King’amuzi ni tofauti na Kisimbuzi

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
Tuzungumzie pia Kisimbuzi na King’amuzi. Kisimbuzi ni chombo maalumu kinachotambua ishara zilizofichwa na kuzifanya zionekane au kusikika katika redio, simu au televisheni. Visimbuzi ndivyo tunavyovitumia katika televisheni majumbani mwetu. Kisimbuzi kimetokana na neno simba ambalo kinyume chake ni simbua. Kusimba ni kuelezea jambo kwa namna ya kificho kwa kutumia ishara na alama. Kinyume chake ni kusimbua yaani kubaini taarifa uliyopewa kwa njia ya kificho. Hivyo, kifaa kinachowezesha kubaini yaani kusimbua ni Kisimbuzi. Mfano wa matumizi unaweza kuwa, ‘Baba amelipia Kisimbuzi chetu ili tuone fainali za kombe la dunia’ au ‘Kisimbuzi chetu kilipoharibika tulikirudisha kwa wakala aliyetuuzia.’

King’amuzi kwa upande wake ni chombo maalumu kinachogundua kuwapo kwa vitu kama vile mabomu, madini, dawa za kulevya na vitu vingine. Mfano wake wa matumizi unaweza kuwa,King’amuzi kimefungwa katika mlango wa uwanja wa ndege ili kuwabaini wanaoingi na vitu visivyoruhusiwa’ au ‘Ving’amuzi vilitumika kutafutia mabomu yaliyofukiwa.’ King’amuzi kinatokana na neno ng’amua ambalo maana yake ni tambua au fahamu jambo fulani.
 
Kama nimekuelewa unamaanisha kuwa kisimbuzi kwa lugha yetu sisi wengine, ni decoder au decipher na king'amuzi ni Sensor, si ndio?
 
Back
Top Bottom