Kitimtim Bungeni: Wenje atolewa nje ya Bunge

Kitimtim Bungeni: Wenje atolewa nje ya Bunge

Mbona ana fanana na Wenje wana undugu au mie naona vibaya ?
 
Tena amevaa kaunda suti ileile aliyovaa siku anapiga magoti! HA HA HA HA HA HA HA HA HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAAA!
 
Nadhani nchi zinazotaka kuendelea kwa haraka ni kujitahidi kuuza Vinavyopatikana ndani ya nchi na kuzuia mali toka nje kuja kuangusha soko la ndani.Hapa ni Athari zinazotokana na utegemezi unaoweza kuleta madhara kwa wananchi.WAZIRI ANONGEA NA ANATOA MAELEZO YA BAADHI YA SAMAKI AMBAO BADO WAPO SOKONI NA WATANZANIA SI WATAALAM WA KUJUA NI NINI KILICHOPO NDANI YA SAMAKI HIZO ILI KUJUNISURU NA MADHARA YA MIONZI.Hoja ni nzito sana bado.WAZIRI ANATOA CHETI CHA UASILIA KILICHOSAINIWA NA SUZUKI HUKO TOKYO NA KIBALI TOKA TFDA KUINGIZA SAMAKI.WAMEPATA BARAKA ZOTE..TUONE KINACHOENDELEA NA TUAMBIZANE TU.
 
Mimi simuelewi huyu waziri porojo kibao anataja hadi majina ya magari eti cheti cha ubora wa samaki kimesainiwa na Mr Suzuki nchini japan na kila aina ya blabla.
Waziri amemaliza porojo zake sasa tusubili punchline kutoka kwa wabunge makini hasa wa Upinzani.
 
Tujikumbushe na yale maziwa yenye sumu nadhani wizara hii inahusika pia
 
He is fast becoming my favorite...akiwa na PR mzuri this guy will go places....trust me. Kichwani hakuna kitu ila he comes across as likable
 
Mimi simuelewi huyu waziri porojo kibao anataja hadi majina ya magari eti cheti cha ubora wa samaki kimesainiwa na Mr Suzuki nchini japan na kila aina ya blabla.
Waziri amemaliza porojo zake sasa tusubili punchline kutoka kwa wabunge makini hasa wa Upinzani.
ujuha wa viongozi wetu sasa kama Waziri Suzuki ameidhinisha samaki hawani sumu sisi kitengo chetu cha atomic Arusha kinafanya nini? hatupashwi kuangalia upya? je kama Wabongo wame-forge cheti ili kuingiza hao samaki humu nchini?
 
Wachina husema -Ukitaka kumsaidia maskini usimpe samaki mfundishe kuvua.. Expression hii ililengwa haswa kwetu lakini maadam masikini mwenyewe anataka samaki na hataki kuvua. matokeo yake ndio haya!
Being Responsible na Accountable ni utamaduni ambao WaTanzania hatuna , kwetu sie haya ni ya Mungu!
 
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kushoto) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na baadhi ya wabunge wa upinzani Moses Machari (kulia), Philipa Mturano (katikati) na Ezekia Wenje (kushoto) baada ya Filikunjombe kumwambia Wenje kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
attachment.php
 
Namuona mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa tunae online hapa JF, bravo kiongozi, wakati wabunge wa CCM wanatumia muda huu kulala wabunge wa Taifa mnafuatilia mjadala bungeni huku Ipad, Iphone na Blackberry zenu mmelog in JF. hii ndio speed ya kisasa. be the first to know, mibunge michovu ya CCM inasubili kupata habari kwenye magazeti ya kesho.
 
Jioni hii, bunge kupitia kwa mwenyekiti wake Jenesta Mhagama limeiomba Serikali kuja na majibu makini kuhusu samaki walotoka Fukushima. Wenje alikusudia lijadiliwe kwa dharura.

Tupe chanzo cha taarifa yako ili tuamini kwamba ni kweli,au kama ni tetesi kuwa muwazi.
 
What next!! Tanesco wameishachukua chao; wenye access ya umeme tujuze juu ya sakata la samaki wenye sumu.
 
ujuha wa viongozi wetu sasa kama Waziri Suzuki ameidhinisha samaki hawani sumu sisi kitengo chetu cha atomic Arusha kinafanya nini? hatupashwi kuangalia upya? je kama Wabongo wame-forge cheti ili kuingiza hao samaki humu nchini?
Kwani hujui kama makamu wa Rais wetu ni Dr wa nyuklia?
 
mkuu umefanya vizuri kutujuuza lakini kama umeanzia njiani vle. Nini sababu ya huyu mheshimiwa kuzodolewa vile?
 
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti Maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto) Suzan Kiwanga (aliyevaa kitenge) na Mbunge wa jimbo la Kasulu mjini (NCCR – MAGEUZI) Moses Machari baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.

 
Mbunge wa Ludewa (CCM) Deo Filikunjombe (kulia) akisutwa nje ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa viti maalum (CHADEMA) Philipa Mturano (kushoto ) na Maryam Msabaha (katikati) baada ya Filikunjombe kumwambia Ezekia Wenje mbunge wa Nyamagana (CHADEMA) (hayupo pichani) kuwa alikosa ustaarabu kwa kutokumtii Mwenyekiti wa kikao cha Bunge cha leo Mbunge wa Dole (CCM) Silvester Mabumba pale alipomwambia akae chini na kutokutoa hoja ya dharula kuhusu samaki wa sumu kutoka Japan.
 
Back
Top Bottom