Kiteto: Wakulima mji wa Kibaya wagomea bei ndogo ya mnada zao la mbaazi

Sep 14, 2023
82
66
Mnada huo ambao ulitarajiwa kufanyika toka Jumanne, uliahirishwa mara mbili na hatimaye kufanyika Alhamisi 14/09. Wakulima zao la Mbaazi, walishangazwa na bei ya mnada kuwa chini kuliko matarajio.

Kwa masikitiko makubwa walitangaziwa Bei ya Tshs 2190/ Ukiniunganisha na Bei ya Mbaazi Kwa soko la Dar es salaam ambayo inauzwa Kwa Tshs 2400/ na zaidi

Tunaomba Serikali ingilie kati hili suala la Wakulima wa MBAAZI Kibaya - Kiteto

Tunaomba Bei ikiwa chini ya Tshs 2350/ kwa KG Moja basi watu wapewe kibali cha kusafirisha kupeleka Dar es Salaam
 
Mlio kwenye Mnada wa Mbazi Leo tunaomba Update Eli tujue tunafanyaje wengine tumetangulia mbele, kufuata Haki zaidi, Hima Wana Mibbaya tusiburizwe na kupelekeahwa Kwa Maslahi ya watu wachache Tupambane tupate Bei nzuri ya kuanzia Tshs 2400/ Kwa kg ndio Bei inayotakiwa na ndio iliyopo kwenye masoko mbazi ya Kibaya ni Bora kuliko Mbazi zote.
 
Mbaazi ni mboga nyie jitoeni akili,au manataka bei za 100tsh kwa kilo.

Chukueni mpunga huo maisha yendelee
 
Sihaelewa mantiki ya kugomea bei.
Sasa hapo tofauti ya Kibaya na Dar ni 250 mtu anataka apewe kibali aprleke dar atapeleka na ungo?
Hatalipia usafiri?
Hatakula njiani?
Hatalala lodge?

Akili za usiku hizi
Gharama za usafiri Kwa Semitrela la kupakia Gunia 300 ni 1.5M ukigawa gharama zake za ote ni chini ya 70kwa KG? Na tofauti ya Soko la Kibaya ni zaidi 200/ Kwa kg chikulua mtu ana KG 60000 mara Tshs 200 ni zaidi ya Tshs 12M jee hiyo ni ndogo
 
Walio nyuma ya hili soko wanajulikana na Muda sio mrefu watajulikana na ikibidi tuweke wazi majina Yao na maslahi Yao?
NEXT .... episode... Downloading
Yajayo yanafurahisha Kila kitu kutakuwa wazi Wacha nirudi kutoka safarini Dar es salaam nikiwa Kibaya nitaweka wazi Kila kitu
 
Sijaelewa mantiki ya kugomea bei.
Sasa hapo tofauti ya Kibaya na Dar ni 210 mtu anataka apewe kibali aprleke dar atapeleka na ungo?
Hatalipia usafiri?
Hatakula njiani?
Hatalala lodge?

Akili za usiku hizi
Pamoja na kulipa gharama zote Bado mtu atapata Faida, Kama Bei inalipa hapo Kibaya kwanini watu walaximishe kuingia gharama?
Kama Bei ni nzuri hapo kwanini watu walazimishwe kupeleka ghalani?
 
Kwa mara ya kwanza ukombozi wa watu wa Kibaya utapatikana kwenye mambo mengi tunayoburuzwa Kila siku. Wacha tusubiri.
Yajayo yanafurahisha , Muda ni rafiki tusubiri tuone
 
Sijaelewa mantiki ya kugomea bei.
Sasa hapo tofauti ya Kibaya na Dar ni 210 mtu anataka apewe kibali aprleke dar atapeleka na ungo?
Hatalipia usafiri?
Hatakula njiani?
Hatalala lodge?nyanya iashara

Akili za usiku hizi
Kwa mfanyabiashara ashapiga hesabu zote hizo Soko lipo wazi, unapakia kwenye gari mzigo inapokelewa sokoni , na Hela unawekewa kwenye akaunti yako , kusafiri wanasafiri watumishi wasiojuwa Mipango mizuri ya matumizi ya Hela tupo kwenye Digital era unapima mzigo unajuwa KG zako then unapakia kwenye gari , unaingia gharama za usafirishaji bidhaa tu wewe inaendelea na mambo yako mengine.
Ndugu upo Dunia ipi ya kutaka kusafiri wewe na mzigo? Huo ni ushamba uwe unauliza kwanza ndugu
 
Inaitwa biashara. Unauza kama unaona faida. Usiwaze mwenzio anaenda kupata sh ngp Dar.

Piga hesabu zako za kulima kuhudumia adi kuvuna, kama ukiuza kwa iyo bei unapata faida uza, ata kama mwenzio anauza Dar mara 2 yako.
 
Kusafirisha hadi Dar, unaweza ukapta hasara kubwa sana, kwanza madalali+garama za kusafirisha
 
Inaitwa biashara. Unauza kama unaona faida. Usiwaze mwenzio anaenda kupata sh ngp Dar.

Piga hesabu zako za kulima kuhudumia adi kuvuna, kama ukiuza kwa iyo bei unapata faida uza, ata kama mwenzio anauza Dar mara 2 yako.
Nafikiri wengi ni madalali
 
Gharama za usafiri Kwa Semitrela la kupakia Gunia 300 ni 1.5M ukigawa gharama zake za ote ni chini ya 70kwa KG? Na tofauti ya Soko la Kibaya ni zaidi 200/ Kwa kg chikulua mtu ana KG 60000 mara Tshs 200 ni zaidi ya Tshs 12M jee hiyo ni ndogo
Mkulima mwenye kilo 60,000 sio mdogo uyo. Ebu tuongelee wakulima wadogo wadogo.
 
Mkulima mwenye kilo 60,000 sio mdogo uyo. Ebu tuongelee wakulima wadogo wadogo.
Kwa muda huu ni mwishoni mwa Msimu wakulima wengi wadogo walishauza mbazi Toka Mwezi August , Kwa Sasa zimebaki Kwa wakulima wakubwa, Hao wakulima wadogo huwa wanauza pale wakivuna tu, huwa hawasubiri habari za mida, Piya mbazi watu huwa wanachanga kupakia kuanzia Tani Moja ambapo Tani kumi fuso wanaweza kupakia watu watano Hadi Saba, wakiuza sokoni Hela inatumwa Kwa mtu Moja wanagawana, maana gharama za soko zipo wazi Dar es salaam
 
Kwanini
Inaitwa biashara. Unauza kama unaona faida. Usiwaze mwenzio anaenda kupata sh ngp Dar.

Piga hesabu zako za kulima kuhudumia adi kuvuna, kama ukiuza kwa iyo bei unapata faida uza, ata kama mwenzio anauza Dar mara 2 yako.
Nisipeleke sokoni Dar es salaam mwenyewe nikapate Bei halisi ya Soko. Gharama za kilimo zipo juu sana, Kuna changamoto nyingi sana kilimo Cha Kiteto wafugaji kulisha mashamba ya wakulima hiyo inapunguza kipato Cha mkulima na kufanya gharama za uendeshaji wa kilimo kuwa Juu, Eli mkulima aweze kukabili hizi gharama lazima apate Bei nzuri.
.Kilimo Cha. Mbazi Kwa Kiteto ekari Moja unaweza pata Gunia Moja ama liwe chini ya Gunia angalia gharama za Kulima ekari Moja ni shilingi ngapi?
Ndio upige hesabu hiyo Bei na kipato Kwa ekari Moja ndio changamoto kubwa, ukiwa unajadili angalia ekari Moja mtu anavuna kiasi Gani? Kwa sisi tunaolima pori namba Moja mwaka huu tumekosa kabisa Mazao Shambani , tunatefemea hicho kidogo tulichopata kwenye Mbazi
 
Back
Top Bottom