IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,184
- 7,820
Huko tambarare kila kipande kina mwenyewe mkuu, ukigusa tuu balaa labda ununue.Mimi sio mchagga lakini nimeishi moshi zaidi ya miaka 10 sasa na sina mpango wa kuhama. Tatizo kubwa la wachaga ni mila zao za kupenda kila mtoto (wa kiume na sometimes hata wa kike) lazima agawiwe eneo "kihamba" nyumbani kwao na ajenge huko.
Kiuhalisia, mkoa wa kilimanjaro hauna tatizo kubwa la ardhi naweza kusema tatizo lipo huko juu vijiji vinavyozunguka mlima kilimanjaro. Kule watu wanapapenda kwasababu ya udongo mzuri wenye rutuba na hali nzuri sana ya hewa, vijito visivyokauka na mazingira ya kuvutia ya kijani kibichi.
Lakini ukishuka uwanda wa chini barabara ya moshi -dar na moshi - arusha utaona maeneo makubwa sana ambayo watu wameyageuza mashamba ya mahindi na wakaaji ni wachache sana.
Olu in olu mkoa wa kilimanjaro ni mkoa wa tatu kwa udogo kwa Tanzania bara, ukizidiwa udogo na dar na mwanza tu.