Kiswahili kimezidi mno kuelemea kwenye Kiarabu zaidi ya Kibantu. Je, upendeleo wa Uarabu dhidi ya Ubantu?

Kiranga,
Kuna maneno siku hizi wanaongeza kwenye Kiswahili, hasa yale yanayoibuka baada ya kuwepo kitu fulanileo ambacho huko nyuma hakikuwepo. Baadhi ya maneno haya ni kama: mtandao, luninga, mubashara, kumbukizi (japo hili si mojawapo ya yale niliyeleza hapa), kinakilishi (kompyuta), n.k. Wanaofanya jitihada hizi nzuri nadhani ni TATAKI (UDSM) au BAKITA au wote wawili kwa pamoja. Kwa hiyo kuna baadhi ya maneno machache siku hizi yanatungwa na professional Bodies na kuongezwa kwenye Kiswahili
 
Hakuna mwana-adamu aliye juu ya mtego wa ulimbukeni,

Heck, hakuna kujua hata kwamba hakuna kujua!
Hapana kwenye hiyo bolded hauko shaihi. Hapa hauko sahihi, mimi nakukatlia. Kwani ulimbukeni ni nini? Ulimbukeni ni tabia ya mtu kufanya jambo katika namna ambayo inamwonyesha kuwa yeye ni kama mtu wa kwanza kulifanya, wakati jambo hilo linaeleweka na kuzoeleka na watu wengi kiasi kwamba si geni kwao. Kwa hiyo huyu limbukeni yeye huwa anakuwa haelewi hilo, ila yeye anaona kama anafanya jambo jipya na ambalo wengi hawalijui au hawajawahi kulifanya.

Kwa mantiki hii basi, watu ambao ni malimbukeni, ni wachache sana na si kweli kwamba wengi wanaweza kuangukia kwenye mtego huo. Ni sawa kuwa wapo ila siyo wengi
 
zomba,
Toeni kwanza definition ya ulimbukeni halafu ndiyo muanze kujadili. Mnajadili ulimbukeni katika mazingira ambayo ni heregeneous, kila mmoja ana definfinition yake kichwani kwake tofauti na ya mwenzake, kitu ambacho hamuwezi kufikia muafaka. Define ulimbukeni kwanza. Mimi nimeshatoa definition hapo juu na kama haiko shaihi nakaribisha hoja. Kiswahili nilisoma mpaka F4
 
Ajuaye mengi, hasemi mengi
Who knows more speaks less
Empty vessels make the loudest noise
"A silent fool is considered wise".
Niliwahi kucheka sana siku moja wakati tuko chuo. Jamaa wawili walikuwa ni watani, siku moja mmoja akamwibukia mwenzake kuwa huwa anaongea pointless. Akamwambia unajua wewe fulani, muonekano wako ulivyo kwa nje unaonekana mtu wa heshima sana, isipokuwa kasoro moja kubwa kabisa uliyonayo huwa unaongea pumba full time.

Sasa mimi nakushauri unapokuwa uko kwenye hadhira ya watu, uwe unajitahidi unakaa kimya tu usiongee kitu. Hii litakufanya uwe unapata credit kwa sababu watu wakishaondoka kwenye hadhira hiyo, kwa namna walivyokuoona na ukimya wako wa kutokuongea, njiani wankwenda wanaelezana wakisema KWA MFANO KAMA LILE JAMAA KAMA LINGEONGEA (yaani wakimaanisha sasa yule aliyekuwa anakatazwa asiwe anaongea). Yaani nilicheka siku hiyo. watani watu wa ajabu sana
 
Hapana kwenye hiyo bolded hauko shaihi. Hapa hauko sahihi, mimi nakukatlia. Kwani ulimbukeni ni nini? Ulimbukeni ni tabia ya mtu kufanya jambo katika namna ambayo inamwonyesha kuwa yeye ni kama mtu wa kwanza kulifanya, wakati jambo hilo linaeleweka na kuzoeleka na watu wengi kiasi kwamba si geni kwao. Kwa hiyo huyu limbukeni yeye huwa anakuwa haelewi hilo, ila yeye anaona kama anafanya jambo jipya na ambalo wengi hawalijui au hawajawahi kulifanya.

Kwa mantiki hii basi, watu ambao ni malimbukeni, ni wachache sana na si kweli kwamba wengi wanaweza kuangukia kwenye mtego huo. Ni sawa kuwa wapo ila siyo wengi
Kama kuna vitu tunavifanya kwa mara ya kwanza kwenye maisha, hapo ndo kuna kulimbuka.

Ukipiga picha ya nyumba yako mpya na kuiweka Facebook unalimbuka.

Ukipiga picha ya gari lako jipya na kuiweka Instagram unalimbuka.

Ukiweka picha ya mtoto wako mpya unalimbuka.

Maadam kuna vitu vipya tunakutana navyo, tutalimbuka tu.

Na ukikataa hilo, hapo napo unalimbuka kwa kukataa kuwa unalimbuka.

Kulimbuka si lazima kuwe kitu kibaya, inawezekana kabisa kukawa ni sehemu ya kawaida tu ya maisha.

Ukilazimisha kuwe kitu kibaya, hyjaelewa kulimbuka ni nini na hapo unalimbuka kuhusu kulimbuka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa, hii (sijui niite dosari) favouritism ya Uarabu dhidi ya Ubantu inatokana na nini, is it the case for inferiority complex ya aina fulani hivi, elimu au nini haswa?! Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.
Waaarabu ndiyo wameiga kiswahili! na kukopa maneno! tangu zamani kiswahili kimebadilika jina tu lkn kwa asili ni ki-Summeria kilicho ongewa kama Lugha rasmi Mesopotamia ya kale,

Arabs hawana Official recognised National ethnic identity kamili kwa sababu siyo Race, kama zilivo Race za Ma bara mengine Duniani, bali ni Political Race.

Mchanganyiko, wa Wa-giriki na wabantu! walikiendeleza ki-summeria wakachanganya na maneno machache ya kwao! wakidai wao ni Mabwana, waungwana, hawawezi kuongea Lugha sawa na ya kitwana (weusi!) Baba zao ni wazungu!

Kosa wabantu Mkilichukulia hili jambo la mfanano wa Lugha kama inferiority complexes ndiyo mnapotea mazima kihistoria, mnatakiwa kufanya uchunguzi wa kina, ili...

tujue nani mkopaji na nani mkopwaji, hii itasaidia pia kujua tumetokea wapi, na tulidanganywa wapi! sababu haijawahi tokea eti lugha ya miungu waungwana/ Watawala ifanane na ya Nyani wa Porini, nani ka kwambia?


Lugha kama Kiaramaic, kifoeniki, Ki- Coptic, ndo Lugha Mama kule Mesopotamia ya kale! Babylonians, Cush land,(Ethiopia ya leo!) kwa nini Lugha hizi zilipotea hapo Middle East yote mpaka na Egypty ya leo? jibu ni rahisi tu
sababu ilikuwa Lugha ya watumwa weusi. leo vitabu vingi tunadanganywa tumekopa maneno, na ukisoma vitabu tofauti tofauti zaidi ya kumi, utaona ukweli wao ndo wametukopa! Lugha zetu kiswahili, ya kibantu, ni km nilivosema hapo juu!

Hata hao wanahistoria mpaka leo wanajifanya hawajui kibantu kiliingiaje kwenye kiarabu, wanakuja na jibu jepesi sana eti Mwingiliano wa kibiashara! huko Mara,Serengeti, thika hawakufika lkn ni wabantu!

Sehemu pekee wanayoongea Lugha ya kale Africa ni Ethiopia, wote twajua Ethiopia kamwe haikuwahi kutawaliwa na mkoloni, yaani Lugha ya Ki-Aramaic(kiamhara) ilibaki dumu dumuni, wakati wa mkoloni/British, tuliwahi kutumia hii lugha kwenye noti zetu!

Kumbuka Mitume wote akiwemo Yesu mwenyewe waliongea Lugha 2 sana, yaani Ki-Aramaic na Kigriki, angalia sasa kigiriki kipo mpaka leo! Girikiz walikiendeleza,

Ki-Aramaic kilipotezwa mpaka leo, sababu ya machafuko ya vita, na watumwa kulazimishwa kuongea Kiarabu, na kubadili majina yao ya asili. mpaka leo tunabadilishwa majina kwa hiari, km Maxmillian Melo, John, eti Musarya Mwuudavwadi ni jina la kishenzi kweli?

Kiswahili {Kibantu haswa} hakijakopa maneno kutoka kiarabu big NO. sababu ni Afro- asiatic Language, tangu zama kabla ya Waarabu kuvamia Mesopotamia ya kale haikwepeki.

Hata neno Arabs walilikopa kwa wenyeji walio ishi hapo tangu zama za kale! wao wakajiita Waarabu, Sababu Ulaya hawakukubalika tena, wakajiundia kaumoja kao! yaani umoja wa nchi za kiarabu. na Wasummerians- weusi wapo mpaka leo huko Middle east but wamemezwa. na kupachikwa majina eti masalia ya watumwa!
 
Mokaze,
Boss sasa umeruka kutoka wa aborigine ukaenda Americas haya. Tafuta "Olmecs" Watu asili wakiafrika wanapatikana kote duniani. Huko uropa tafuta "Etruscans" ( Watu weusi kama wewe na mimi) Hata Asia kuna watu weusi kule philippines, kule Indonesia, Malaysia, Kule India, Uarabuni. Hata bara uropa kulikuwa na watu weusi. Wengi wao waliuliwa ama kuchanganyika na wazungu.

Hata "Neanderthals" Jiulize swali Neandearthals walitoka wapi?. Ukitafuta kwenye google utapata kuwa watafiti wengi wamekubaliana kuwa walitoka Afrika.

"Homo Sapiens" pia walitoka Afrika halafu wakasambazika duniani kwote. Usisahau pia kuna wakati wa "Ice Age" Sehemu nyingi duniani zilikuwa na barafu/ zilikuwa hazikaliki. Muafrika alianza kutembea kwa miguu na pia boti za zamani akaanza kusambazika duniani. Hao binadamu wengine wamebadilika kimwili, na ki DNA, kwa sababu ya vitu kama hali ya anga, baridi, kutokuwa na jua ya kutosha, chakula, na kadhalika. Pia wazungu wako na melanin chache. Nchi zao zina jua chache. Rangi ya Ngozi inabadilika kwa sababu ya upungufu wa jua. Haya yote yanafanyika kwa muda murefu, na sio miaka kadhaa.

Tofauti ya Homo Sapiens na Neanderthal ni binadamu mmoja ameendelea kiakili/kimageuzi(Evolution), na mwengine bado yuko nyuma yaani "Primitive", mmoja ana umewo kiakili kuliko mwengine. lakini wote walitoka Afrika.

Hata utafiti wa DNA wanasayansi wengi wanakubaliana kuwa muafrika ndiye original binadamu.

Binadamu wote walitoka Afrika. Kama hukubaliani na haya weka hapa research/utafiti wenye unaonyesha Waafrika walitoka kwengine kama vile uarabuni kwa mfano.

Hata tuwache sayansi. Muafrika anaweza zaa binadamu mweusi, mweupe, wa rangi ya kahawa na kadhalika. Muafrika anaweza zaa binadamu mwenye nywele ya aina ya blonde, mwenye macho ya buluu, ya kahawa, mwenye nywele ngumu, ama nywele ya kisomali, kihindi, waafrika wako wenye macho ya kiAsia, wafupi, warefu.

Haya weka hapa utaftiti wako wenye unaonyesha wazungu wanaoweza hayo yote nimeandika hapo juu?

Wacha nikupe source mzuri ya kujifunza historia yako kama mwafrika.


Pia soma akina DR John Henrik Clarke

Cheikh Anta Diop

Yosef Ben-Jochannan

Ivan van sertima

Theophile Obenga

Hawa wataalamu wana patikana pia kwa youtube.
Jifunze historia yako kama mwafrika.


Kiswahili ni lugha ya kibantu. Si lugha ya Kiarabu. Kimekopa tuu maneno ya kiarabu kama vile imekopa ya kireno, kizungu, kihindi, na kijerumani. Lugha zote duniani zinakopa maneno kutoka lugha zengine.
 
Nyaru-sare,
Safi sana.Watu kweli wanafaa wafanye utafiti zaidi juu ya hizi lugha zetu. Tumepumbazwa ili tujione kwa lugha zetu ni duni (inferior)

Pia naweza ongeza kuwa dhana/wazo la ( Race) sio msingi wa sayansi. Hii ni dhana wazungu wametumia kuwagawanya watu haswaa kwa rangi. Hakuna sayansi kamwe kwenye hiyo dhana.
 
Kiranga,
Nimesema hivi: ulimbukeni nii kufanya jambo UKIWA UNAONYESHA KAMA KWAMBA wewe ni wa kwanza kulifanya. Sijasema kuwa ulimbukeni ni kufanya jambo kwa mara ya kwanza. Please get me correctly!
 
Kwani ulimbukeni ni nini? Ulimbukeni ni tabia ya mtu kufanya jambo katika namna ambayo inamwonyesha kuwa yeye ni kama mtu wa kwanza kulifanya, wakati jambo hilo linaeleweka na kuzoeleka na watu wengi kiasi kwamba si geni kwao. Kwa hiyo huyu limbukeni yeye huwa anakuwa haelewi hilo, ila yeye anaona kama anafanya jambo jipya na
Wote mmekosea Kufanya kitu kwa Shauku siyo ulimbukeni, umejuaje kuwa yeye anajua kuwa, yeye ndiyo wa kwanza kulifanya hilo jambo jipya?

Hata km jambo limezoeleka naweza kulibadili likawa zuri zaidi, mfano huyu kagundua Hadubini ya jua, Mimi nakuja na Hadubini ya Umeme wa jua! si ni jambo lile lile? . au limbukeni?

Kuwa na furaha wa sababu ya kushinda changamoto si ulimbukeni! Limbukeni ni yule anayewaza kwa mtizamo wa ku-limbuka! lkn muhusika dhaniwa hayajui hayo!

Sawa sawa na kumuhukumu mtu kifo kwa sababu una Madaraka, ila umaeamua tu afe! au afungwe maisha na ikawa hivo! mfano;

mwana JF mmoja anaweza kuona maandishi yako haya akakufikiria wewe ni limbukeni unajidai kunako key board yako wkt hajawahi hata kukuona!

Jambo ulilo fanya kiulaini, ukafanikiwa ni kawaida kwako! lkn unae mwita limbukeni kalishinda kwa changamoto nyingi za kutisha, anajua kuwa '' hakuna jipya chini ya jua'' ila wewe utadhani hajui pia ni ulimbukeni!

mfano km Lisu akishinda U- Rais leo, akafurahia, akabadili katiba,nk, kwa mtizamo wa Jiwe/lumumba watamuona ni limbukeni sababu yeye huyu jiwe amezoea kuiba kura kiubwete!, na kutetea maslahi binafsi

Kum-judge mtu/watu eti ni malimbukeni, ndiyo uliimbukeni haswa, ni mawazo potofu, sawa na uchawi, ambao unaloga tu bila sababu! huu usemi niwa watu wa daraja la chini kabisa waliokosa mwelekeo! kisiasa kiuchumi, na kiutamaduni! incompetent one!
 
Waaarabu ndiyo wameiga kiswahili! na kukopa maneno! tangu zamani kiswahili kimebadilika jina tu lkn kwa asili ni ki-Summeria kilicho ongewa kama Lugha rasmi Mesopotamia ya kale,
Unaweza kunitajia maneno ambayo Waarabu wameiga toka kwenye Kiswahili na ilikuwa lini ?

Je hi tamko "Swahili" kiasili ni la Waswahili au ?

Summeria sarufi yake ikoje ? Maana kwenye Kiswahili hakuna mfatano wa heruki mbili zenye sukuun (Zisizo tamkika, kama "mm....)
 
UKIWA UNAONYESHA KAMA KWAMBA wewe ni wa kwanza kulifanya. Sijasema kuwa ulimbukeni ni kufanya jambo kwa mara ya kwanza. Please get me correctly!
Nikivaa sweta au koti langu katikati ya jiji, nakatiza mitaa, bila shaka Narrow minded wataniona ni limbukeni naonyesha uzuri wa sweta langu la South, eti anatulingishia kaishi bondeni, kumbe nina Malaria, na baridi ni dalili kubwa ya Malaria,

Sasa kwa nini niko City centre?
Naenda Burhani Hosp. kumuona Dakta kwisha!
 
Unaweza kunitajia maneno ambayo Waarabu wameiga toka kwenye Kiswahili na ilikuwa lini ?

Je hi tamko "Swahili" kiasili ni la Waswahili au ?

Summeria sarufi yake ikoje ? Maana kwenye Kiswahili hakuna mfatano wa heruki mbili zenye sukuun (Zisizo tamkika, kama "mm....)
Haya ni mambo ya 400 BC, Nomino, Mofimu, muundo wa sentesi na maana, vitenzi nk vina shabihiana na kibantu. muda hautoshi nakupa kwa kifupi

jina la mfalme huyu, ''Ubara Tutu''

Dingi kiswahili.......... Dingir - Sumerian

Enki-mungu maji......Ea

enkibara ...kihaya!

Kanjir-sumerian, ... M-Kanja- buro kihaya

Urusese- mbwa kwa kikurya, ...Ur-Mbwa -summerian

Kwen-----Mamba.............kwenna--kisotho

Tulisan---sum.., na........ tulisa ngwana kindebele/ south

soma vizuri neno ''Arab''
Kamusi ya SUMMERIAN inapatikana google!
 
Kwanza kabisa napenda nianze kwa kukiri kuwa Kiswahili bado ni lugha inayonipiga chenga pahala pengi. Hivyo kuna pahala pengi katika hoja yangu nitachanganya na lugha ya Kiingereza, pamoja na kwamba ningelipenda sana kuepuka. Lakini hilo lingewezekana tu kama ningelikuwa na muda na uwezo wa kupangilia na kukumbuka maneno fasaha ya kutumia.

Pia nakili kuwa hii hoja sijaifanyia utafiti madhubuti kuhakikisha kuwa ina vielelezo vya kutosha ili kuchanganua na kufafanua mifano mbalimbali ambayo inaweza kutumika kuikoleza na kuipa msingi zaidi hoja yenyewe. Ni imani yangu kuwa wale walio bobea kwenye maswala ya lugha wanaweza kuiendeleza zaidi. Shukrani.
------------------ ***** --------------

Nitaanza;

Nikisema 'ngoko' au 'nkoko' Wasukuma, Wahaya na ninaamini makabila mengine mengi ya Tanzania wataelewa kuwa ninalotaka kulitaja ni jina la ndege tumjuaye kama 'kuku' kwa Kiswahili. Si makabila ya Tanzania tu, bali Wabemba wa Zambia, Washona wa Zimbabwe, Baganda wa Uganda nao wangelielewa.

Nikisema 'nzoka' au 'nyoka' vivyo hivyo makabila mengi yenye asili ya Kibantu yatanielewa.

Sawa, lugha nyingi zinakua na kuendelea kwa kuazima maneno kutoka kwenye lugha nyingine. Na maneno mengine yanajitokeza na kukua na kukubalika kama moja ya maneno ya lugha fulani kutokana na mazingira yanayozungukuka jamii.

Maneno kama 'swahiba', 'mstakabali', na mengine mengi yenye kusikika na kutamkwa kwa lafudhi ya pwani asili yake kubwa ni kutoka Kiarabu. Na ukweli wa mambo ni kwamba chimbuko la lugha ya Kiswahili ni lugha ya Kiarabu.

Hoja yangu: Je, chimbuko la lugha yetu ambayo tumerithi, tumejifunza, tumeikuza na kuienzi ndiyo kipimo pekee cha uhalisia wa maneno tuyatumiayo katika Kiswahili chetu?

Kimfano, nasema hivi kwani leo hii nikija na neno fulani hivi kutoka katika lugha ya Kihaya na neno hilo hilo kuwa tafsiri ya kitu ambacho kinapatikana Uhayani lakini hakipatikani katika Pwani, lakini hapo hapo kitu hicho kikabahatika kuwa na tafsiri yake katika lugha ya Kiarabu; uwezekano wa neno la Kiswahili kutumia (au hata kunyambulisha tu hilo neno la Kihaya ili iwe tafsiri yake katika Kiswahili) neno la Kihaya ni mdogo kuliko ambavyo urithi au ukubalianaji wa tafsri ya neno hilo ungelikuwa ule wa kutoka kwenye neno la Kiarabu.

Sasa, hii (sijui niite dosari) favouritism ya Uarabu dhidi ya Ubantu inatokana na nini, is it the case for inferiority complex ya aina fulani hivi, elimu au nini haswa?! Kwanini tunaenzi sana maneno kutoka Kiarabu kuliko maneno ambayo yana maana ileile kutoka lugha zetu za Kibantu. Seriously, I think there is an over-arabization of Kiswahili from its conception to this day.

"Akhsanteni", "Shukrani", natanguliza "Fadhila" zangu, au basi niseme... "ndaga fijo", "mwabeja"?!

SteveD.

MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU:

===

===


Ahsante mkuu kwa kuonesha kujali hii lugha ila FADHILA nalo pia ni neno ya kiarabu, hebu fikiria leo tutoe 40% au zaidi ya maneno kwenye hii lugha, tutabakiwa na lugha pungufu mno, tujaalie kingereza kitoe maneno ya kifaransa / kilatini basi watakuwa na upungufu mkubwa mno.
Jibu ni kuwa haikhalisi au haiyumkini kuyatoa kwa kuwa ni mengi mno mkuu, mfano hesabu 10 mpaka 100, 9 kati ya kumi ni ya kiarabu, sasa tutumie lugha gani ili kuziba pengo ? Ukisema kingereza ndo Yale yale ya kuruka mkojo.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom