1. Baba ipo hivi
mawasiliano ya dishi yanategemea satellite iliyopo huko juu angani kwenye space. na hizo satellite zinamilikiwa na makampuni. ili uweze kutumia inabidi ukodi upewe nafasi ndio utumie. kutokana na u ghali wa huduma hiyo, hupelekea hata vifurushi vya Ving'amuzi vya Dishi viwe vikubwa ili kupata fedha ya kulipa pango
utakua shahidi kwa startimes, bei ya vifurushi vya dish na antenna vina utofauti , vya dishi ghali
kwa hiyo azam wamesimika mitambo mipya ( New project) ya ardhini( Minara) ili kupunguza ghalama kwa mtumiaji wa mwisho
2. Mawasiliano ya Dish/ Satellite yana changamoto ya hali hewa. utakua shahidi, ikinyesha mvua kidogo au wingu kubwa matangazo ya azam huwa yanakwama kwama hata ya DSTV
Sasa kwa mitambo ya ardhini na ving'amuz vya antenna havipati hii shida hata mvua inyeshe
3. Nenda dukani ulizia king'amuzi cha startimes cha dish na antenna kipi kina bei. Cha dish kinabei sana kwa sababu ya kulipia technlogies zilizimo mule ndani. so decoders za antenna zina bei ndogo na itakuwa nkomboz wa watz wengi