KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Wazee nashukuru kwa msaada wenu...

Ama kweli nimeelimika. Nilikuwa sichangii lakini nasoma kila kinachoandikwa.

Hivi, nini atakiwacho kujibu mtu akiambiwa maneno haya:

1. KARIBU - ?

2. Usiku mwema - ?

3. Alhamsiki - ?

4. Karibu tena - ?

6. Pole kwa kazi - ?

Hayo 6 ni mwanzo; nitaendelea endapo nitajibiwa na kufafanuliwa.

Ahsanteni


Karibu - Asante
Usiku Mwema - Na wewe
Alhamsiki - Alhamsiki
Karibu tena - Asante (ila usirudi endelea na safari!)
Pole kwa kazi - Asante nshapoa!
 
Ah, lakini bado nahitaji mawazo zaidi. Wakijibu wanne kwa namna ulivyonijibu Kijana Mwanakijiji (j.k) basi nitaamini ni sahihi.

Shukrani kwa ufafanuzi wako wa kwanza... Walau najua kuwa majibu ni:

Karibu - Asante
Usiku Mwema - Na wewe
Alhamsiki - Alhamsiki
Karibu tena - Asante (ila usirudi endelea na safari!)
Pole kwa kazi - Asante nshapoa!

Nitakuwa nawajibu hivyo watu kwa sasa hadi nipate jibu tofauti au msisitizo.

Asante (japo nilidhani mwanzo kuwa ni Ahsante)
 
inategemea unaweza kuandika "akhsante", au kimwanakijiji "asante" hasa kama kwenu hamna sauti ya "kha".... ambayo inapatikana katika lugha ya kiarabu!
 
Nadhani neno "Shukrani" lina-fit badala ya asante/ahsante.

Siku njema Mwanakijiji
 
Neno Shukrani pia linatokana na neno la kiarabu "Shukran". Waarabu wengi wanatamka hivyo au kusema hivyo badala ya ahsante/asante.

Lakini jamani angalieni neno hili "WANYE" ambalo limetumiwa na mwandishi huyu. Ametumia neno hili vibaya. Hapa alitakiwa kuandika "Wenye visus vya ukimwi". Wahamiaji hawawezi "kunya" virus vya ukimwi.
Mfano: Hatuwezi kulazimisha watu "wanye" virus vya ukimwi.
"mtu anye"
"watu wanye"

KISWAHILI NI LUGHA YETU LAKINI TUNAKIFAHAMU VIZURI ?

...........................................................................................................

Waziri Mkuu wa Australia apingwa kwa kukataa wahamiaji wanye virusi vya ukimwi

2007-04-14 16:23:44
Na EAR Habari
Mashirika mbali mbali ya misaada duniani, yamekasirishwa na hatua ya waziri Mkuu wa Australia Bw. John Howard kupinga wahamiaji wenye maambikizi ya virusi vya Ukimwi kuingia nchini humo.

Akiongea na radio moja wakati wa ziara yake mjini Melbourne, katika jimbo la Victoria, ambapo aliulizwa juu suala hilo, kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya Ukimwi nchini humo, hasa katika jimbo hilo, Bw. Howard amependekeza kupigwa marufuku kwa wahamiaji walioathirika kuingia nchini humo, kwa madai kwamba hatua hiyo inaweza kupunguza ongezeko la maambukizi.

Hata hivyo wanaharakati wa mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Ukimwi nchini Australia wamesema kwamba sheria ya uhamiaji ya nchi hiyo tayari ina vipengele vinavyowabana waathirika, ambapo pia Taasisi ya taifa ya misaada Uingereza, imeyaita mapendekezo hayo kuwa ni kinyume cha sheria na ya kibaguzi.
· SOURCE: EAR

IPPMEDIA
 
Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Compyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo


Vukiza au fukiza ni kitendo cha kufuka moshi ulio kwenye chombo maalumu kwa lengo maalumu kwa mfano kufukiza ubani.
Vundika ni kitendo cha kuweka matunda mahala kwa lengo la kuyafanya yaweze kuiva haraka, kwa viazi au muhogo kitendo cha kutaka kuivisha kwa joto kali ni kufumbika.
Compyuta= bado nalifanyia kazi.
Mtandao= Ni uwepo wa hali ya watu kuwa katika aina fulani ya utekelezaji wa jambo fulani liwe halali au la, lakini bila kujulikana wazi wazi.
Ila= Ni hali ya kutokuwa na ushirikiano endelevu kati ya mtu na mtu. Mmojawapo anakuwa na ile roho ya kwanini. Mtu huyu ni mwenye ila.
Ingawa= Maana yake hata kama...
Msanii ni mtu mwenye kipaji cha masuala ya burudani kwa malengo mbali mbali, mfano mchoraji, mwimbaji, mchezaji sinema (Kumbuka Mchezaji Mpira si msanii)
PUCHU= Nisubiri natafuta jiibu lake
MKWARA= Ni aina ya kuonyesha maguvu, mbele za watu kuonyesha wewe ni mtu mwenye nguvu au uwezo wa kupata taarifa unazotaka kwa kuwa wewe ni usiye shindwa kitu. Unachimba mkwara kupata taarifa fulani.
MWAKE=Maana yake ni ndani yake
CHUNA= Kitendo cha kutoa aidha ngozi ya mnyama kwa kitu chenye makali
au ngozi ya mmea kwa lengo la kupata aina nyingine ya usaidizi katika kutekeleza majukumu mfano KUCHUNA kamba.
MBONGO= Ni mtu aishiye Tanzania
 
MADA HII ENDELEVU NAMI NAOMBA MNISAIDIE YAFUATAYO:-

Mtu mmoja aliingia katika hoteli moja na alipofika alikaa muda mrefu bila mhudumu kufika kumhudumia. Baadaye aliende Meneja wa hoteli ile kumsikiliza yule Bwana aling'aka ... unaona siku zote nakwambia hawa wahudumu wako wapo hapa kwa kutafuta mabwana. Ona nimefika muda mrefu bila wao kunilete "kinywaji". Alipoletea alilalamika kuona hajapewa "glasi" ya kunywea. Baada waliingia wateja wengine na kuketi karibu yangu nikamsikia mmoja anaagiza; Naomba uniletee chai na "vitafunio"vile pale akiwa anaonyesha vipande vya keki.

Katika tafakari yangu nilikosoa baadhi ya maneno waliyotumia hawa jamaa.
Mteja wa kwanza aliyelalamika kwamba hajaletewa "vinywaji" tangu afike pale alikosea kwani kinywaji ni kinywa chake. Kile alichotakiwa kuagiza ili akinywe ni "Kinyweko" Na glasi aliyolalamikia ni "kinyweleo" cha kinyweko kile.
Kuhusu wateja wa kundi la pili nikaona makosa yao ni kuita keki kuwa ni "kitafunio" wakati ukweli ni kwamba keki ni "kitafunwa"
Naomba nanyi wenzangu mtoe mchango wenu tuweze kuboresha kiswahili chetu kinachoenda mrama katika enzi hizi za utandawazi.
NAWASILISHA
 
Kwa kiingereza wanasema "open the pandora's box" yaani ukitaka maneno ya kiswahili ambayo yana utata hayataisha. Kuna neno TAKO au ******=Kiswahili wanamaanisha "Buttocks" lakini maana halisi ya maneno haya ni "need/s" na buttocks ni makalio.

Pia wadau naomba mnisaidie tofauti kati ya MSENGE na SHOGA.
 
Puchu - kwa kiswahili cha mtaani ni punyeto, mfano kijana akimwomba msichana anaweza kumwambia 'nimechoka kupiga puchu' yaani nimechoka kupiga punyeto!
Mwake - pia kwa kiswahili cha mtaani inamaanisha belonging there! Mfano karibu mkjj hapa ni 'mwako' mwana wane. mwake = pake = mahali pake.
 
MSENGE ni mwanamume anayetiwa na wanaume wengine.
SHOGA pia ni mwanamume anayetiwa na wanaume wengine lakini naye aweza kuwatia vile vile.
Waswahili mwasemaje?
 
Kitafunwa ni chakula ambacho kiko kwenye hali ya yabisi, ili ukimeze inabidi ukitafune hence kitafunwa! Mara nyingi yatumika kwenye vyakula vinavyoliwa ama kutafunwa mtu akinywa chai/kahawa ama kinywaji kingine. Kwa hiyo mfano wa kitafunwa ni maandazi, chapati n.k.
Kitafunio ni meno, yaani kiungo kinachotumika kutafunia.
Kinywaji ni kitu kinachokuwa katika hali ya majimaji, huhitaji kukitafuna ili ukimeze. Maji, juisi na pombe ni baadhi ya vinywaji.
Siku hizi watu wanapenda kusema kinywaji wakimaanisha pombe/bia! Na vijana wa mtaani hasa maeneo ya casablanca ama pr camp pale mwanamboka wakaenda zaidi kusema pombe/bia ni kilaji, ina maana ina maji na chakula. Kwa hiyo kilaji, kinywaji, kilauri yote inamaanisha pombe/bia.
wenye kamusi kichwani sijui mna hoja gani hapo?
 
Sijui kama hiki ni kiswahili cha kinyamwezi lakini nadhani kuwa:

(a) "Puchu" linaweza kuwa na maana ya kutokuwa na ladha. Kwa mfano chakula kilikuwa puchu puchu; kwa maana kuwa hakikuwa na viungo vya kutosha na hivyo kukosa ladha.

(b) "Kutiwa" lina maana ya kuwekwa. Kwa mfano maembe yote yale yalitiwa ndani ya kapu moja.

(c) "Shoga" ina maana mbili: kwanza ni rafiki wa kwaida wa kike kwa mwanamke mwingine, pili ni rafiki wa kujamiiana wa kiume kwa mwanaume mwingine.

(d) "Msenge" ni mwananme anayejamiiana na wanaume wengine kwa kutumia njia yake ya haja kubwa ili kujipatia mapato. Ni kama "kahaba" linapotumiwa kwa mwanamke.

(e) "Kinywaji" ni kitu chochote cha majimaji ambacho mtu anakunywa ili kujiburudisha. Kinywaji kinaweza kuwa pombe, togwa, soda, uji na kadhalika al-mradi tu kinanywewa kwa nia ya kujiburudisha. Dawa haziwezi kuwekwa katika grupu za vinywaji.


Mchango wangu kwa leo
 
Ndugu zanguni, kiswahili kimekuwa kwa kasi sana miaka ya hivi karibuni kiasi kuwa kila ninaposikiliza Star TV na Channel Ten kwenye internet huwa naachwa nje kabisa kutokana na msamiati unaoutimiwa na watangazaji. Kwa leo nauliza, je neno Unyanyapaa maana yake ni nini?
 
Yaani hakuna anayejua maana ya Unyanyapaa jamani? Mbona mmenisusia?
 
Yaani wote JF hamjui maana ya neno hili ambao kila sikua naliskia kwenye luninga
 
Kichuguu

Kwa tafsiri yangu isyo rasmi Kunyanyapaa ni kumtenga mtu kwa Kiingereza cha karibu ni Stigmatise or Stigmatization
 
Sasa linatumikaje katika sentensi:
1. Aliyetenda:
(a) Jumuia imemnyanyapaa mgonjwa
(b) Jumuia imemnyanyapaia mgonjwa
(c) Jumuia imemnyanyapaisha mgonjwa
.
.
.
.

2. Aliyetendewa:
(a) Mgonjwa amenyanyapaa na jumuia
(b) Mgonjwa amenyanyapaaiwa na jumuia
(C) Mgonjwa amenyanyapawa na jumuia
 
Back
Top Bottom