Naombeni msaada kuhusu changamoto hii ya kisimbuzi cha Azam

danhoport

JF-Expert Member
May 20, 2020
1,611
3,196
Habari wakuu,

Naombeni msaada wenu.

Nimenunua kisimbuzi cha antena cha Azam bila antena nimekuja nacho kibaha nikaunganisha kwenye antena.

Cha ajabu zinakuja channel za startimes na nimejaribu kusearch zaidi ya Mara tatu lakini channel ni zile zile za startimes zinakuja.

Shida inaweza kuwa ni nini?
 
Ume-disconnect cable inayotoka kwenye kisumbuzi cha startimes kwanza? maana inakuaje uweke cha AZAM alafu zionekane za Startimes, check vizuri mkuu hasa kwenye kuhamisha hapo kwenye TV
 
Ume-disconnect cable inayotoka kwenye kisumbuzi cha startimes kwanza? maana inakuaje uweke cha AZAM alafu zionekane za Startimes, check vizuri mkuu hasa kwenye kuhamisha hapo kwenye TV
Kisimbuzi Cha startimes nimekitoa, ilo swali Mimi mwenyewe ndo linanichanganya inakuaje nikisearch zinakuja za startimes? Na hazioneshi
 
Au tusipoteze muda nenda kwenye setting then channel seach badilisha freequency kwenda namba 504 juu na chini weka hiyo hiyo then seach papo hapo zinakuja hizo channel za azam
Nashukuru mkuu ngoja nifanye hivyo🙏 ila nitaleta mrejesho baadae mana sahv sipo nacho karibu
 
Frequency zinasoma 474 hazibadiliki
Au tusipoteze muda nenda kwenye setting then channel seach badilisha freequency kwenda namba 504 juu na chini weka hiyo hiyo then seach papo hapo zinakuja hizo channel za azam
 
Wakati unanunua uliwauliza kama signal ya azam inafika vema huko kibaha ?.maana vya antenn ninavyojua mimi si kila maeneo yana hyo signal
 
Nimeamua kukirudisha nilipokinunua
Azam ya antena sio kwamba inashika kila eneo mkuu,mimi ni fundi wa hivi vitu,wanachokifanya wanasimika mnara mfano kwa mbezi upo kifuru na unarusha signal kwa mfan 22km radius. Kwahyo ukiwa nje na hizo km bas huwezi kupata signal hata iweje,nje na hapo zitakuwa zinakuja za startimes tu,pia antena ya azam haitaki karibu na miti mirefu sana ama majengo marefu kuipata inakuwa kidogo changamoto,nje na hapo tumia dish ambalo halichagui uko mkoa gani kutokana na kupokea mawimbi kwa njia ya satellite.
 
Vya antenna uongo chukueni vya dish.. Mimi mwenyewe nataka nichukue cha dish tu japokua nilipo cha antenna kina works vizuri tu...
 
Back
Top Bottom