KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Kaka Worm, nimejaribu kuandika maana ya baadhi ya hayo maneno,lakini Waungwana wengine Ruksa kunisahihisha;

1. Fala - Mjinga,Mzembe.

2. Nyomi - Wingi.

3. Mdebwedo - Nafikiri neno hili lina maana sawa na Mdabwada
(nguo chakavu)

4. Mswano - Nzuri,neno hili lina asili ya kigogo.

5. Tinginya - Kubwa.

6. Chelea Pina - Mambo poa/mambo mazuri
(Neno hili lilikuwa linatumiwa sana kwenye
gazeti la sani)

7. Msela - Mjanja,Bitozi.

8. Mneli - Sifahamu maana yake.

9. Msuba - Bangi,Hashish,Ganja,Jani kubwa etc

10. Fyatu - Kupungukiwa akili,kichaa.
 
Naona bwana Mwawado ametoa maana sahihi kabisa ya hayo maneno. Ingawa kuna mengine naomba kumrekebisha na kuongezea maaana ya yale aliyoshindwa.

1. Fala

2. Nyomi-wingi ( Ukumbi wa harusi ulikuwa nyomi-ulijaza watu)

3. Mdebwedo- Ni neno ambalo limeingizwa hivi karibuni na vijana wanavichekesho (The comedy), maana yake ni rahisi, nyepesi, siyo ngumu ( maisha mdebedo, au mtihani ulikuwa mdebwedo)

4. Mswano

5. Tinginya (Nene, hasa kwa wanawake wanene, pia wengine husema nyambizi, mtu/mwanamke mnene)

6. Chelea pina

7. Msela

8. Mneli - Ni msokoto wa bangi

9. Msuba

10. Fyatu
 
Mheshimiwa Mtu Maana halisi ya neno "kukandamiza" ni sukuma (push) chini kwa nguvu,mara nyingi mkandamizo unakuwa na egemeo la kitu yabisi kama Ardhi au Ubao,Lakini kwa kiswahili kipya neno kandamiza linatumiwa kwa maana ya "ONEA" au "UONEVU".

Hapo kwenye post #53 ya YournameisMINE kuna maneno 10 ambayo yote yanaendana sawa kwa maana isipokuwa wakati na mahali pa kuyatumia,nitarudi baaadye kujaribu kuyanyambulisha.Maneno mengi yaliyoandikwa hapo hayapo kwenye kamusi kwa sababu ni maneno mapya kwenye jamii.
 
Hapa nimepata wazo kuhusu maana ya maneno....GLOSSARY. Vipi kuhusu technical terms kwenye siasa, uchumi, sayansi, sheria, ICT nk?

Naanza na neno la kiingereza: co-opetition. Naomba wenye maelezo wanieleweshe.
 
CHUNA kwa mtazamo wangu mi naona ni kutoa ngozi kutoka sehemu ya mnyama au kitu chochote kile ambacho kinaweza kuchunika.
PILI kwa maana nyingine ni kumchunia mtu yaani kutoongea naye.

MKWARA- ni kumtishia mtu kitu furani ili akuogope, mfano mzuri tu ni hivi karibuni wanamziki wetu hawa KIKOSI CHA MIZINGA walivyowachimbia mkwara CLOUDS FM kuwa wasipige nyimbo zao. huo ndio mkwara so umenipata........!

MSANII hili ni neno ambalo chimbuko lake nimetokana na neno ni sanaa. ukiwa unaigiza unaitwa msanii na kwa maana nyingene iliyoibuka hivi karibuni ukitapeli mtu tu unaitwa msaniii au hawa wabongo wenzangu hapa town "mission town" ni wasanii tu wanaishi kwa kuigizaigiza kisanii kisanii tu hii ndio maana halisi ya msanii......!!

jr....!!!
 
Wandugu!

Hivi kwa nini tunawaita African Americans "wanugu?"

Je nugu ni neno la kiswahili? If so, lina maana gani?
 
Jamani waungwana naomba jibu kamili maana ya tafsili halisi ya neno "fisadi" maana naona hao watuhumiwa wanapunguza ukali wa neno na kudai eti, "nimewekwa kwenye list of shame" sidhani kama fisadi maana yake ni shame naomba tulitafutie jina jingine lenye nguvu na maana sawa kwenye kingeleza.:)
 
kwa mujibu wa kamusi mpya ya Kiswahili sanifu, Fisadi ni mtu mbaya,mtongozaji,mharibifu,mpotevu, mwasherati, kama vile guberi.
Nadhani kwa tafsiri hiyo labda naweza kusema sio sahihi sana kama ni kutambulisha watu walioko kwenye list of shame, ingawa hao jamaa wa kwenye list of shame wanaweza kuwa na hayo yote lakini definition fupi ya kiingereza ni........ lack of integrity or honesty (especially susceptibility to bribery); use of a position of trust for dishonest gain.....hapa ukiwa ni pamoja na kutoa kupokea milingula, ten percent, danganya toto nyingi za kuwafanya wananchi wajinga, unawaambia tunajenga shule kumbe wanajenga vibanda vitakavyobomoka baada ya miezi sita. Kuna mambo mengi sana yanayohusiana na hii.
 
QM,
ninavyojua mimi NUGU au Wanugu ni neno Nigga ambalo limetoholewa kwa kiswahili. Jamaa wa NYC ndio walianzisha hiyo in mid 90s......kama latinos, waswahili wanawaita "wanyola" kutokana na Espaniola!!! mambo ya East Coast hayo.

Nimekupata... Lakini kwa nini tulibadilisha "i" kuwa "u" kwenye Nigga?

Najaribu ku-imagine sentensi hipi, kati ya hizi mbili, ina rhyme vizuri wakati wabongo wanakonyezana kuhusu African American anayepita mbele yao:
1. Ebwaneee check Mniga huyo na bling bling zake
2. Ebwaneee check Mnugu huyo na bling bling zake
Interesting...

Anyway, nilikuwa sijui kuwa Latino tunawaita "Wanyola"
 
Jamani naomba mnisaidie, hivi 'MAMABO' ni neno gani tena hili, maana nimeliona hapa jamvini mara kadhaa sasa... asili ya neno hili ni nini?! Ahsante.

SteveD.
 
Ndugu, naomba mnipatie tafsiri au ufafanuzi wa neno 'thread' kwa kiswahili kama itumikavyo kwenye forum hii.

Je,neno jarida/daftari/ukurasa yanaweza kufaa kama tafsiri yake ya kiswahili?

Nyongeza; kwa sababu nauliza swali hii karibia na mwisho wa juma kuanza na kwenye shamlashamla za Eid, nawasihi basi kwa wale wepesiwepesi wa kuchombeza na maneno kuwa tayari nimeshafikiria neno 'kamba' na 'uzi' na nafikiri hayafai kuwakilisha neno thread kama litumikavyo kwenye forum hii. Ahsanteni.

SteveD.
 
Nifahamhuvyo mimi ni kuwa neno kiva ni jina la watu ambalo zaidi hutumika huko upareni.Lakini pitapita yangu kwenye mtandao imenipa picha tofauti na kunifanya nipoteze mwelekeo wa maana ya neno hilo.Hebu soma habari hii hapa chini,na utoe ufafanuzi kama unaufahamu zaidi

Kiva CEO to lecture at Monmouth College Thursday

Monday, October 22, 2007

MONMOUTH - Matt Flannery, co-founder and CEO of Kiva.org, will deliver the Wendell Whiteman Lecture at 11 a.m. Thursday in Monmouth College's Dahl Chapel and Auditorium. It is free and open to the public.
Kiva, which derives its name from the Swahili word for "agreement," is a non-profit organization based in San Francisco that provides modest loans to entrepreneurs in developing countries. While the "microlending" concept is not unique to Kiva, Flannery and his wife, Jessica, who will join him on stage, developed the idea of allowing ordinary individuals to become microlenders using the Internet.

More information on Kiva is available at www.kiva.org.

Source: http://www.register-mail.com/stories/102207/EDU_BEMHA4O4.GID.shtml
 
Tulianza kuambiwa "Kanye" ni "The only one" kwa Kiswahili, sasa "Kiva" ni "Agreement", mhhh kwa mwendo huu itabidi nitafute tuition ya Kiswahili.
 
Kweli kiswahili kinakua,Lakini napata wasiwasi kwamba maneno mengine watohoa kutoka kwenye lugha zao.Nakwasababu kiswahili ni lugha inayokuwa,basi watu hutumia mwanya huo kujitungia maneno na kusema ni neno la kiswahili.Baraza la kiswahili linahitajika kuratibu maneno kama haya,na ikiwezekana kurekebisha pale inapobidi.Ni kweli lugha inakuwa lakini je maneno yanayotumika nia sahihi?

Soma hapa chini maana ya neno Hulu.


October 28 2007

Hulu Launches Private Beta, Makes Very Good First Impressions


http://www.techcrunch.com/2007/10/28/hulu-launches-private-beta-first-impressions-very-good/

--------initial press release, we gave the joint venture a lot of grief for failing to pick a name for the project, eventually settling on a name - Hulu - that meant “cease” and “desist” in Swahili
 
Please Mimi ningependa kujua tafsiri ya maneno yafuatayo; A copule of thousands, a couple of hundreds
 
Ukiitwa Mswahili Maana Yake ni nini ?-Kikwete
Ni kweli baada ya kumchafua Salim A. Salimu anampa nafasi kamati kuu,baada ya kumuwanika Salimu kuwa ndiye aliyehusika kumuuwa Rarume kwenye magazetila mwananchi wakati wa kampeni 2005.
 
Back
Top Bottom