Kiukweli huwa sipendi usafiri wa ndege basi tu

Kiukweli huwa sipendi usafiri wa ndege basi tu

Ingawa ndege Ni usafiri wa kuaminika lakini tatizo lake moja ikipata ajali Ni Mara chache Sana kusikia Kuna majeruhi ila Mara nyingi utasikia wote wamekufa tofauti na basi au meli
 
Napenda ile mbaya, siku zote my sit ni dirisha, my longest flight time Joberg-Sydney 11:50 hrs
 

Attachments

  • 1420239909770.jpg
    1420239909770.jpg
    31.9 KB · Views: 547
  • 1420239949507.jpg
    1420239949507.jpg
    32.3 KB · Views: 521
  • 1420239983462.jpg
    1420239983462.jpg
    30 KB · Views: 505
Kwa ushauri wangu kwa wale wanaoogopa usafirihuu.
Tafuta nafasi na fedha kidogo uende sehemu
Ambayo wanafanya pilot training au organisation yeyote ile yenye ndege binafsi . Utakaa kiti cha
Mbele na instructor atakuonyesha jinsi ndege inavyo take off, cruise, na Ku land . inasaidia sana na kupunguza uoaga ukisha ona jinsi kitu kinavyo Fanya kazi . na haita kuchukua muda instructor anaweza akakuachia control ukafnya one or two medium turns , climb, descending, .. Nusu SAA tu au lisaa inatosha kabisa kwa wewe kuona jinsi ndege inavyo Fanya kazi.
.
Kuna aviation ccollege hapo Dar inaitwa "Mosswood Aviation Academy " ..
Mikoani kuna mashirika mbali mbali ya ndege
Yanayo Fanya bush flying .
 
Usafiri wowote Waweza kukuletea ajari, haina haja ya kuogopa kwamwe....
 
Ndege ni kati ya usafiri ninaoutumia kwa IMANI tu ila nna mashaka nao,nikisafiri na gari naweza nisisali kabisa ila ndege uwiiiiiiii namkumbuka Mungu iweje chuma lielee kirahisi vile.
 
Huwa nasikia kuwa usafiri wa ndege ndio wa usalama kuliko usafiri mwingine wowote (sijui kama ni kweli), lakini binafsi kati ya usafiri sipendi ni wa ndege na sababu kubwa huwa ninakuwa na hofu muda wote tangu ndege inapaa mpaka inashuka, na kama ni masaa mengi ndio kabisaa. Itokee sasa mmepita kwenye mawingu au hali mbaya ya hewa na ndege inayumba mpaka pilot anawaambia fungeni mikanda, halafu ukute ndio kwanza hata kufika bado labda kuna masaa kama manne mbele ndio mfike. Huwa nasali sana kila ninapoanza safari lakini kusema na ule ukweli nikiwa angani huwa sina amani kabisa mpaka pale ndege inapotua. R.I.P wote mliopoteza maisha katika ajali za ndege na nyinginezo.
Naunga mkono hoja kwa 100%. Mi naonaga kama ndio nimeianza safari rasmi ya kuelekea kwa BABA! Basi tu
 
Nenda TCAA watakusaidia kukuelekeza namna usafiri wa anga ulivyo mzuri na salama.
 
Mi namshukuru sana Mungu kwani huwa nipo happy muda wote wa safar,kwa aina yoyote ile ya usafir, though hutokea wengine kuogopa lakin i believe kuwa"ajali yangu kamwe siwezi kuiepuka ni bora nikawa happy tu
 
Kwa mie ninaogopa usafiri wa ndege sio kwasababu si salama hapana....usalama nafaham ni wa hali ya juu mno.

Shida ni safari yenyewe ndugu ndio huwa hekaheka.....

Kama binadam huwezi kuzuia fikra za kujihami endapo tatizo linatokea...hiyo ndio shida, walau ingejulikana ndege huwa hazipati ajali kabisa hapo sawa...lakin huwa zinapata ajali na kati ya hizo chache huwezi jua kama na yako itakuwemo siku hiyo.

Nimewahi kutumia fastjet kwa route mbalimbali za hapa ndani na siku za nyuma ilikua poa sana.

Sasa juzijuzi hapa Novemba na Desemba nilisafiri kati ya Mwanza na Dar....maweeee.... wakati wa kukaribia kutua mwanza jamaa sijui alianzia kuishusha Tarimee...weeeee....ngoma ilikua chinichini ikawa inaelea kwa kupanda na kushuka ghafla kama kwa dkk 15 au 20 hivi nilikomajeee??

Kutua dar nako...jamaa sijui aliishushia kilombero...tulianza kuelea elea tena mle kitunda...Mungu wangu...sitak hata kukumbuka. Alafu wakati wa kutua mwanza...jamaa alikua anaichezesha kiuno kama mwewe vile....nilikosaje amani wandugu?? Hadi nikahisi bawa litaanza kugusa chini...alafu tunashuka pilot anasema welcome again kwa kuchagua usafiri wetu...nusu nimtukane.

Hawa jamaa sijui wakati mwingine wanafanya kusudi...utafikiri wao hawawezi kufa ikidondoka...wa.she..nzi.. sana aisee na vishati vyao vyeupe!
 
Ha ha ha....... SaidAlly nadhani nikisafiri na wewe ndege moja.........tutawaua abiria wengine kwa pressure.........sasa ukitaka kudance sawasawa.........panda ndege ya watu 4-12.........mambo ya ndege ni magumu sana kwa kweli.........sijawahi kuzoea na wala sitakaa nizoee............
 
Last edited by a moderator:
Humu n kwa waliopanda ndege mi bado, jamani tutaonana baadae kwenye thread zengine
 
Sijui lini na mie nitapanda nijionee tofauti

Pole mummy! Mwenzio nilikamatwa overstay, bahati mbaya walindaka na mshiko wa nguvu kiasi! Wazungu bhana, wakakataa rushwa, wakanikatia ticket ya Dsm! Walindaka asubuhi, ndege ya Dsm jioni yake!
Basi nikaonja na mimi! Mpk sasa nina uzoefu wa 8yrs kusindikiza na kupokea wajomba pale kipawa!
 
Sikuwahi kuzoea aisee , angalao pombe hunisaidia sana
 
Ha ha ha....... SaidAlly
.........panda ndege ya watu 4-12.........mambo ya ndege ni magumu sana kwa kweli.........sijawahi kuzoea na wala sitakaa nizoee............

Preta: Ni kweli kabisa ndege huwa haizoeleki na huwa nawashangaa sana wale warembo wazuri wanavyojiongezea maisha ya hofu muda wote kwa kufanyakazi kwy ndege.

kuhusu ndege ndogo nina experience mbaya zaidi na nimeisha andika wosia endapo nikifa na ikalazimika mwili usafirishwe kwa ndege..ni bora nizikwe na manispaa kuliko kuupakia kwenye hizo ndege ndogo nife mara mbili, nisije kuchelewa siku ya ufufuo maana vitabu vinatuambia haitakuwa mara mbili.

Nina rafiki alisafiri na ndege ya watu wanne toka Moshi kwenda Nairobi...jamaa alitapika ilibakia utumbo tu kutoka na alipofika alipitilizia hospitali na kulala huko wiki nzima.

Nami pia yalinikuta japo ndege ile ilikua nadhani ni ya watu 30 au zaidi kama sikosei maana hofu niliyoipata wakati napanda sikuthubutu hata kupepesa macho.

Kisa ilikua ni huu ubahili wetu, nilikua nasafiri btn DC na CA sasa kwa unafuu wa gharama nikanunua cheap ticket ambayo ilikua ni ya kuungaunga ndege. Bhanabhana....kumbe kuna sehemu zingine kuna kua na connection za ndege ndogo abiria mkiwa wachache, hilo mie sikujua...yesuuu....ilikua ni DELTA aisee....najuta. Kwenye ile ndege mbongo (black) nilikua peke yangu the rest ni wazungu alafu ilikua alfajiri flan ndio namalizia trip yangu ya kuungaunga...ndege yenyewe ni kama hizi rwandair injini zake zinaning'inia mkiani juujuu...wacha kabisa. Inaruka chinichini sasa hata upepo tu wa kawaida kidude hichooo...
yani ile panda shuka ya ghafla plus kutetemeka nikawa nahisi kama zile injini zinang'oka sasa.

Kwakweli ndege haizoeleki na tunapanda kwasababu hatuna jinsi...ni kama kukamua jipu hamna jinsi lazima uisome ili ufike.
 
Last edited by a moderator:
Ndege ni kati ya usafiri ninaoutumia kwa IMANI tu ila nna mashaka nao,nikisafiri na gari naweza nisisali kabisa ila ndege uwiiiiiiii namkumbuka Mungu iweje chuma lielee kirahisi vile.

Speaking of imani umenigusa... Mimi huwa naanza kusali one day before... Nikiinngia ndani naanza kufanya sala ya toba kabisa.... Aaagh basi tu ingekuwa kuna uwezekano ningekuwa nasafiri kwa gari
 
Back
Top Bottom