KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Pili atoa ushahidi wake

Wamekimbilia moja moja, kungangania waoneshwe mtoa thread na mchangiaji/wachangiaji, ili wawakamate na kuwapoteza...

Bila kuanzia mamlaka husiku na kuthibitisha kama hizo tuhuma ni za kweli au uzushi...
 
Hahaaa nimecheka sana, mi nahis hata IQ test ziwe zinapimwa mahakaman, hamna kaz ngumu kama kupangua maswali yanayokuja kama mvua, unaweza umwambie wakili hayo maswali yote yanayokuja majibu yake sijui, ukileta utani unaweza ulizwa umekuja kufanyaje hapa mahakamani useme sijui.


Yaani mkuu watu wenye IQ kubwa wanajidhihirisha hapo aisee!
 
mmmnhhhhhhhhh iambieni hio jamuhuri iache kupoteza muda,JF ni kama kioo kwao juu ya utendaje wao,na baadhi ya mashirika yake kama Tanesco wanatumia hii platform.....sielewi wanacho kitafuta ni nini?
 
Polisi weupe sana, kwahiyo sampuli ya hawa ndiyo walitegemea wakifika Canada ile ndege itarudi?

Hii ndio inayochangia wakikamata mtu bila kufuata utaratibu huishia kumpiga na watawala wanafurahi maana wanajua wajinga ndio wanawasaidia kukaa madarakani. Huoni hata watawala huwa hawataki sana mambo ya mahakamani maana wanajua wataumbuka kwa kutofuata kwao sheria.
 
Ina maana Polisi hawakutaka kuchunguza siri ya mkwepa kodi??
Mbona hawakushirikisha TRA??
Kuna haja ya kuanzisha FBI Tanzania!!
Mkwepa kodi hakuguswa lakini mpuliza filimbi (mtoa taarifa) anatafutwa kushitakiwa!
Kwa mfano yule aliyetoa taarifa ya nyufa kwenye maghorofa ya hostel kama asingejitambulisha jina naye angesakwa lakini mjenzi haguswi!
Hii nchi inataka watu waishi Kwa hofu, waovu wasisemwe!
 
Hizi kesi zitaishia kuidhalilisha tu polisi na serikali Kwa ujumla! Whistle blower huwa hana hatia!
Afadhali uamuzi umalizike Mahakani kuliko kutokea uamuzi wengine wa ajabu ajabu wa kutishiana maisha bora imalizike kesi iishe kwa usalama muamuzi wa mwisho ni Hakim au Jaji kuhusika bora iwe salama.
 
Hivi ukituhumiwa unaenda polisi kuwaambia wamshitaki mtuhumu wako au wewe ndio unamshitaki ili upate haki yako? Sielewi hii kesi, maana ni polisi vs JF wakati polisi hawakutuhumiwa. Wanasheria nisaidieni.
 
HUYO SHAHDI NAYE KILAZA, KAULIZWA UNAIJUA KESI ILIYOKUWEPO MAHAKAMANI, ANAJIBU HAJUI, SASA MAHAKAMANI KAENDA KUFANYA NINI? JPM FUKUZA HAWA WATU RUDISHA WENYE VYETI FEKI, HALAFU HUYO SHAHD HUENDA KAFOJI CHETI, HAIWEZEKAN AWE MWEUPE HV KAMA THELUJI.
 
Back
Top Bottom