KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Pili atoa ushahidi wake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,877
Kesi namba 457 inayoikabili JamiiForums, kuhusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi, imeanza kusikilizwa leo.

Kesi hii ipo chini ya Hakimu Godfrey Mwambapa. Wakili wa Jamhuri alikuwa Kishenyi na mawakili wa Utetezi walikuwa Mtobesya na Jebra.

Shahidi wa kwanza alishahojiwa hapa: ‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao‬

Katika kesi hii, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada na mchangiaji mmoja ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu, JamiiForums inadaiwa kuwa ilikataa kutoa taarifa binafsi za mwanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

Fuatilia mlolongo wa shauri hilo ulivyokuwa leo katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu iliyopo Jijini Dar es Salaam.
-----------

Shahidi anajitambulisha..

Naitwa ASP Fadhili Bakari. Ni Afisa Polisi, Kanda maalum Dar es Salaam tangu Machi 2016.

MAJUKUMU: Ni mkuu wa kitengo Cha uhalifu wa kifedha Kanda maalum ya DSM, pia kitengo cha uhalifu wa makosa ya kimtandao kipo chini yangu.

Mnamo tarehe 10/05/2016 nikiwa ofisini alikuja mpelelezi wa Kesi, Assistant Monica na jalada la uchunguzi linalohusiana na tuhuma zilizoletwa ofisini na mkurugenzi wa wakala wa forodha CUSNA Investment na Ocean Link kwamba kuna taarifa zimesambazwa kwenye mtandao wa JamiiForums kwamba kampuni tajwa inajihusisha na wizi, ukwepaji Kodi na kughushi vitendo ambavyo vimeisababishia Serikali hasara.

Tuhuma zilizoletwa na watu wawili ambao ni Amrish Puri na Kwayu. Taarifa zilizodaiwa kusambazwa mnamo 08 Dec 2015.

Inspekta Monica alikuja kwangu ili niweze kuwasiliana na Mkurugenzi wa JamiiForums ili tupate details za wateja zitakazosaidia kwenye Kesi/uchunguzi.

Niliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu wa JamiiForums ikimtaka anipe Ushirikiano wa kunipa information(Namba za simu na taarifa za usajili za watu hao). Baada ya kuandika barua na kuisani nilimpatia mhusika kufikisha kwa anaehusika, Inspekta Peter Kayumbi aliniambia siku ya pili kuwa barua imepokelewa na kusainiwa na aliyeipokea.

Sikuweza kupata information nilizokuwa nazitaka ambazo zingenisaidia kwenye kesi (Shahidi anaonyeshwa kielelezo na anasema anaitambua kuwa ndio yenyewe na kuiomba mahakama iipokee kama kielelezo). Wakili wa utetezi (Jebra Kambole) anakubali ipokelewe na hakimu anaikubali.

Shahidi anaisoma barua ambayo alimuandikia mkurugenzi mkuu wa JamiiForums kuhusu taarifa inayoihusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link ya kuomba taarifa za usajili na namba za simu walizotumia kipindi wanajisajili kwenye mtandao wa JamiiForums.

Barua ilipokelewa na Chrispine Muganyizi siku moja baadae, Shahidi anaulizwa kuhusu taarifa zilizopo kwenye barua na kusema kulikuwa na makosa ya kiuandishi kwenye mwaka. Shahidi anaendelea kusema hakupatiwa taarifa zozote kama alivyoomba.

Wakili wa Serikali ameishia hapo na anafuata wakili wa utetezi, Wakili Jebra Kambole.

Wakili: Umesema unamsaidia mkurugenzi wa upelelezi?
Shahidi: Sahihi

Wakili: Kwa uelewa wako wewe humfahamu mmiliki wa JamiiForums?
Shahidi: Simfahamu

Wakili: Unafanya kazi JamiiForums?
Shahidi: Hapana

Wakili: Una uhakika gani taarifa ulizoomba walikuwa nazo?
Shahidi: Nina uhakika walikuwa nazo.

Wakili : Una ushahidi?
Shahidi: Sina ushahidi mwingine

Wakili: Kwa kuwa hauna ushahidi, inawezekana huyo mtu taarifa ulizoomba alikuwa nazo au hakuwa nazo!?
Shahidi: Haiwezekani

Wakili: Kwa kuwa barua iliandikwa Mkurugenzi mtendaji, akiwemo mtu mwingine atakuwa ameonewa?
Shahidi: Siwezi kujua maana mimi sikuhusuka kwenye ukamataji

Wakili: Kifungu Cha kumi hakikupi mamlaka ya kudai taarifa. Mtoa taarifa alitenda kosa gani?
Shahidi: Hili ni jalada la uchunguzi

Wakili: Hamkuona haja kuitaarifu TRA kuhusu mtu anayekwepa Kodi?
Shahidi: Haihusiani na hii kesi. Binafsi sikuwapa.

Wakili: Unajua mtu asikupokupa taarifa unaenda mahakamani kuomba amri?
Shahidi: Sijui.
---------

Wakili Mtobesya: Naomba nipatiwe exhibit P1. Nawasilisha ombi hili kwa mujibu wa kosa la jinai na makosa ya mtandao.

Maswali kwa Shahidi..

Mtobesya: Unaelewa kama washtakiwa wanashtakiwa kwa kosa gani hapa mahakamani?
Shahidi: Sijui

Mtobesya: Nitakuwa sahihi kama nitasema Polisi hamjui mlitakiwa kufanya nini wakati mnatafuta taarifa?
Shahidi: Mimi nilitaka nipate details

Mtobesya: Kwa hiyo taarifa ulizokuwa unazitaka zilikuwa kwenye mtandao?
Shahidi: Ndiyo

Mtobesya: Naomba niishie hapo

Wakili wa Jamhuri: Uliwahi kupata majibu kutoka uongozi wa JamiiForums?
Shahidi: Sikuwahi kupata

Kesi itaendelea kesho..
 
Hahaaa nimecheka sana, mi nahis hata IQ test ziwe zinapimwa mahakaman, hamna kaz ngumu kama kupangua maswali yanayokuja kama mvua, unaweza umwambie wakili hayo maswali yote yanayokuja majibu yake sijui, ukileta utani unaweza ulizwa umekuja kufanyaje hapa mahakamani useme sijui.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom