lane.... unashitukia tu kitu "vuuuuuuum" ukigeuka kukiangalia "kileeeeeeeeee" kinachanja mbuga.... hapana aisee!kwenye ndege nisipokunywa nitakunywa wapi,usafiri wa ndege mi naona ndo mzuri kwangu na pia najisikia poa,usafiri ninaoogopa ni wa majini.
Kama usafiri wa majini ingekuwa umesambaa kama wa ndege au magari/mabasi basi my best option kwangu wakati wote ingekuwa ni usafiri wa maji... very safe, next airway. Usafiri wa gari ndo hivyo tena, hamna jinsi lakini hakuna usafiri ambao ninauogopa kama usafiri wa barabara... hususani kama barabara zenyewe ni hizi za kwetu ambazo regional roads zote ni single lane.... unashitukia tu kitu "vuuuuuuum" ukigeuka kukiangalia "kileeeeeeeeee" kinachanja mbuga.... hapana aisee!
Suala la usafiri wa maji nalo linategemeana na asili ya mtu... kwa mfano mtu wa Iringa au Mbeya huwezi kumwambia kwamba usafiri wa maji ni salama halafu akakuelewa... usafiri wa treni nautamani sana lakini sijawahi kuujaribu! Sijaujaribu kwa sababu moja kubwa... kibongo bongo ningetamani sana nipande daraja la tatu ambako ni full kijichanganya sema kuna siku nilimsindikiza mshikaji aliyekuwa anatumia Central Line... aisee nikaona hii daraja la tatu yetu ni zaidi ya full kujichanganya... sema ndo vile tena watu have limited options.Aisee usafiri wa majini nauogopa sana naona,ila usafiri ambao naona usalama upo Sana ni wa treni,sijawahi kusikia ajali za treni yaani mara chache mno
Malia usingizi kwanza ndege zinasafirisha abiria mikoani via visawani vingi vinakuwa vichater namaanisha ndogo sio zile kubwa zinazootoka nje ya nchii
Usafiri wa ndege ndiyo salama kulinganisha na usafiri mwingine wowote,ila usafiri wa anga kwa bara la AFrica si kuaminika sana,ndege chakavu zinafanya kazi,vyombo vinavyosimamia usafiri huo barani humu vimeoza kwa rushwa,mbiundombinu mibovu,na sababu zingine kadha wa kadha....
Pilot ukipata nafasi angalia post # 85 kwa kweli kuna vitu vingine nimevijua kupitia hii link (50 minutes duration) wala sikuvidhania kama vinaweza kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege. Kuna mfano wametoa wa ile Concorde iliyoanguka pale Paris mwaka 2000, lakini usiogope unaweza ukajifunza mawili matatu ambayo yatakuwa na manufaa makubwa siku za usoni.
Asante sana Captain BAK nimeona hizo clip .
huwa napena kufuatilia sana kwenye internet, TV na kuongea tu na
watu wengine..
Nyingi ya hizo ajali ni combination ya
1.Human error (ambayo inaweza kusababishwa na rubani, air-traffic controller, engineer,hijackers etc )
2.Mechanical error (engine failure, blockages pressure instruments etc )
3.Weather( hali mbaya CB Cumulonimbus ambazo zinaleta thunderstorms etc.)
Kuna kitu kinaitwa "Aviation chain of errors"
na hii husababishwa sana sana na Human errors.
kama engineer ametoka nyumbani kagombana na mke wake
anafika kazini kachelewa, anaanza kazi lakini akili yake haiko hapo
anafanya vitu ambavyo sio sahihi ......Au rubani ameacha mtoto nyumani anaumwa
anafika kazini hajajipanga anaongezewa majukumu mengine hajakaa sawa yuko kwenye
ndege anaanza kupewe clearences na air traffic control, mara hafuati checklist vema...
Yaani hivyo vyote vina build up badaye inakuja kuwa kitu kikubwa na hata kusababisha ajali ..
ndio maana kuna somo moja muhimu sana linaitwa Human Factors marubani wote wamelisoma na unafundishwa
jinsi ya ku vunja hiyo " Chain of errors"..
cha mwisho ajali ni ajali tu .
Kuna za kupanga na ambazo hutokea bahati mbaya.
lakini ningependa kusisitiza usafiri wa ndege si mmbaya kama wengi
hapa wanavyofikiri.