KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
Nimekuwa nasikia maneno haya lakini yananichanganya kujua matumizi yake sahihi.

Vukiza au fukiza?
Vundika au vumbika?
Kompyuta?
Mtandao
ila
ingawa
msanii
puchu
mkwara
mwake
chuna
mbongo

Ninayo maneno lukuki lakini nashindwa kuyaainisha yote hapa. Naomba wataalam wa lugha hii adhimu mnisaidie nitoke niliko walau hatua moja mbele katika kujifunza Kiswahili.

Ahsanteni
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,346
38,995
Haya nitaanza kukusaidia kidogo:


Vukiza au fukiza?
Vukiza linatokana na nahau ya "Vuka" yenye maana ya kupitisha kitu kwenda upande mwingine bila kukutana na kizuizi. Mf. Kuvuka mto, kuvuka daraja n.k Hivyo neno vukiza ni tendo lakutendewa ingawa neno linalotumika kwa usahihi ni "vukisha" na si "vukiza" Wakati mwingine watu wanalitumia neno hilo kwa makosa wakitaka kumaanisha "fukiza"

Fukiza ni nahau yenye maana ya kupepea moshi, gasi n.k kuelekea upande fulani kwa makusudi. Ni hapo basi watu wanafukiza ubani, wanafukiza moshi wa maji ya mwarobaini n.k


Vundika au vumbika?
Vundika inatokana na neno "Vunda" lenye maana ya kitu kilichoharibika na kuchacha kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu bila kutumika na kimefanywa hivyo kwa makusudi. Ni tofauti na kitu "kuoza" Ni kwa sababu hiyo watu wanavundika mchele, mtama, ndivi n.k ili kutengeneza pombe au matunda mengine ili kutengeneza mvinyo.

Vumbika, bila ya shaka linahusiana na kitu kuwekwa vumbi!!!

Ila na Ingawa
Neno "Ila" lina asili ya kiarabu ambapo maana yake haswa ni kusema "Isipokuwa" K.m Ni lazima mtu atii mamlaka ila ile isiyo ya halali!

Ingawa ni neno lenye maana ya "licha ya kwamba" au "pamoja na ukweli kuwa" au "hata kama". mf. watu walienda shule ingawa mvua kubwa ilinyesha!

Msanii ni neno lilatokana na neno "Sanaa". Aneyejishughulisha na sanaa huyo anaitwa msanii. Hata hivyo neno hilo siku hizi linatumiwa kuonesha kuwa mtu "ni mjanja mjanja na si mkweli" katika mambo yake.

Kwa leo hayo yatosha.
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
Nashukuru... Naambiwa computa si kiswahili fasaha. Ila huyu kanijibu kwa PM. Ati ni tarakirishi. Shukrani kwa walionisaidia. Nina maneno mengi ningependa wenye upeo wa kuainisha kama mheshimiwa Mzee Mwanakijiji alivyosaidia hapo juu. Kuna maneno yamesalia sijapewa majibu, nikipata nitafurahi.

Internet kiswahili chake ni kipi?
Mchakato ndiyo maana ya process?

Kuna neno linakuwa linatamkwa mara nyingi SANJALI je lina uhusiano na Mkabala?

Mzee naomba unisaidie kama unaweza. Nipo kizani na napenda kujifunza zaidi lugha hii kwa mapana. Ahsante
 

Kulikoni

JF-Expert Member
Aug 28, 2006
205
25
Nashukuru... Naambiwa computa si kiswahili fasaha. Ila huyu kanijibu kwa PM. Ati ni tarakirishi. ....

Yapata miezi miwili hivi sasa tangu nisanidi Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003 kipatikanacho hapa: Download details: Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003

Kwa hiyo violesura vyangu vya word, excel, outlook na power point vyooote viko kwa kiswahili. Ni burudani flani hivi I must say.. maana kuna maneno ya ajabu ajabu hata sijui waliotafsiri wameyatoa wapi, kwa mfano ... kujibu swali lako .. pahala pa "My Computer" pameandikwa 'Ngamizi yangu'. Sasa hata sijui computer kuwa Ngamizi inangamiza nini!
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
Duh, hao wamefurahisha. Basi wacha niitembelee hiyo link. Tunapenda wazalendo wa aina yako! Ahsante
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
Kuna maneno sijajibiwa lakini naamini kuna watanzania wanaweza kunisaidia. Kuna wanaosema Computer ni Tarakirishi, sasa naona kuna Ngamizi sijui ni lipi sahihi. Hivi hakuna mtanzania anayejua kiswahili chake kilichokubalika?

Nisaidieni tafadhali!
 

Maarifa

JF-Expert Member
Nov 23, 2006
4,504
2,816
I do think sometimes tunalazimisha maneno ya kiswahili na as a result hata haileti maana wala ladha ya Lugha. Computer ni neno geni, yaani halikuzaliwa na waswahili. Therefore kama yalivyo maneno mengine ya kigeni tuliyorithi whay not call it KOMPYUTA kama yulivyozoea yaani tunaandika kama tunavyotamka neno ingawa ni la kigeni.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,346
38,995
Haya niendelee:

Puchu - koswa, ni kama almanusura, mf. Aliponea puchu gari lilipomkaribia! kusisitiza mara nyingi husema puchu puchu yaani koswa koswa!!

Mkwara - kwa kifupi lina maana ya vitisho ambavyo mara nyingi havitekelezwi. Lengo ni kuhakikisha matokeo yanayotakiwa. Mf. Alimpiga mkwara kuwa ampe shilingi 50 ama sivyo atamuambia mama!

Mwake - sijaelewa umelitoa wapi maana lina maana nyingi na sijui ni ipi ambayo unaitafuta!

Chuna - maana ya kwanza ni kuondoa ngozi bila kukata nyama! lakini linatumika katika kiswahili cha mtaani kumaanisha mtu kuchukuliwa pesa zake kwa hiari yake lakini bila yeye kutambua analaghaiwa!

Pia lina maana ya mtu kutotaka kusema au kujieleza kwa namna yoyote ile kwa vile amekasirika au ameamua kutozungumza. Linaendana na neno "Nuna" ambapo aliyenuna ana sababu, aliyeu"uchuna" hataki kusema awe na sababu au la.

Mbongo, ni neno la kiswahili cha mtaani likimaanisha mtu anayetoka Bongo (kama nchi) au anayetoka Dar.. lakini siku hizi inakubalika zaidi kuwa mbongo ni mtu anayetoka Tanzania!!

Kompyuta kwa kiswahili sijui kwa nini inaitwa ngamizi. Kwa maoni yangu ingeitwa Kikokotoshi, kwani neno compute (ambalo ni chanzo cha neno computer) kinatokana na uwezo wa chombo hicho kukokotoa (calculate) hesabu kwa haraka kuliko kutumia kalamu na karatasi!
 

dondola

Member
Nov 14, 2006
29
7
I do think sometimes tunalazimisha maneno ya kiswahili na as a result hata haileti maana wala ladha ya Lugha. Computer ni neno geni, yaani halikuzaliwa na waswahili. Therefore kama yalivyo maneno mengine ya kigeni tuliyorithi whay not call it KOMPYUTA kama yulivyozoea yaani tunaandika kama tunavyotamka neno ingawa ni la kigeni.
Hapo Umenena:)
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
WoRM, umeridhika?

Mzee Mwanakijiji,

Nashukuru kwa namna ambavyo umekuwa ukinifundisha lugha yetu hii adhimu. Aidha nawashukuru wote walioonyesha ushirikiano kwa namna moja au nyingine.

Kusema ukweli SIJARIDHIKA. Ninayo orodha ndefu ya maneno yanayonitatiza na ningependa kujua kwa upana wake kabla Rwanda na Burundi hawajaanza kuitumia lugha hii na kunizidi kung'amua maana ya maneno ilhali mi mzalendo na mswahili asilia siyajui.

Baada ya kufatilia huku na kule nimekuja gundua kwamba neno Computer limechukuliwa kama Tarakirishi (as it computes) na si Ngamizi kama walivyoandika wengine. Hii inaleta maana walau. Nikaulizia neno Calculator nikaambiwa na mtu mmoja hivi kuwa ni Kikokotozi. Ajabu! Aidha kuna maneno kama Fridge ambayo naambiwa ni Jokovu, neno Mdau sijajua kama ndo Stakeholder au Shareholder. Lugha inanichanganya (inanizingua).

Natamani ningepata kujua maana ya maneno zaidi. Lakini kwakuwa umekuja lazima nikuvae ulivyo hivyo hivyo Mzee Mwanakijiji, naomba usinichoke. Nisaidie kujua maana ya sentensi hii:

Chama cha mlengo wa kulia/kushoto. Nimekuwa nasikiliza BBC nasikia usemi huu. Najifanya najua wanaongelea nini lakini hali halisi SIJUI!

Alhamsiki :-D
 

Kulikoni

JF-Expert Member
Aug 28, 2006
205
25
Puchu - koswa, ni kama almanusura, mf. Aliponea puchu gari lilipomkaribia! kusisitiza mara nyingi husema puchu puchu yaani koswa koswa!!

Mwanakijiji,

Nahisi kama neno hili umelichanganya, hapa umetoa maana ya Chupu badala ya Puchu. Na mara nyingi hutumika maradufu "Kaponea chupu chupu kugongwa na gari"

Neno puchu maana rasmi binafsi siifahamu, ila nimewahi kulisikia katika wimbo wa Dully Sykes uitwa Nyambizi. Wakati anambembeleza bembeleza huyo Nyambizi anasema:

"Aah! Nyambizi, nionee huruma mi sio kuchu,
Nipe japo kiduchu, mi n'shachoka kupiga puchu!"

Sasa kwa kweli sina hakika kuwa maana iliyotumika hapo ndio maana rasmi au ndio msanii kachomekea tu.

Ahsante.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
13,192
14,172
Kama ambavyo tulichukua neno baiskeli na kulifanya la kiswahili, sioni kama ilikuwa ni lazima kutafuta neno jipya kwa vitu kama computer badala ya kuiita kompyuta
 

MgonjwaUkimwi

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
1,320
835
Mdau ni stakeholder

Chama cha mlengo wa kushoto ni chama kinachofuata sera za conservatism na chama cha mlengo wa kulia ni kile kinachofuata liberalism. Mlengo ni position katika political spectrum yenye ncha mbili ambazo ni extreme: liberalism na conservatism
 

Ogah

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
6,228
1,515
lukuki ni neno litumikalo kwenye fedha tu na si vinginevyo.
mfano: Mwanakijiji ana fedha lukuki na si mwanakijiji ana maneno lukuki
 

Zacharia

Member
Mar 20, 2007
6
0
Kweli Watanznia tunasafari nzito kuhusu hiki kiswahili chetu. Ni kweli kabisa lugha yetu ya kiswahili ina uhaba wa maneno ambayo yanaweza kuwa na maana halisi ya kile kinachoulizwa.

Lugha yetu kwa hivi sasa inakuwa kwa kiasi kikubwa sana kwa pande mbili tofauti. upande wa kwanza ni ule wa kutohoa (kulichukua neno kama lilivyo kutoka katika lugha nyingine na kulitumia katika kiswahili)

Na upande mwingine ni maneno yaliyo kuwepo tokea nuda mrefu yanaongezewa vionjo flani almradi lugha ya kiswahili ilete burudani sambamba na hili neno hili hili moja linaweza kubeba maana zaidi hasa kwa lugha zetu za mitaani

mfano:-

Mchizi wangu - rafiki ,jamaa nk. (Mtu asiye timamu)
Msela wangu - rafiki, kijana nk
Kichaa wangu -rafiki jamaa nk (Asiyetimamu)
kachala wangu- rafiki jamaa nk
baharia wangu - rafiki jamaa (mhusika wa vyombo vya baharini kama meli)
mwana
mshikajiwangu - Rafiki jamaa (mkamataji wa kitu flani)

huo ni mfano mdogo wa maneno ya kiswahili kinavyozidi kukua

tuko pamoja jamani tasaidiane kuendeleza utamaduni wa kiswahili
 

Jizaledo

Member
Sep 5, 2006
89
13
Ila tu neno "vumbika" halihusiani na kuweka vumbi bali hutumika katika utayarishaji wa matunda machanga ili yalike na matumizi yake halisi hayahusiana na vumbi hata kidogo. Kuvumbika tunda kama vile embe ni kuliweka ili liive barabara. Kuiva kwa tunda hakuhusiani na kupikwa tunda hilo bali ni pale linapokomaa likalika kwa utamu wake. Kama halikuivia mtini ndipo hapo linapovumbikwa. Karibu mara zote tunda liitwalo fudu (limefanana na zambarau bali lenyewe haliko majimaji kama zambarau) uvumbikwa ndipo liive.

Ama kweli, kiswahili ni kitamu!


Haya nitaanza kukusaidia kidogo:

Vundika au vumbika?
Vundika inatokana na neno "Vunda" lenye maana ya kitu kilichoharibika na kuchacha kwa sababu ya kukaa kwa muda mrefu bila kutumika na kimefanywa hivyo kwa makusudi. Ni tofauti na kitu "kuoza" Ni kwa sababu hiyo watu wanavundika mchele, mtama, ndivi n.k ili kutengeneza pombe au matunda mengine ili kutengeneza mvinyo.

Vumbika, bila ya shaka linahusiana na kitu kuwekwa vumbi!!!


Kwa leo hayo yatosha.
 

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,009
11,932
Wazee nashukuru kwa msaada wenu...

Ama kweli nimeelimika. Nilikuwa sichangii lakini nasoma kila kinachoandikwa.

Hivi, nini atakiwacho kujibu mtu akiambiwa maneno haya:

1. KARIBU - ?

2. Usiku mwema - ?

3. Alhamsiki - ?

4. Karibu tena - ?

6. Pole kwa kazi - ?

Hayo 6 ni mwanzo; nitaendelea endapo nitajibiwa na kufafanuliwa.

Ahsanteni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom