Kiswahili kimezidi mno kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Je, upendeleo wa Uarabu dhidi ya Ubantu?

avogadro

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
3,663
Points
2,000

avogadro

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2013
3,663 2,000
Historia imepinsishwa. Kamwe kiswahili si KIARABU hata siku moja ndio maana leo ukimchukua muarabu kutoka uarabuni hawezi kuongea kiswahili vivyo hivyo sisi waswahili hatuwezi kuongea kiarabu

Waarabu walikuja wakakuta tayari watu wa pwani wana kiswahili chao ila wao walilazimisha baadhi ya maneno ya kiarabu yawe sehemu ya mawasiliano na kupitia kwa baadhi ya majinga ya wakati huo ambayo yalikuwa karibu na majamaa hayo yakaona ni ufahari sana wao kutamka maneno ya kiarabu ndivyo hivyo walivyochafua Lugha yetu hadi leo.

Hiyo ni historia basi kama kuna baadhi ya mameno ambayo yalifanikiwa kupenya na kuwa sehemu ya Lugha sii mbaya kwa sababu nyakati hizo zilikuwa nyakati za giza na lugha yetu ilikuwa bado inakuwa.

Kinachonikereketa roho sasa hivi ni nyakati za mwanga, watu wamesoma, kuna maneno mengi ya kibantu lakini kuna baadhi ya watu wanaona fahari sana kuchanganya maneno ya Lugha ya kiarabu na kiingereza kwenye lugha yetu kwa makusudi ili yaonekane ama yamesoma dini saana ama yamesoma elimu nyingine kuliko watu wengine.

Nimeshangaa majuzi kuna neno ambalo linatumika wakati wa kurusha matangazo ya moja kwa moja maarufu kama LIVE siju ni mtu gani kaenda kwenye kamusi ya kiarabu na kutuletea neno MUBASHARA. Kwanza neno lenyewe ni lirefu sana na limeshindwa kuendana na neno LIVE na je kwa sasa tunashindwa kupata neno mbadala wa LIVE mpaka tukakope UARABUNI? Yaani kwenye makabila yote ya Afrika tumekosa hadi tuvuke mabara kwa hao jamaa?
 

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,241
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,241 2,000
Steve Dii,
Wewe ungalijua kwamba Kiarabu ndiyo mama wa Lugha zote DUNIANI wala usingekuja na hiyo hoja.

Lugha ya kiswahili ni Mkusanyiko wa lugha kuu mbili Kibantu na kiarabu, kibantu ni 65- 70%, Kiarabu ni 20-25%, lugha zingine kama kiingereza, kireno, kihindi, kijerumani ni 3-5%-- kama 65-70% ni kibantu, je, haitoshi tu hadi tuendelee kuingiza maneno mengine ya kibantu (kihaya, kisukuma, kiha nk)??!!--- juu ya yote hiyo inawezekana kujenga ukabila na uhasama wa makabila kwani kila kabila labda linaweza kutaka maneno yake yaingizwe katika matumizi ya kiswahili (standardized into kiswahili).

Juu ya yote Hakuna hata lugha moja ya kibantu ni ya kimataifa kinyume na kiarabu ambayo ni miongoni mwa lugha kuu 5 za kimataifa hivyo kuingiza maneno ya kiarabu katika kiswahili ni njia moja ya kukifanya kiswahili kiwe chepesi kueleweka kimataifa na kufundishika na kupata kasi ya kimataifa kama kiarabu.

Kule comoro kuna lugha moja inazungumzwa na wenyeji wa huko karibu asilimia 40 ni maneno ya kiswahili,Wataalamu wa kiswahili wanasema hiyo lugha ni kipande/ mtoto wa kiswahili.
 

black sniper

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Messages
14,489
Points
2,000

black sniper

JF-Expert Member
Joined Dec 10, 2013
14,489 2,000
Mokaze,

Mkuu umenikumbusha siku moja nilisafiri na watu ambao walikuwa wanaongea lugha ambayo nilijikuta natega masikio kama popo anaetafuta mdudu
Lugha ni kiswahili lakini sielewi maana ila nasikia kabisa kiswahili ila sielewi sentensi kamili
Nilishindwa kuvumilia nikawauliza mnatokea wapi wakaniambia Comoro
Nilishangaa sana


Sent from my iPhone using Tapatalk
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
68,421
Points
2,000

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
68,421 2,000
Niliwahi kuleta mada hapa JF kuhusu hilo, jisomee...

 

falamangaa

Member
Joined
Jan 21, 2013
Messages
58
Points
95

falamangaa

Member
Joined Jan 21, 2013
58 95
avogadro,
Asante sana. Kiswahili ni lugha kamili ya kiafrika. Lugha zote duniani hukopa maneno kutoka lugha zengine. Msingi wa kiswahili ni lugha za kibantu. Kuna wataalamu wa lugha na historia ambao wameshafanya epelezezi wa uhusiano wa Kiswahili na lugha za kiafrika za kibantu haswaa lugha za pwani ya Afrika mashariki. Lugha za Zanzibar, Pemba,pwani ya Tanzania, Lugha za pwani ya Kenya (Jamii zinazoishi karibu na mto sabaki) na visiwa vya bahari ya hindi karibu na pwani ya afrika mashariki.

Pia usisahau kuwa wanasayansi wamesha sema kuwa binadamu alianza maisha hapa Afrika. Kwahivyo kama sisi waafrika ndio binadamu wa kwanza basi sisi ndio wa kwanza kuwa na lugha.

Waafrika wameishi hapa Afrika miaka mingi sana. Kuna wataalamu wengi wameandika uongo tangu siku za ukoloni juu ya maisha ya waafrika kwasababu hawataki waafrika wajue ukweli wa maisha yao. Hata uwongo kama wa historia ya kule misri kwa mfano.

Mwafrika ameishi hapa duniani miaka mingi sana.
 

avogadro

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
3,663
Points
2,000

avogadro

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2013
3,663 2,000
falamangaa,
Ni kweli waafrika kila jamii Mungu aliwajalia Lugha Tena Lugha zilizokamilika ukichukulia Tanzania tuu mfano kuna Lugha nyingi sana za kikabila tofauti na nchi za Ulaya ama ASIA ambako Mungu aliwapa lugha chache pamoja na herufi na maandishi kitu ambacho nchi nyingi za kiafrika zina maneno tuu maandishi ya asili kama wachina, wahindi, wajapani, waarabu hatukujaliwa. Sasa hawa wanaojiita wataalamu wa kiswahili wanataka kukiarabisha moja kwa moja kuwa kiarabu si jambo bora kwa sasa
 

falamangaa

Member
Joined
Jan 21, 2013
Messages
58
Points
95

falamangaa

Member
Joined Jan 21, 2013
58 95
Ni kweli waafrika kila jamii Mungu aliwajalia Lugha Tena Lugha zilizokamilika ukichukulia Tanzania tuu mfano kuna Lugha nyingi sana za kikabila tofauti na nchi za Ulaya ama ASIA ambako Mungu aliwapa lugha chache pamoja na herufi na maandishi kitu ambacho nchi nyingi za kiafrika zina maneno tuu maandishi ya asili kama wachina, wahindi, wajapani, waarabu hatukujaliwa. Sasa hawa wanaojiita wataalamu wa kiswahili wanataka kukiarabisha moja kwa moja kuwa kiarabu si jambo bora kwa sasa
Maandishi yako, lakini machache. Pia wakoloni waliharibu historia yetu nyingi. Kama wanubi walikua maandishi ya meroitic ambayo mpaka sasa haijatafsirika. maandishi ya Geez kule Ethiopia. maandishi ya Nsibidi kule Nigeria. Hata maandishi ya Misri (Hieroglyphics)

Historia ya kiafrika bado haijakamilika. Ngoja uone vile vijana waafrika wa sasa wataanza kusema ukweli wa historia yao baada ya kupeleleza wenyewe, na kufichua uongo uliosemwa na wakoloni.

Pia nafikiri historia ya Nubia na Misri ni ya zamani zaidi kuliko tulivyo ambiwa. Pia historia ya sehemu zengine nyingi Afrika kwote.

Wewe fikiria mpaka sasa bado tunajadili vile piramidi zilivyojengwa. Bado hatuelewi kabisa. Hio inamaanisha waafrika wa zamani labda walikua na akili kubwa kutuliko. Hawakuwa wajinga.

Hata kule Papua New Guine waaafrika wa kule wana kabila 800 kwa Nchi moja. ( Lugha mianane)
 

falamangaa

Member
Joined
Jan 21, 2013
Messages
58
Points
95

falamangaa

Member
Joined Jan 21, 2013
58 95
Nani kasema wenyeji wa papua new guinea ni waafrika???
Waafrika walisambazika duniani kote kutoka Afrika miaka elfu nyingi iliyopita. Ni wazi( Inajulikana) kuwa hawaishi Afrika kwa sasa, lakini ni wa asili ya kiafrika ( Rangi ya ngozi, mila, mienendo) na kadhalika. Nilitumia nambari ya kabila zao kama mfano wa wingi wa lugha zinazoongelewa na watu weusi.
 

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,241
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,241 2,000
Waafrika walisambazika duniani kote kutoka Afrika miaka elfu nyingi iliyopita. Ni wazi( Inajulikana) kuwa hawaishi Afrika kwa sasa, lakini ni wa asili ya kiafrika ( Rangi ya ngozi, mila, mienendo) na kadhalika. Nilitumia nambari ya kabila zao kama mfano wa wingi wa lugha zinazoongelewa na watu weusi.


Siyo lazima kwamba Rangi ya ngozi nyeusi iwe ni kitambulisho cha mtu mwenye asili ya Afrika.

Unasemaje kuhusu Aborigines wenyeji wa asili ya Australia? ?, Genes zao ni za kipekee hazifanani na Genes za waafrika weusi japokuwa Wao ni weusi ni hivyohivyo kwa Wenyeji wa Papua new Guinea.
 

falamangaa

Member
Joined
Jan 21, 2013
Messages
58
Points
95

falamangaa

Member
Joined Jan 21, 2013
58 95
Siyo lazima kwamba Rangi ya ngozi nyeusi iwe ni kitambulisho cha mtu mwenye asili ya Afrika.

Unasemaje kuhusu Aborigines wenyeji wa asili ya Australia? ?, Genes zao ni za kipekee hazifanani na Genes za waafrika weusi japokuwa Wao ni weusi ni hivyohivyo kwa Wenyeji wa Papua new Guinea.
Wana sayansi wameshakubaliana kuwa binadamu alitoka Afrika kabla ya kusambazika duniani kote, kwahivyo pia aborigines walitoka Afrika miaka karibu 75,000 zamani. Boss haya ni mambo wanasayansi wengi wameshakubaliana. Ndipo kuna "Out of Africa Theory"
 

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,241
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,241 2,000
Wana sayansi wameshakubaliana kuwa binadamu alitoka Afrika kabla ya kusambazika duniani kote, kwahivyo pia aborigines walitoka Afrika miaka karibu 75,000 zamani. Boss haya ni mambo wanasayansi wengi wameshakubaliana. Ndipo kuna "Out of Africa Theory"

Mkuu hiyo ni theory, na theory inahitaji proof, ni hivi; kama hao jamaa wa Papua new Guinea na Aborigines wangekuwa wametoka Afrika basi Genes zetu zingefanana kwa kiasi fulani, kama utaniletea "%age Genetical match" hapo sitakuwa na hoja, mfano watu wa Afrika ya magharibi kama Nigeria, Ghana, Senegal, Sieraleone, genes zao ni tofauti na Watu wa Afrika mashariki ndiyo maana katika Genetic utasikia mtu mfano Mzungu wa ulaya anaweza kuwa na say 12% ya African Gene kutoka West Afrika Ghana au Nigeria au Utasikia mzungu mwingine ana % fulani kutoka East Africa, Ethiopia nk,

Mfano mwingine Afro Americans na Afro Jamaicans Haitians na watu weusi wa Brazili na Guyana, Cuba nk, wengi Wanazo genes za kiafrika kutoka west Africa, Ghana au Senegal au siera leone kwasababu mababu zao walichukuliwa utumwani kutoka maeneo ya hizo nchi, huwezi kukuta wanazo Gene za kutoka East Afrika au sehemu zingine za Afrika.

Sasa kwa upande wa watu wa papua new Guinea na Aborigines wa Australia niambie Genes zao zinafanana na watu gani wa Afrika, (Afrika magharibi, Afrika mashariki, Afrika ya kati, Afrika ya kusini nk).
 

falamangaa

Member
Joined
Jan 21, 2013
Messages
58
Points
95

falamangaa

Member
Joined Jan 21, 2013
58 95
Mokaze,
Boss nimekueleza wanasayansi wengi wameshajadiliana na kukuballiana kuwa binadamu alitoka Africa. Naweza kukuwekea hapa links mpaka uchoke. Tumia Google. Nime tafuta mara moja tuu. Link ndiyo hiyo. Unprecedented study of Aboriginal Australians points to one shared Out of Africa migration for modern humans

Wa aborigine walitoka Afrika.

Kuna utafiti na makaratasi mengi yameshaandikwa kuhusu swali hili. Unprecedented study of Aboriginal Australians points to one shared Out of Africa migration for modern humans

Familia ya lugha zao ndiyo si ya kibantu lakini wote wako na ukoo wa ki DNA na watu waliotoka bara la Afrika.
 

Mokaze

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2018
Messages
4,241
Points
2,000

Mokaze

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2018
4,241 2,000
falamangaa,

Siyo kweli mkuu kwamba watu wote wametoka Africa, yawezekana Maisha ya binadamu yameanzia Africa lakini sio kweli kwamba Watu wote duniani asili yao ni Africa. Siyo kweli kwa sababu huwezi kusema watu wa asili ya misitu ya Anazoni (in the interior dense forest of Amazon who have never seen the outside world) kwamba walitoka Africa.

Huwezi kusema watu wanaoishi juu kabisa ya milima ya Himalaya ambao maisha yao yote ni huko huko juu na wala hawajaona outside world uniambie eti hao walitokea Africa huwezi kunishawishi kwamba Wenyeji wa ndani kabisa wa Mongolia wanaoishi huku na tamaduni zao za asili bila kuchangamana na tamaduni zingine useme kwamba walitoka Africa.

Huwezi kunishawishi kwamba Sinhalese walioko katika visiwa vya india (Isolated islands in indian ocean), watu wenye lugha za kipekee na tamaduni za kipekee, watu ambao have never seen outside world uniambie kwamba karne kadha zilizopita walitoka Africa wakasafiri kwenda huko!!!, kwasababu ipi na kwa usafiri gani??.

Katika zama ambapo Mungu alianza uumbaji wa Wanyama na baadaye Watu -billion/millions of years ago- , uso wa dunia ulizungukwa na "Biotic soup" ni zama hizo za Biotic soup ndipo dunia ilipo chipusha viumbe hai (sprouting living organism), ni chemistry iliyokuwa Catalysed na direct sun light (cosmic rays), ndiyo maana ninakuambia siyo lazima kwamba Papua new guineans na Aborigines kwamba walitoka Africa.

Hao walichipuka hapo hapo jinsi sisi Waafrika tulivyochipuka hapa hapa Afrika, yaani Mazingira ya sisi waafrika kuchipuka hapa Afrika ni mazingira ya aina hiyo hiyo yaliyokuwepo sehemu mbalimbali za dunia na ndipo wakachipuka watu wa aina mbalimbali wenye rangi mbalimbali, lugha na tamaduni na mila mbalimbali, hii ilitokana na utofauti wa Biotic soup za mahali mbalimbali.

Chukua mfano huu, huwezi kusema kwamba Ng'ombe kutoka Afrika ndiye aliyeenda kuzaa ng'ombe wote wa duniani, kadhalika huwezi sema jambo hilo kwa kuku, Bata, Mbuzi nk kutoka Afrika ndio waliozaa mbuzi ,Bata, kuku nk wa dunia nzima, ni kwa mfano huo pia huwezi kusema kwsmba Aborigines wa Australia wenye historia ya maelfu ya Miaka huko kwamba walitoka Afrika, Aborigines feature zao ni tofauti sana na Black Africans, wao rangi ya ngozi yao, nywele zao, nyuso zao na stature zao hazifanani kabisa na Sisi black African, sasa huwezi kushikilia theory za wanasayansi kwamba hawa jamaa walitoka Afrika.

Kumbuka theory ni kitu cha kujadiliwa ili kupata ukweli, theory zinaweza kuwa Uongo.
 

Forum statistics

Threads 1,379,776
Members 525,565
Posts 33,756,209
Top