Kiswahili kimezidi mno kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Je, upendeleo wa Uarabu dhidi ya Ubantu?

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,257
Kwanza kabisa napenda nianze kwa kukiri kuwa Kiswahili bado ni lugha inayonipiga chenga pahala pengi. Hivyo kuna pahala pengi katika hoja yangu nitachanganya na lugha ya Kiingereza, pamoja na kwamba ningelipenda sana kuepuka. Lakini hilo lingewezekana tu kama ningelikuwa na muda na uwezo wa kupangilia na kukumbuka maneno fasaha ya kutumia.

Pia nakili kuwa hii hoja sijaifanyia utafiti madhubuti kuhakikisha kuwa ina vielelezo vya kutosha ili kuchanganua na kufafanua mifano mbalimbali ambayo inaweza kutumika kuikoleza na kuipa msingi zaidi hoja yenyewe. Ni imani yangu kuwa wale walio bobea kwenye maswala ya lugha wanaweza kuiendeleza zaidi. Shukrani.
------------------ ***** --------------

Nitaanza;

Nikisema 'ngoko' au 'nkoko' Wasukuma, Wahaya na ninaamini makabila mengine mengi ya Tanzania wataelewa kuwa ninalotaka kulitaja ni jina la ndege tumjuaye kama 'kuku' kwa Kiswahili. Si makabila ya Tanzania tu, bali Wabemba wa Zambia, Washona wa Zimbabwe, Baganda wa Uganda nao wangelielewa.

Nikisema 'nzoka' au 'nyoka' vivyo hivyo makabila mengi yenye asili ya Kibantu yatanielewa.

Sawa, lugha nyingi zinakua na kuendelea kwa kuazima maneno kutoka kwenye lugha nyingine. Na maneno mengine yanajitokeza na kukua na kukubalika kama moja ya maneno ya lugha fulani kutokana na mazingira yanayozungukuka jamii.

Maneno kama 'swahiba', 'mstakabali', na mengine mengi yenye kusikika na kutamkwa kwa lafudhi ya pwani asili yake kubwa ni kutoka Kiarabu. Na ukweli wa mambo ni kwamba chimbuko la lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kiarabu.

Hoja yangu: Je, chimbuko la lugha yetu ambayo tumerithi, tumejifunza, tumeikuza na kuienzi ndiyo kipimo pekee cha uhalisia wa maneno tuyatumiayo katika Kiswahili chetu?

Kimfano, nasema hivi kwani leo hii nikija na neno fulani hivi kutoka katika lugha ya Kihaya na neno hilo hilo kuwa tafsiri ya kitu ambacho kinapatikana Uhayani lakini hakipatikani katika Pwani, lakini hapo hapo kitu hicho kikabahatika kuwa na tafsiri yake katika lugha ya Kiarabu; uwezekano wa neno la Kiswahili kutumia (au hata kunyambulisha tu hilo neno la Kihaya ili iwe tafsiri yake katika Kiswahili) neno la Kihaya ni mdogo kuliko ambavyo urithi au ukubalianaji wa tafsri ya neno hilo ungelikuwa ule wa kutoka kwenye neno la Kiarabu.

Sasa, hii (sijui niite dosari) favouritism ya Uarabu dhidi ya Ubantu inatokana na nini, is it the case for inferiority complex ya aina fulani hivi, elimu au nini haswa?! Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.

"Akhsanteni", "Shukrani", natanguliza "Fadhila" zangu, au basi niseme... "ndaga fijo", "mwabeja"?!

SteveD.

MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:
Historia imepinsishwa. Kamwe kiswahili si KIARABU hata siku moja ndio maana leo ukimchukua muarabu kutoka uarabuni hawezi kuongea kiswahili vivyo hivyo sisi waswahili hatuwezi kuongea kiarabu

Waarabu walikuja wakakuta tayari watu wa pwani wana kiswahili chao ila wao walilazimisha baadhi ya maneno ya kiarabu yawe sehemu ya mawasiliano na kupitia kwa baadhi ya majinga ya wakati huo ambayo yalikuwa karibu na majamaa hayo yakaona ni ufahari sana wao kutamka maneno ya kiarabu ndivyo hivyo walivyochafua Lugha yetu hadi leo.

Hiyo ni historia basi kama kuna baadhi ya mameno ambayo yalifanikiwa kupenya na kuwa sehemu ya Lugha sii mbaya kwa sababu nyakati hizo zilikuwa nyakati za giza na lugha yetu ilikuwa bado inakuwa.

Kinachonikereketa roho sasa hivi ni nyakati za mwanga, watu wamesoma, kuna maneno mengi ya kibantu lakini kuna baadhi ya watu wanaona fahari sana kuchanganya maneno ya Lugha ya kiarabu na kiingereza kwenye lugha yetu kwa makusudi ili yaonekane ama yamesoma dini saana ama yamesoma elimu nyingine kuliko watu wengine.

Nimeshangaa majuzi kuna neno ambalo linatumika wakati wa kurusha matangazo ya moja kwa moja maarufu kama LIVE siju ni mtu gani kaenda kwenye kamusi ya kiarabu na kutuletea neno MUBASHARA. Kwanza neno lenyewe ni lirefu sana na limeshindwa kuendana na neno LIVE na je kwa sasa tunashindwa kupata neno mbadala wa LIVE mpaka tukakope UARABUNI? Yaani kwenye makabila yote ya Afrika tumekosa hadi tuvuke mabara kwa hao jamaa?
===
Steve Dii,
Wewe ungalijua kwamba Kiarabu ndiyo mama wa Lugha zote DUNIANI wala usingekuja na hiyo hoja.

Lugha ya kiswahili ni Mkusanyiko wa lugha kuu mbili Kibantu na kiarabu, kibantu ni 65- 70%, Kiarabu ni 20-25%, lugha zingine kama kiingereza, kireno, kihindi, kijerumani ni 3-5%-- kama 65-70% ni kibantu, je, haitoshi tu hadi tuendelee kuingiza maneno mengine ya kibantu (kihaya, kisukuma, kiha nk)??!!--- juu ya yote hiyo inawezekana kujenga ukabila na uhasama wa makabila kwani kila kabila labda linaweza kutaka maneno yake yaingizwe katika matumizi ya kiswahili (standardized into kiswahili).

Juu ya yote Hakuna hata lugha moja ya kibantu ni ya kimataifa kinyume na kiarabu ambayo ni miongoni mwa lugha kuu 5 za kimataifa hivyo kuingiza maneno ya kiarabu katika kiswahili ni njia moja ya kukifanya kiswahili kiwe chepesi kueleweka kimataifa na kufundishika na kupata kasi ya kimataifa kama kiarabu.

Kule comoro kuna lugha moja inazungumzwa na wenyeji wa huko karibu asilimia 40 ni maneno ya kiswahili,Wataalamu wa kiswahili wanasema hiyo lugha ni kipande/ mtoto wa kiswahili.
===
Kwa kweli kiasili Kiswahili ni lugha ya kichotara lakini hii si aibu. Lugha za kichotara zinastawi vizuri kwa sababu ni rahisi zaidi kupokea maneno mapya. Mfano mkuu ni Kiingereza ambacho ni mchanganyiko wa Kigermanik na Kifaransa cha kale; muundo wake unafanana na Kiswahili kwa sababu kuna msingi upande moja (Kiing.: Kigermanik; Kiswahili: Kibantu) na msingu huu ni sarufi pamoja na kiasi kikubwa cha msamiati halafu lugha ya pili iliyoingiza maneno mengi.

Kiingereza kiliweza kupokea kirahisi maneno mengi kutoka kote na kuimarika hivyo. Maneno ya Kisayansi ambayo tunajifunza kama "Kiingereza" si Kiingerza kiasili bado Kilatini au Kigiriki hasa ila tu Waingereza hawapigani nayo wanayapokea tu. Hapo ndipo pia nguvu moja ya Kiswahili ninavyoona na asili yake ya kichotara inasaidia sana. Kwa zaidi angalia hapa.
 
Steve,

Hii mada inaturudisha katika historia nzima ya Kiswahili. Kama unavyoweza kuwa unafahamu, Kiswahili ni "lingua franca" lugha iliyokuzwa na biashara katika Pwani ya Afrika Mashariki. Kutokana na hili, kiarabu kilikuwa na mizizi mirefu mapema sana katika Kiswahili. Kiswahili, tofauti na Kifaransa, hakina chombo kinachokipangia msamiati na matumizi fasihi, hata Baraza la Kiswahili halina kazi hii kwa mujibu wa nielewavyo. Katika hili Kiswahili kiko sawa na Kiingereza, lugha nyingine iliyokuzwa kwa kuchanganywa sana na lugha nyingine za Kihindi-Kiulaya (Indo-European languages) hususan Kijerumani (the Saxon in "Anglo-Saxon") na Kilatini.

Ukweli ni kwamba huwezi kuongelea Kiswahili kiujumla bila kuhusisha lahaja unayozungumzia. Kwa sababu za kihistoria na ki Jiografia, lahaja za pwani (Kiunguja, Kitumbatu,Kimrima, Kimakunduchi, Kimgao, Kipemba, Kimvita zimepatwa na mvuto wa kiarabu zaidi kutokana na kuwa pwani, lakini lahaja kama za Kingwana za huko DRC ziko kibantu zaidi. Na maneno mapya mengi ya Kiswahili yanakuwa na tashtiti za kibantu zaidi kama si Kiingereza.

Uzuri au ubaya wa Kiswahili ni kwamba lugha hii inakua kiasili, bila kuingiliwa. Nyerere katika jitihada zake zote za kukuza Kiswahili hakuwahi kukibadilisha na kukilazimisha kwa watu kama alivyofanya Mustapha Kemal Ataturk kwa Waturuki baada ya kuudondosha utawala wa Ottoman.

Kwa hiyo ukiangalia muelekeo, Kiswahili kilikuwa kinavutwa zaidi na kiarabu zamani kuliko hivi sasa, sasa hivi muelekeo unaenda kwenye Kiingereza (sijui kama kumbadilisha muarabu na muingereza ni kitu kizuri) na maneno yanayotamkika kibantu.

Kitu tunachoweza kujifunza kutoka katika Kiingereza ni kwamba hata lugha hii ya watawala wa dunia ilibidi kukubali mabadiliko makubwa sana kutoka Kiingereza cha zamani mpaka hiki cha sasa.Katika Kiingereza cha sasa ni vigumu kuandika sentensi ya maneno kumi bila kutumia neno lenye msingi wa kilatini.

Labda tabia moja isiyoepukika ya lugha zenye mafanikio ni kuweza kutohoa vizuri.
 
Kwanza kabisa napenda nianze kwa kukili kuwa Kiswahili bado ni lugha inayonipiga chenga pahala pengi. Hivyo kuna pahala pengi katika hoja yangu nitachanganya na lugha ya Kiingereza, pamoja na kwamba ningelipenda sana kuepuka.


...Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.

Ni ulimbukeni!

Limbukeni, limbukeni!

Eti unasema "Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day."

Mtanzania na utashi wako unadiriki kusema kiswahili kinakupiga chenga na utakaposhindwa utatumia kiingereza? Hicho kitu hapo juu ndo huwezi kukisema kiswahili? Acha kupotosha kwamba umejaribu kuepuka. Hujajaribu!

Tumenyanyaswa na mabeberu wa Magharibi, tukapelekwa Uarabuni wakatukata mapumbu tusizaliane, tukapelekwa Marekani kutumikishwa kwenye visiwa vilivyoibiwa kulimishwa miwa na tumbaku na kuchapwa mbakora kama punda, halafu leo unatamka hadharani kwamba lugha ya Mama yako huijui vizuri na ukishindwa utatumia ya watwana na mabwana wa magharibi!

Wewe ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni.

Huna soni!
 
Kuhani,

Sawa Kuhani. Mimi limbukeni nisiye soni. Naomba mchango wako kwenye hoja yangu. Shukrani.
 
Sawa Kuhani. Mimi limbukeni nisiye soni. Naomba mchango wako kwenye hoja yangu. Shukrani.

Tutaendeleaje kujadili mada wakati tabia inayopingwa ni ya kilimbukeni na anaepinga anajua, anakubali, kwamba yeye ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni?

Tutakuwa wanafiki kenyekenye.

Anza upya!
 
Lugha kubwa (zenye maneno mengi zaidi au zitumiwazo na watu wengi zaidi duniani) karibu zote, zina maneno ya kutokana na lugha zingine. Sijakutana na lugha ya kimataifa ambayo haina maneno ya lugha zingine.

Ki-swahili kina asili mia kubwa ya maneno yatokanayo na Kiarabu kwa sababu ya misafara mingi ya baharini kati ya nchi zinazo-ongea kiarabu na pwani ya Afrika Mashariki, toka enzi na enzi, hakuna ajuaye mwanzo wake.

Ki-swahili pia kina maneno yatokanayo na ki-hindi, ki-reno, ki-china na kadhalika. Na pia lugha zingine zote za kimataifa utakuta zipo hivyo hivyo.

Kiswahili kuwa na asilimia nyingi ya maneno ya kiarabu pia imechangiwa na kuwa, si zamani sana toka kiswahili kianze kuandikwa na herufi hizi za kilatini tuzitumiazo kwa sasa, kabla ya hapo kiswahili kilikuwa kikiandikwa kwa kutumia herufi za kiarabu. Na mpaka sasa wazee wengi wa pwani ya Afrika Mashariki hutuia herufi za kiarabu kuandika kiswahili.

Sidhani kama itatokea kuweza kukiondowa kiswahili kabisa kutoka kwenye uarabu, kwani hata neno lenyewe ki-''swahili'' ni la kiarabu likimaanishi kando kando ya bahari au pwani kwa kifupi.

Ki-swahili ni luugha yenye chipuko kutoka mwambao wa bahari ya hindi kuanzia Somalia mpaka Mozambique, kwa hiyo kiswahili ni lugha ya mwambao, na ni raha zaidi utaposikia watu wa mwambao wakiiongea kuliko wakiiongea watu wa bara.

Natamani nimsikie Msukuma (ambae hajaishi mwambao) akisoma mashairi ya ki-Swahili.
 
Tutaendeleaje kujadili mada wakati tabia inayopingwa ni ya kilimbukeni na anaepinga anajua, anakubali, kwamba yeye ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni?

Tutakuwa wanafiki kenyekenye.

Anza upya!

Sitoanza kwa matakwa yako. Naamini kuna WanaJF watakayoichukulia hoja yangu kimsingi na kuijibu kama hoja iliyokamilika.

SteveD.
 
Tutaendeleaje kujadili mada wakati tabia inayopingwa ni ya kilimbukeni na anaepinga anajua, anakubali, kwamba yeye ni mfano wa kitabuni wa saratani ya ulimbukeni?

Tutakuwa wanafiki kenyekenye.

Anza upya!


Labda ingekuwa vigumu zaidi kujadili mada kama mtoa mada asingekubali kwamba yeye ni limbukeni kuliko hivi sasa ambapo mtoa mada amekubali.

Katika kukubali kwake ulimbukeni, tumeona mizizi ya ulimbukeni ilivyokuwa mirefu, kiasi cha kwamba hata mtoa mada inayopinga ulimbukeni ametumbukia katika ulimbukeni ulio katika nusu-ufahamu wake.

Kanuni tunayojifunza hapa ni kuwa ulimbukeni unaenda mbali sana, na kama hata anayeleta mada ya kupinga ulimbukeni anaweza kutegeka na mtego wa ulimbukeni, mkosoaji mleta mada inayopinga ulimbukeni kwa msingi wa kwamba mleta mada inayopinga ulimbukeni ameileta mada iliyochanganya na ulimbukeni naye pia hayuko juu ya kuanguka katika mtego wa ulimbukeni.
 
Kuhani,
Unajuwaje kama kugha ya mama yake ni ki-Swahili? wacha lawama zisizo na msingi, kuna watanzania wengi hii leo hawajui ki-swahili na kuna wengine wanajuwa kidogo sana, tembea Tanzania hii ukaone.
 
Kanuni tunayojifunza hapa ni kuwa ulimbukeni unaenda mbali sana, na kama hata anayeleta mada ya kupinga ulimbukeni anaweza kutegeka na mtego wa ulimbukeni, mkosoaji mleta mada inayopinga ulimbukeni kwa msingi wa kwamba mleta mada inayopinga ulimbukeni ameileta mada iliyochanganya na ulimbukeni naye pia hayuko juu ya kuanguka katika mtego wa ulimbukeni.

Sawa, Kiranga, ni kwa vipi aliyemkosoa limbukeni mleta mada pia hayuko juu ya mtego wa ulimbukeni?
 
Sawa, Kiranga, ni kwa vipi aliyemkosoa limbukeni mleta mada pia hayuko juu ya mtego wa ulimbukeni?

Hakuna mwana-adamu aliye juu ya mtego wa ulimbukeni, maadam unaishi siku yoyote unaweza kuuonyesha ulimbukeni wako, kizuri ni kujifunza.

Ulimbukeni unakuja kwa sura nyingi, naamini sana katika kukosoana, lakini kuwa na asili ya ubishi uso kipimo, kutokuwa na tabia ya kuchukuliana, kushailoki, kuona maovu tu kunamuweka mkosoaji mtoa maada katika mtego mkubwa wa ulimbukeni kuliko ule wa mtoa maada.

Nuita huu ulimbukeni wa ujuaji, ambao kwao tunachofikiri tunakijua kinatupa ujivuni wakati kwa kweli kujua ni kitendawili cha kifalsafa.

Hakuna kujua :) Tunajifunza tu.

Heck, hakuna kujua hata kwamba hakuna kujua!
 
Kiranga,
Kuto kujuwa ki-Swahili nawe um-Tanzania si ulimbukeni, Kiswahili toka kiwe lugha ya Taifa la Tanzania si miaka mingi sana, nadhani hata hamsini haijafika. Nadhani ni baada ya mwaka 1961 ndio ki-Swahili kikaanza kuwa lugha ya Taifa. Kabla ya hapo, ki-Swahili kilikuwa kikiongewa sana kwenye ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki na katika miji mikubwa ya biashara kuingia bara.

Kwa miaka chini ya 50 kuwa kugha ya Taifa ni michache sana kwa nchi yenye lugha zaidi ya mia moja kukifanya kiwe lugha mama ya kila m-Tanzania.

Lugha mama ni ile unayoisikia toka unazaliwa, kuna makabila mengi Tanzania yanajivunia lugha zao za asili kiasi cha kwamba, kuna wa-Tanzania wengi mpaka leo hii, huanza kujifunza ki-swahili wanapoanza shule, hao huwezi kusema kuwa ki-swahili ni lugha yao mama. Kwa wao kutokujuwa ki-swahili fasaha si ulimbukeni, ulimbukeni ni kuanza kushambulia mtu bila kuwa na mantiki.
 
@SteveD,

STEVE D unaelewa nini hasa kuhusu lugha ya kiswahili na chimbuko lake pili unaelewa kuwa kiswahili hapa TANZANIA hakikuwa kinazungumzwa na watu hote tatu nenda katafute kumbukubu za mwali julis utakuka ni siku gani mwalimu alitangaza rasmi kutumika kiswahili kama ndio lugha ya taifa ?naimani itasaidia kuelewa chimbuko lake
 
Hakuna mwana-adamu aliye juu ya mtego wa ulimbukeni, maadam unaishi siku yoyote unaweza kuuonyesha ulimbukeni wako, kizuri ni kujifunza.

Ulimbukeni unakuja kwa sura nyingi, naamini sana katika kukosoana, lakini kuwa na asili ya ubishi uso kipimo, kutokuwa na tabia ya kuchukuliana, kushailoki, kuona maovu tu kunamuweka mkosoaji mtoa maada katika mtego mkubwa wa ulimbukeni kuliko ule wa mtoa maada.

Kiranga, nashukuru kwa hili. Kuhusiana na ndugu Kuhani kuna mengi yameandikwa jamvini hapa kuhusiana na misimamo yake.Pia kuna mengi ameandika ambayo yanaelezea misimamo yake. Nathubutu kusema kuwa, misimamo yake mingi ni yenye ku-challenge fikra na ukiipima ni yenye manufaa overall.

Hata hivyo pahala pengi provocative language anayotumia inafanyika makusudi, kwa malengo ya kukatisha tamaa au kukomoa kwa maneno ya kejeli na yaliyojaa dhihaka dhidi ya wale anaowalenga. Na mara nyingi anachagua target, again kwa makusudi kabisa. Tatizo ni pale unapojitokeza kuonesha mapungufu yake, ni vitisho na visa vinafuatia kwa almost kila utakachokiandika baada ya hapo. Nadhani ni sahihi kusema kuwa ni mtu ambaye anaamini kwenye 'infallibality' and may be thinks he's one.

Mkuu, mimi nachukulia kila post kama vile ni mtu mpya amejiunga na kutuma maoni yake. Hivyo, hata kama kwamba ni mmoja wa wanaJF ambao wamekumbana na visa vyake, kwangu mimi kila atakachoandika nitakisoma na kukichukulia kama post ya mwanachama mpya na inayohitaji kuwa judged by its own merit, jambo ambalo wengine laweza kuwaghafrisha.

Ahsante.

SteveD.
 
STEVE D unaelewa nini hasa kuhusu lugha ya kiswahili na chimbuko lake pili unaelewa kuwa kiswahili hapa TANZANIA hakikuwa kinazungumzwa na watu hote tatu nenda katafute kumbukubu za mwali julis utakuka ni siku gani mwalimu alitangaza rasmi kutumika kiswahili kama ndio lugha ya taifa ?naimani itasaidia kuelewa chimbuko lake

Sonara, challenge kubwa hii na nina ahidi kuijitahidi kuitekeleza. Ahsante.

SteveD.
 
@SteveD,
Umesoma Tanzania? Kama umesoma Tanzania elimu ya msingi na ya upili huwezi kuacha kujua maneno haya. Labda uwe unaidharau lugha ya Kiswahili kiasi kwamba hutaki kuwa makini nayo.
 
Sasa, hii (sijui niite dosari) favouritism ya Uarabu dhidi ya Ubantu inatokana na nini, is it the case for inferiority complex ya aina fulani hivi, elimu au nini haswa?! Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.

"Akhsanteni", "Shukrani", natanguliza "Fadhila" zangu, au basi niseme... "ndaga fijo", "mwabeja"?!

SteveD.

Kama ni hivyo, basi kuna favourism vilevile ya Ubantu dhidi ya sisi wengine ambao ni Non-Bantus. .. Na hii ni mabaya zaidi. Kiswahili hakina maneno yanayotoka ktk Non-Bantu languages kama Kimasai, Kimang'ati, Kijaluo, Kisandawi, n.k.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom