Kituko cha mwaka - Wananchi wa Vunjo wamtuma mwakilishi wao Bungeni kuomba kupewa rasmi ardhi na Serikali ili kufanya makazi mapya

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,329
6,447
Yaani Mbunge wa Vunjo mwenye PhD anamwomba Waziri wa Ardhi awapatie Wachagga wa Vunjo ardhi kwingineko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu ni ili walime kwani kwao wamegawana ardhi kwa mila zao na kujikuta na vipande vidogo sana ambavyo mtu hawezi kulima. Eti wamesongamana, si mpunguze kuzaana.

Hivi huyu Mbunge na hao wachagga wenzie hawaijui Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu freedom of movement?

Hivi yeye mhe. Dr Kimei alipojenga Dar es Salaam na kupata ardhi kubwa Dar mbunge wake wa wakati huo ndio alienda bungeni kumuombea hiyo ardhi? Yaani kabisa anataka annexation ya mkoa wa Kilimanjaro! Au Vunjo nzima ni registered company?

Hivi hao Wasukuma waliojaa huko Mbeya na Morogoro waliomba wapewe hayo maeneo bungeni kupitia wawakilishi wao?

Kwa fikra zake kama hizi huyu bwana hafai kabisa kuwa kiongozi wa juu katika taifa hili kutokana na misingi yake.

 
Hivi yeye mhe. Dr Kimei alipojenga Dar es Salaam na kupata ardhi kubwa Dar mbunge wake wa wakati huo ndio alienda bungeni kumuombea hiyo ardhi? Yaani kabisa anataka annexation ya mkoa wa Kilimanjaro! Au Vunjo nzima ni registered company?
Anataka New Vunjo in Manyara, Mbeya, Tabora
 
Yaani Mbunge wa Vunjo mwenye PhD anamwomba waziri wa ardhi awapatie Wachagga wa Vunjo ardhi kwingineko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sababu ni ili walime kwani kwao wamegawana ardhi kwa mila zao na kujikuta na vipande vidogo sana ambavyo mtu hawezi kulima. Eti wamesongamana, si mpunguze kuzaana..
Weka na link hapa tumsikie pengine umetafsiri visivyo.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom