Kitimtim Bungeni: Wenje atolewa nje ya Bunge

Kitimtim Bungeni: Wenje atolewa nje ya Bunge

Nianze kwa kumnukuu Waziri Mkuu mstaafu Mh. Joseph Warioba.

''...Bunge limegeuka kuwa sehemu ya vichekesho, limekosa nidhamu linahitaji kuchukua maamuzi magumu,...” alisema Warioba ambaye alikuwa akizungumza na Televisheni ya Taifa (TBC1) jana asubuhi.

Tangu uchaguzi ukamilike mwaka jana na kuanza rasmi Bunge letu kumekuwa na matukio mengi ambayo yanaacha alama za kuuliza nyuma,la kwanza kabisa ni kutoka nje ya ukumbi wa bunge mara Raisi alipoanza hotuba yake nadhani wote tunakumbuka,baada ya hapo kumekuwa na muendelezo wa matukio mengi sana ya kurushiana vijembe na kutosikiliza/kutofuata/kukiuka na wakati mwingine kupinga kauli kutoka kwa spika au mwenyekiti wa Bunge.

Vitendo vya kuwasha vipaza sauti na kuzungumza bila kuruhusiwa imekuwa jambo la kawaida kwa sasa,kama mtakumbuka kuna mbunge aliwahi kuwasha kipaza sauti na kusema wafunge milango ili wapigane na mengineyo mengi hadi ilipelekea Spika kulifananisha Bunge na soko la k/koo (ila aliomba radhi kwa kauli hiyo).

Hebu wana JF tujadiliane katika hili,ni kweli Bunge limekosa nidhamu kama waziri mkuu mstaafu alivyosema!!,je ni uhuru wa kuongea au ndo maendeleo yenyewe au ni kitu gani kinachoendelea katika bunge letu???
 
Tundu Lisu ameomba muongozo wa mwenyekiti wa kikao cha Bunge akiomba athibitishe zile tuhuma alizozitoa asubuhi kuhusu waziri kusema uongoc TBC wamekata matangazo, upuuzi huu wa TBC sijui utaisha lini utadhani wanaonesha sinema ya x? kha!
 
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia), Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
quote_icon.png
By VIKWAZO
attachment.php
mbona hakuna anayerusha ngumi
 
mimi ni mpenzi wa miaka mingi wa kuangalia vipindi vya bunge lakini bunge la mwaka huu nimechoka nalo limetawaliwa sana siasa kwani inaonekana wabunge wengi wanaposimama kuchangia huwa wanachangia pumba na wengi huwa hawajui au sijui hawaelewi kanuni za bunge, nidhamu kwao kwa spika hakuna kabisa na hii imeishatokea kwa zitto kunyanyua kipaza sauti bila ruhusa spika leo tena wenje amefanya kitu cha aibu bungeni cha kubishana na spika, je? wanafanya hivi kwa kutokujua au ni makusudi, hii pia inaonekana kuwa kiongozi wa upinzani mh mbowe ana udhaifu, mbona bunge la 2005 hadi 2010 lilikuwa zuri na mh Hamad Rashid aliwaongoza vizuri wabunge wa upinzani na ikapelekea wanainchi kuwa na imani na upinzani na uchaguzi wa 2010 wakatuongeza wabunge wengine, lakini kwa mwendo tunaokwenda nao ndani ya ya bunge kelele nyingi, ubabe maneno yasiyo na staha na sidhani kama wanainchi wanafurahishwa na matendo ya wapinzani na hii itapelekea kutuadhibu katika uchaguzi ujao, chadema jirekebisheni!!!!
Pamoja na ugeni wako humu jamvini mbona tatizo liko wazi tu spika anaongoza bunge kama mkutano wa chama tawala na sio bunge la wananchi, hebu fuatilia kwa makini hoja zinazotolewa na kina Zitto ni pumba au za msingi ndio urejee na hoja yako
 
Tena amevaa kaunda suti ileile aliyovaa siku anapiga magoti! HA HA HA HA HA HA HA HA HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAAA!
Wale watoto watakuwa walimwambia kapendeza siku anawapigia magoti.
 
Filikunjobe alitetea kuondolewa kwa wenje

wamemtesa hadi sura imekua kama ya mtoto aliyenyimwa uji aisee
 
umejuaje kama hicho ndicho wenje alitaka kijadiliwe?

Asubuhi wakat Kambi ya Upinzani inatoa Maoni yao kuhusu Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi walisema hoja ya Wenje ilikuwa ni kuhusiana na suala hilo baada ya Vyombo vya Habari kuripoti toka J'2 na kisha Serikali kukaa kimya wakati tayar Mitaani kuna hofu juu ya usalama wa Samaki hao kutoka Japan.
 
Tupe chanzo cha taarifa yako ili tuamini kwamba ni kweli,au kama ni tetesi kuwa muwazi.

Kwa walioangalia Bunge jioni hii Mwenyekiti Mhagama kamwambia Waziri kwamba kwa kuwa suala la hao Samaki linagusa hisia za Watz wengi baada ya kuripotiwa na Vyombo vya Habari na kuhojiwa na Wabunge wengi kwenye Michango yao, basi Waziri wa Mifugo na Uvuv wakat anahitimisha hoja ya Bajeti yake aanze na kutoa taarifa juu ya Samak hao.
 
Nianze kwa kumnukuu Waziri Mkuu mstaafu Mh. Joseph Warioba.''...Bunge limegeuka kuwa sehemu ya vichekesho, limekosa nidhamu linahitaji kuchukua maamuzi magumu,...” alisema Warioba ambaye alikuwa akizungumza na Televisheni ya Taifa (TBC1) jana asubuhi.Tangu uchaguzi ukamilike mwaka jana na kuanza rasmi Bunge letu kumekuwa na matukio mengi ambayo yanaacha alama za kuuliza nyuma,la kwanza kabisa ni kutoka nje ya ukumbi wa bunge mara Raisi alipoanza hotuba yake nadhani wote tunakumbuka,baada ya hapo kumekuwa na muendelezo wa matukio mengi sana ya kurushiana vijembe na kutosikiliza/kutofuata/kukiuka na wakati mwingine kupinga kauli kutoka kwa spika au mwenyekiti wa Bunge.Vitendo vya kuwasha vipaza sauti na kuzungumza bila kuruhusiwa imekuwa jambo la kawaida kwa sasa,kama mtakumbuka kuna mbunge aliwahi kuwasha kipaza sauti na kusema wafunge milango ili wapigane na mengineyo mengi hadi ilipelekea Spika kulifananisha Bunge na soko la k/koo (ila aliomba radhi kwa kauli hiyo).Hebu wana JF tujadiliane katika hili,ni kweli Bunge limekosa nidhamu kama waziri mkuu mstaafu alivyosema!!,je ni uhuru wa kuongea au ndo maendeleo yenyewe au ni kitu gani kinachoendelea katika bunge letu???
Ungekuwa unafanya research ungeambiwa kuwa research question yako haina mashiko.Unauliza swali na jibu unalo.Au unaifanya jf kama kipima joto cha itv wanao sema asilmia kadhaa wamesema ndiyo au hapana au hawajui bila ya kuspecify idadi ya respondents?
 
Hizi ni zama za ukombozi kama ilivyokuwa miaka ya 1951 hadi 1961 Tanganyika au wakati wa kumchapa Nduli Amini 1978..Mungu awatie Nguvu sana wapiganaji wetu akina kamanda Wenje, kamanda Kafulila, kamanda Mdee, kamanda Zuberi Kabwe, kamanda Mnyika, Brigedia Mbowe, Field Marshal Dr Slaa na wengineo. Wapiganaji tupo pamoja nanyi kuikomboa Tanzania na pachimbike.
 
Kumbe kuongoza Bunge si kazi nyepesi! Kumbe Sylvester Masele Mabumba ni mbunge wa Dole!! Kumbe kuongoza bunge kunahitaji umakini!! Hivi spika na naibu spika wapo wapi hadi wanawaachia wenyeviti ambao nao wanaonekana wanapwaya!! Au hawa wakuu wa bunge wanakimbia mioto ya wabunge?
 
Hizi ni zama za ukombozi kama ilivyokuwa miaka ya 1951 hadi 1961 Tanganyika au wakati wa kumchapa Nduli Amini 1978..Mungu awatie Nguvu sana wapiganaji wetu akina kamanda Wenje, kamanda Kafulila, kamanda Mdee, kamanda Zuberi Kabwe, kamanda Mnyika, Brigedia Mbowe, Field Marshal Dr Slaa na wengineo. Wapiganaji tupo pamoja nanyi kuikomboa Tanzania na pachimbike.

Mkuu hili jashi lako limejipanga!!! Lina Brigedia (One star General) na Field Marshal lakini sijaona Two, three and four star generals!! Mbona gap ni kubwa!! Teh teh teh. Wengine hivyo ndio vyeo vyetu mkuu vitumie kwa umakini!
 
Nimeangalia sababu ya kumtoa wenge nje sikujua kabisa....yaani sijui?? Acha wanahabari watatueleza zaidi kesho mtandaoni..
 
waliogopa kumpa muda wa kuthibitisha palepale ndani ya Bunge alipotaka kufanya hivyo kwa hofu ya kuwa serikali itadhalilika, kwanini baadaye mwenyekiti ajidai kuwa na haraka na taarifa hiyo?

Lakini pili mwenyekiti amekuwa akiruhusu kelele za wabunge wa ccm wanapozomea wabunge wa upinzani wanapotoa hoja zao, kama ilivyotokea kwa Moses Machali MB. wa Kasulu NCCR Mageuzi wakati mwenyekiti anao wajibu wa kuhakikisha bunge lina utulivu wa kutosha kwa maslahi ya wengi.

Hoja yako haina msingi unaendeshwa na emotions za ccm, jitahidi huenda ukapewa ubunge wa viti maalum 2011.
 
Thinktank, upo sahihi kabisa. Kweli kuna haja ya kuangalia hawa CDM wanavyobehave bungeni. LAKINI, pale mbuge anaposimama na dharura yenye maslahi kwa taifa halafu unakataa kuisikiliza. Nadhani hii ni hatari sana kwa usalama wa nchi. Unless mwenyekiti atuambie alijua Wenje anaongelea nini. Anyways, thinktank you are quite right but remember; the way Wenje behaved is exactly how people are behaving now! Na wananchi wakishaona Bunge haliwajibii hoja zao basi watafanya mass uprising. Siamini kama CCM wanapenda kufikia huko!!! Swaga ya CDM ni PEOPLE'S POWER hivi swaga la CCM ni nini?
Kwa mtu yeyote mwenye busara hawezi kushabikia ujinga ulioonyeshwa na Wenje bungeni. CDM inabidi wawafundishe vijana wao umuhimu wa kutumia nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu kama wanavyoelekea saivi. Mbona kina Dr. Slaa walijivunia heshima sana kwa kutoa hoja nzito bungeni kiasi tena katika bunge ambalo lilitawaliwa na idadi kubwa ya wabunge wa CCM kuliko ilivyo sasa. Tunashuhudia wabunge kama kina wenje wakiwekeza sana katika vituko na fujo ambazo kimsingi haziwasaidii watanzania. Inavyoonekana CDM hakuna tena mtu wa kuvaa viatu vya slaa katika kutoa uwakilishi makini. Kinachojitokeza sasa ni fujo zisizo za msingi katika masuala yasiyo ya muhimu kwa taifa hili.
 
Wale watoto watakuwa walimwambia kapendeza siku anawapigia magoti.
Ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaa kweli wale watoto walimwambia umependedhaaa kweli ulivyotupigia magoti na thuti yako ndhuri kweli.... Huyo jamaa ni kilaza kupitiliza
 
Hao ndio watoto wa dr slaa! Wako kikazi zaidi!!
 
Nimeangalia sababu ya kumtoa wenge nje sikujua kabisa....yaani sijui?? Acha wanahabari watatueleza zaidi kesho mtandaoni..

Mkuu nadhani Mwenyekiti wa Kikao cha Bunge Ndg. Sylvester Masele Mabumba ALIHEMEWA
 
leo ilikuwa ni kizazaa bungeni baada ya mbunge wa nyamagana chadema kutolewa nje,ndipo pale mh Deo filipikunjombe alipotoka nje na kuwarushia maneno ya kejeli na kuwaambia wabunge wa chadema kuwa wanasumbuliwa na utoto ndipo walipokuja juu na kuanza kurushiana maneno kama watoto wadogo ambapo nusura wachapane makonde. aibu kweli hii!!! Tanzania yetu inaelekea wapi.?
 
Back
Top Bottom