Kitendo cha kuwakatalia Wakurugenzi wa Kenya na kuruhusu wengine ni ubaguzi

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
3,912
2,000
Tanzania tumekuwa na tabia ya kuwakatalia Wakenya kwenye nafasi za juu vibali vya kazi huku tukiwapa wale wengine ambao sio Wakenya bila sababu ya Msingi.

Nimesikia Mkurugenzi wa Cocacola Kwanza kakataliwa kibali wakidai kuna Watanzania wenye uwezo lakini vilevile Mkurugenzi wa Voda naye wa Kenya alikataliwa kwa sababu hizohizo.

Cha ajabu mfano Voda hiyo nafasi hajapewa Mtanzania badala yake idara hiyo hiyo ya uhamiaji imempa kibali Hisham Hendi ambaye katokea Misri.

Sasa Tanzania ina vigezo gani vya kutoa vibali? Hii inashangaza sana. Lakini ukienda kwenye viwanda vingi kuna wahindi wengi tu wana vibali ambavyo wenzetu wa EAC hatuwezi kuwapa.

Hii inaonyesha sio sera bali ni chuki binafsi kama tunanyima tunyime wote lakini isifikie mahali kujidharau wenyewe maana kumuona mtu kutoka Misri ni bora kuliko Mkenya ni sawa na sisi kujibagua wenyewe.

Hii haiko sawa maana haitasaidia Watanzania kujiamini wala kusaidia kampuni za nje kuamini watu weusi kama wenyewe tunajibagua bila sababu za msingi.
 
Tripo9

JF-Expert Member
Sep 9, 2009
3,728
2,000
Una maana gani? Una maana wakenya ni bora kuliko wamisri? Una maana ni lazima wakenya wawe considered kwanza kabla ya watu wa mataifa mengine? Una maana hatuna uhuru wa kumpa mtu mwingine kabla ya wakenya? Huu ni ujinga wa aina fulani. Tanzania is a sovereign state.
"Tanzania is a sovereign state"🙇
Hiki kibwagizo mpk kinachosha.

Namsaidia mleta mada.
Reasons zinazowekwa public kukatalia wakenya ni kua kwani sisi hatuna mtu wa kujaza hizi positions mpk aje mkenya?
Then hizo hizo position tunakuja skia kapewa mtu mwingine mgeni.
NB: sitakujibu hata ukiijibu hii post sema nita like post yako. Maana nimehisi ni mmoja wa wale mtu akisema anything against mawazo ya wale anatazamwa kwa jicho la tatu wakati kiuhalisia facts ndio mpango mzima especially Karne hii.
 
emmanuel mruma

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,389
2,000
Una maana gani? Una maana wakenya ni bora kuliko wamisri? Una maana ni lazima wakenya wawe considered kwanza kabla ya watu wa mataifa mengine? Una maana hatuna uhuru wa kumpa mtu mwingine kabla ya wakenya? Huu ni ujinga wa aina fulani. Tanzania is a sovereign state.
Ishu ni kwamba wananyimwa wa Kenya kwa kusema hata watanzania wapo wenye sifa matokeo yke hawapewi watanzania wanapewa watu wamataifa mengine tena ya mbali.
 
UmkhontoweSizwe

JF-Expert Member
Dec 19, 2008
4,306
2,000
Ishu ni kwamba wananyimwa wa Kenya kwa kusema hata watanzania wapo wenye sifa matokeo yke hawapewi watanzania wanapewa watu wamataifa mengine tena ya mbali...
Aliyekwambia kuwa lazima wapewe wakenya ni nani? Hata tukikosa watanzania, kwani ni lazima wapewe wakenya? Acheni kujifanya kama nyie ni bora kuliko watu toka nchi zingine. Hide your stupidity by arguing like an intelligent person.
 
Randy orton

JF-Expert Member
Apr 29, 2019
262
1,000
Kwahiyo kunya anye Kuku ila akinya bata ameharisha!!

Hapo Kenya kuna mkurugenzi gani mwenye asili ya Tanzania kwenye Kampuni yeyote kubwa ya Kikenya.

Angalau sisi tuliwapa nafasi kwenye makampuni yetu na mashule, huko kwao ndio waanzilishi wa kubaniana fursa so its tit for tat.
 
Laki Si Pesa

JF-Expert Member
Dec 20, 2018
3,446
2,000
Aliyekwambia kuwa lazima wapewe wakenya ni nani? Hata tukikosa watanzania, kwani ni lazima wapewe wakenya? Acheni kujifanya kama nyie ni bora kuliko watu toka nchi zingine. Hide your stupidity by arguing like an intelligent person.
hujaelewa, kampuni ya VODACOM ndio ilimchagua mkenya awe mkurugenzi wa VODACOM TANZANIA , Serikali ya tanzania ikamnyima kibali, kampuni ya vodacom ikamchagua tena mmisri awe mkurugenzi wa vodacom tanzania, serikali ikampa kibali, hiyo ndio hoja ya mleta mada
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
4,010
2,000
Kwahiyo kunya anye Kuku ila akinya bata ameharisha!!

Hapo Kenya kuna mkurugenzi gani mwenye asili ya Tanzania kwenye Kampuni yeyote kubwa ya Kikenya.

Angalau sisi tuliwapa nafasi kwenye makampuni yetu na mashule, huko kwao ndio waanzilishi wa kubaniana fursa so its tit for tat.
🤣🤣
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
4,010
2,000
hujaelewa, kampuni ya VODACOM ndio ilimchagua mkenya awe mkurugenzi wa VODACOM TANZANIA , Serikali ya tanzania ikamnyima kibali, kampuni ya vodacom ikamchagua tena mmisri awe mkurugenzi wa vodacom tanzania, serikali ikampa kibali, hiyo ndio hoja ya mleta mada
Hebu nisaidieni...

Katika DIPLOMASIA Serikali zina uwezo wa KUMKATAA balozi mkaazi wa nchi nyingine kwa SABABU MBALIMBALI....

Je Serikali haina MANDATE kisheria kumnyima MTU VIBALI vya kazi ima kwa mtumishi mgeni wa kawaida hadi wakuu wa MAKAMPUNI makubwa?!!!
 
pendomamtefu

JF-Expert Member
Jul 9, 2018
1,765
2,000
Yaan kama kuna watu nawachukia basi ni wakenya. Hivi ni hiyo kuongea kingereza ndo munawashobokea hivi? Aisee... ama ni zile confidence zao zinawafanya muwaone wa muhimu sana? Naomba ufatilie jinsi wanavyotubagua huko kwao. Katafute kama kuna mtanzania ana hizo positions kwenye maofisi yao huko. Tena wanyimwe haswa.

Wamekuja wakenya hapa tuliingia nao ubia kilichoikuta kampun yetu Mungu anajua. Wana ujuni sana. Wanajikuta wajuaji kila kitu. Wameblock account kibao za wateja mpk kampuni imeshindwa jiendesha. Tulivyokuwepo wenyewe mambo yalikua mazuri kbs. Wao wamenipa positions kubwa na mamishahara makubwa. Na wanapenda kupelekesha watu balaa.

Ifike mahali tuache kuwalea jap watu. Simpendi jiwe ila kwa anachowafanza wakenya am very okey. Huwa wefanya kama shamba la bibi hapa. Kwanini usiseme mtanzania and si mkenya? Ama kisa EAC? kwani si kuna AU pia?

Mbona watanzania kibao tu wenye uwezo wapo. Wabaki kwao. Usije ukasema sisi ni wazembe. We are also good ila ni priorities that matters. Tuna haki ya kumkataa yeyote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom