Huwa nasikia kuwa usafiri wa ndege ndio wa usalama kuliko usafiri mwingine wowote (sijui kama ni kweli), lakini binafsi kati ya usafiri sipendi ni wa ndege na sababu kubwa huwa ninakuwa na hofu muda wote tangu ndege inapaa mpaka inashuka, na kama ni masaa mengi ndio kabisaa. Itokee sasa mmepita kwenye mawingu au hali mbaya ya hewa na ndege inayumba mpaka pilot anawaambia fungeni mikanda, halafu ukute ndio kwanza hata kufika bado labda kuna masaa kama manne mbele ndio mfike. Huwa nasali sana kila ninapoanza safari lakini kusema na ule ukweli nikiwa angani huwa sina amani kabisa mpaka pale ndege inapotua. R.I.P wote mliopoteza maisha katika ajali za ndege na nyinginezo.