Kisima cha kutunzia maji ya mvua

Nawashukuru sana wote kwa michango yenu wadau,nimefarjika sana. Nitawaletea mrejesho. Nawatakia usiku mwema. Bado milango iko wazi kwa maboresho. MUNGU awabariki sana mliochukua muda wenu kunisaidia maboresho haya. Asanteni
 
Hivi kwa mfano ukiamua kujenga tanki la juu ya ardhi na kulifunika, say kwa ujazo huo huo - gharama haziwezi kuwa nafuu Zaidi?
Naamini hilo zoezi litakula hela mpaka uikimbie dunia mkuu. Huo mpango ni hatari. Naamini inaweza kuwa zaidi ya milioni 9 ya kisima
 
Wana JF wote nawasalimia kwa umoja wetu. Bila kupoteza muda naombeni ushauri.

Home kijijini kwetu kuna hali ya uhaba wa maji,nilikuwa nina mpango wa kuchimba kisima cha drilling. Sasa jana kuna mtaalam amekuja akanishauri ili kupunguza hizo gharama za kisima cha drilling zinazofikia milioni 8 mpaka 9,akanishauri tuchimbe kisima futi 20,kijengelewe vizuri kifungwe juu.

Gharama ya hii ni usiyozidi milioni 3,then niwe navuna maji ya mvua lita zisizopungua 60,000 kwa mwaka. Tunayatia dawa,water gud.Nayavuta kupandisha juu kwenye tank then tunaya-saplay nyumba nzima kwa matumizi ya kupikia na kufulia na kuoga. Sasa nauliza mwenye uzoefu vipi kuhusu hayo maji na huo mpango?
Binafsi ndo nipo kwenye mchakato huo na shimo langu ni kwenda chini ni foot 24
Upana ft 10

Kwa upana huo natarajia kuvuna Lt 40000 elfu

Na matumiz yangu kwa siku nimepiga hesabu
Kwa idadi ya watu ma shughul za kila siku home ni Lita 100 tu ambapo hizo 40000 nikigawa kwa 100 napata siku 400

Nb kuna siku matumiz yatapanda na sio Ila siku itakuwa 100 kuna siku yatashuka mpaka 60

Kwa wewe Lt 60000 naona kama nyingi sana kumbuka msimu wa mvua matumiz ya karo yatapungua sana

Miez mitatu yote
 
Hayawezi kuwa na vumbi,ni Kama tumeyatumia mara nyingi,isitoshe tutaweka dawa. Japo sawa hayawezi kuwa sawa na ya kisima kwa ubora. Tuna compare na gharama pia. Asante kwa maoni pia sister.
Pia unaweza kuweka filter kabla ya kuingia kwenye storage tank.. na filter wakati wa kuyavuta kujaza Tank la juu.. yanakuwa safi kabisa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Daah...! Umeua kamanda,asante sana. Hilo la cement yupo mtaalam atasimamia. Isitoshe kuhusu tofali kaniambia tutatumia hizi za kuchoma ila atazipanga kama unavyojengwa msingi ili kuufanya huo ukuta wake usipungue futi moja upana wake,hiyo ni kuanzia chini mpaka juu. Zaidi umeongezea kitu ambacho yeye hakusema kuhusu hiyo karatasi la nailoni nyeusi kwa chini. Asante sana mkuu
Jenga na tofali ya block.. na iwe kwa ratio ya tofali 20-25 kwa mfuko wa cement.. zinapojengwa zinakatwa nusu na mortar inakuwa ratio kali.. ukimaliza ndani tumia wire mesh kabla ya kupiga lipu ya kwanza..

Lipu ya pili changanya na water proof cement.. kabla ya Kumaliza ba niru yenye kiwango Cha kutosha Cha water proof..

Nb chini kabla kuanza kunyanyua ukuta Kama unaweza tandika janvi lenye nondo thickness at least cm 15.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Maji ya mvua yana vumbi sana. Aidha, huwa yananuka sana yakikaa muda mrefu. Hivyo, ushauri wangu ni kuchimba kisima.
Msimu wa mvua unapoanza kuna maji hata kimilia Yale ya mwanzo huruhusiwi kuyakinga nakutumia Yale huyaacha walau mvua ipige wiki

Kitaalamu bati linajisafisha kwanza na kuondoka na na vumbi kabisa

Kiimani au kimila wanasema Ya nakuja na majini ndo mana ukinywa utaumwa msimu mzima
 
Hakuna tatizo, utapunguza gharama kubwa sana. 20' deep, 15' diameter gharama inaweza kufika 4m au zaidi kutegemeana na eneo husika.

Muhimu tu utumie tofali imara, usiwe bahili wa cement, ukiweza weka wire mesh ili kuimarisha kuta, chini weka ile nailoni nyeusi ili kuzuia maji kupotea, jenga msalaba ili kuimarisha kuta na hakikisha unalifunika ili mwanga wa jua usipenye ndani. Ukifanya hivi hata hizo water guard utaweka kwa utashi tu ilà haitakuwa lazima.

Utaokoa gharama nyingi kununua maji.
Nipate namba yako
 
Binafsi ndo nipo kwenye mchakato huo na shimo langu ni kwenda chini ni foot 24
Upana ft 10

Kwa upana huo natarajia kuvuna Lt 40000 elfu

Na matumiz yangu kwa siku nimepiga hesabu
Kwa idadi ya watu ma shughul za kila siku home ni Lita 100 tu ambapo hizo 40000 nikigawa kwa 100 napata siku 400

Nb kuna siku matumiz yatapanda na sio Ila siku itakuwa 100 kuna siku yatashuka mpaka 60

Kwa wewe Lt 60000 naona kama nyingi sana kumbuka msimu wa mvua matumiz ya karo yatapungua sana

Miez mitatu yote
Sema lita 100 kwa mfumo wa maji ya man ndani ni kidogo. Ukiweka na upotevu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Binafsi ndo nipo kwenye mchakato huo na shimo langu ni kwenda chini ni foot 24
Upana ft 10

Kwa upana huo natarajia kuvuna Lt 40000 elfu

Na matumiz yangu kwa siku nimepiga hesabu
Kwa idadi ya watu ma shughul za kila siku home ni Lita 100 tu ambapo hizo 40000 nikigawa kwa 100 napata siku 400

Nb kuna siku matumiz yatapanda na sio Ila siku itakuwa 100 kuna siku yatashuka mpaka 60

Kwa wewe Lt 60000 naona kama nyingi sana kumbuka msimu wa mvua matumiz ya karo yatapungua sana

Miez mitatu yote
Lita 100 ndogo sana. HapO hUjafua, mtoto hajasafishwa, vyombo. Fanya 300
 
Tena ukiwa na mfumo wa mabomba ya ndani.. per day kwa nyumba ya familia Inatakiwa at least 350-500litres.. maana single toilet flush ni 5litres .. bado kuoga, jikoni.. usafi mwingine..

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mkuu 500L ni nyingi mno, hiyo ni kama nusu boza(bowser) ambayo ni 1,000L, unless yupo na familia kubwa sana. Ndoo kumi-kumi na tano (200L) hivi zinatosha kwa siku hata kama umeweka system ya maji ndani. Japo katika matumizi ya maji siku hazilingani.
 
Hakuna tatizo, utapunguza gharama kubwa sana. 20' deep, 15' diameter gharama inaweza kufika 4m au zaidi kutegemeana na eneo husika.

Muhimu tu utumie tofali imara, usiwe bahili wa cement, ukiweza weka wire mesh ili kuimarisha kuta, chini weka ile nailoni nyeusi ili kuzuia maji kupotea, jenga msalaba ili kuimarisha kuta na hakikisha unalifunika ili mwanga wa jua usipenye ndani. Ukifanya hivi hata hizo water guard utaweka kwa utashi tu ilà haitakuwa lazima.

Utaokoa gharama nyingi kununua maji.
Ukifata principal hizo unamaanisha maji hayawezi kuleta harufu na utelezi yanapokaa sana? Wazo zuri hili
 
Maji ya mvua ukiyahifadhi vizuri, Yanakaa hata mwaka na yanakuwa vilevile kama umeyakinga leo. Cha msingi ni yahifadhiwe semehu ambayo mwanga wa jua hauyafikii
Hivyo kwenye ujengaji wake yatupasa kuweka nailini jeusi chini ya kisima na juu pia Kama sikosei?
 
Maji ya kisima pia ni mazuri maana ni ya kudumu hasa ukipata maji mapole. Tatizo hizo bei, naona ziko juu sana.

Utaweka ya mvua ni sawa kabisa, hivi wawezaje wote wanaokuzunguka hawana maji wewe uko ndani na familia yako na maji yako, hakika mimi siwezi.

Namkumbuka mtu mmoja alijiwekea matanki makubwa na akawa anapata maji ya mwaka mzima ila kwake husogei maana siyo mageiti hayo. Bahati mbaya sana mume na mke wametangulia, ule mjumba upo hakuna hata anayeishi, maisha bana.

Hapa kwetu tulikuwa na shida sana ya maji chini pia wapimaji miaka ya nyuma walisema maji hakuna, ila nilipochimba nilipata maji ya kisima na ikabidi nichimbe visima viwili changu na cha raia. Yaani wanachota for no cost maana nami ni kama Mungu alinipa maji kwa sababu tu japo nilitumia gharama sana.

Angalia jipime na moyo wako na mazingira ya watu wako ufanye litakalokupendeza.
 
Back
Top Bottom