Kisima cha kutunzia maji ya mvua

Kisima cha kutunzia maji ya mvua

Nimejaribu hii kitu ya kuvuna Maji baada ya Maji ya Makao Makuu kuwa adimu, ni balaa gharama ziko juu pia mafundi wameniogopesha eti kuweka Lita 5000 sio salama.
 
Hujui kitu wewe gamba waachie wataalam waliosomea hizo kazi,kwamba hujawahi sikia water harvesting technology? Hata lichama lako Lina sera hii ili kupunguza upotevu wa maji na uhaba pia
"Nikiibiwa kura nitaingiza watu barabarani"--Tundu Lissu.
 
Kisima cha chini cha kufunikwa cha ujazo wa 60,000 ltr hiyo 3mln hazitoshi kabisa, badala yake bora kuchukua plastic tanks isio zidi 5,000 ltrs @ sababu zaidi ya hapo pia ni ghali zaidi pole pole

USHAURI WANGU: Kama maji ya kuchimba visima virefu yanapatikana hasa yasizidi 120 mtrs na uwezo wa hizo pesa unazo hiyo 9mln plus upate umeme This is the best option

Utapata maji mengi sana kwa mifugo yako na ya kumwagilia bustani, shamba na miti
Na majirani pia watapata maji
 
Naomba namba yako niko tayari kulipa consultation fee , tayari nimechimba kisima, na Tower tumejenga 8 mtr high base ya 3 m diameter matofali ya kulaza kila 2m bean nondo 4 na katikati sbb ni msaraba katikati kuna column ya nondo 4 toka chini.

Swali langu mnara huu unaweza beba tank la ujazo gani wa maji maximum ?
Swali la pili tofauti ya cost ya container per ltr kwa haya matank yafuatayo mfano wa 30,000 ltrs
1. Tank la kujenga chini ya ardhi moja au 2
2. Tank la kujenga juu ya ardhi 1,2 hata 3
3. Tank la plastic kwa maeneo nilipo 10,000L ni sh 2,400,000 site
2,400,000x3 =7,200,000 /30000 = Tsh 240 per lita maji
4. Tank plastic 3000L ni sh 520,000 site
650,000 x 10 = 6,500,000 /30,000 = Tsh 216 per lita

naomba msaada makadirio ya gharama namba 1 na 2 tafadhali
Njoo kwa debe... Nilikuwa safari kikazi

Sorry...
 
Nimejaribu hii kitu ya kuvuna Maji baada ya Maji ya Makao Makuu kuwa adimu, ni balaa gharama ziko juu pia mafundi wameniogopesha eti kuweka Lita 5000 sio salama.
Wamekutisha bure tu...
Na lita elfu tano ni tanki dogo sana... Unless ulitaka kumaanisha 50000! Hata hivyo lita elfu hamsini sio kubwa sana na inajengwa kwa uwezo wa mafundi hawa hawa wa kawaida. Weka makadirio ya ujenzi wa mita moja ya ujazo kwa tshs. 1500000 kwa gharama za juu kabisa (ambayo ni sawa ujazo wa lita elfu moja) lita elfu hamsini zitakuwa kati ya milioni 7 na 8 makadirio ya juu... Na chini inaweza kushuka mpaka milioni 4/5 kwa lita elfu hamsini kulingana na upatikanaji wa materials na gharama za mafundi.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Standard shower head inatoa maji yasiyopungua lita 9.5 kwa dakika. By design. Na vyoo vya kishua vya option ni ghali wengi wetu tunatumia squatting toilets.. ambazo tank yake inakula lita tano.. pale kuna kamba tu au lever haja yoyote ..ile ukikavuta tu tano hizooo.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Dah ndo maana mwenye nyumba kaning'olea kwangu
 
Asante mkuu. Kwa mtaalam kaniambia zitatosha,kwa sababu mvua max zinaanza mwezi wa 11,zinaendelea mpaka wa 5 hivi,zitakoma kisima kitakuwa kimejaa. Tutatumia mwezi wa 6,7,8 9,10. Zaidi hizo lita 60 elfu tutazitegemea kwa hiyo miezi mitano mpaka 6. Kaniambia yatatutosha
Unit 10 kwa mwezi mbona kidogo sana, una familia ya watu wangapi?

Tengeneza lenye ujazo wa lita 100,000 ama 120,000 ili uishi kifalme.

Halafu uelewe kuna upotevu wa asili wa maji.

Maji ni majanja sana lazima yapenye penye, yakutoroke hata kidogo hata kama umeimarisha kihandisi ujenzi wako.

Katika hesabu zako lazima uweke na ziada kukabiliana na loss.
 
Ni kweli mkuu mimi mwenyewe nimeliona hilo. Hicho cha hizo lita 120,000,si itakuwa gharama,sawa na kuchimba kisima cha griling mkuu?
 
Ni kweli mkuu mimi mwenyewe nimeliona hilo. Hicho cha hizo lita 120,000,si itakuwa gharama,sawa na kuchimba kisima cha griling mkuu?
Drilling wana bei chafu sn. Emb jaribu kufanya utafiti kote kote kabla haujachukua maamuzi.

Nijuavyo kujenga ujazo tunaoujadili hakuwezi kukugharimu kama kuchimba.
 
Ndugu ushauri uliopewa Ni nzuri lakini hicho kisima kama unataka kutumia maji ya Mvua kwa Muda mrefu yakutane na maji ya Mvua msimu ujao, nakushauri usije ku- supply kwenye mabomba nyumba nzima hata miezi 8 hayawezi kufika. Ukitaka hayo maji yakufikishe na Mvua nyingine mchote kwenye kisima kwa kutumia ndoo au dumu hapo yatafika.

Ukichota maji kwenye ndoo ndogo unaoga vizuri tena kwa bajeti. Uweke Bomba la Mvua watu wengi wanaoga ndoo 2 badala ya moja.

Maji ya kufungua kwenye koki Yana rahaa Yake yanatumika mengi kuliko kuchota kwenye kisima.

Kama unataka ku- supply kwenye system nzima ya mabomba ndani nyumba nakushauri chimba kisima cha drilling
 
Drilling wana bei chafu sn. Emb jaribu kufanya utafiti kote kote kabla haujachukua maamuzi.

Nijuavyo kujenga ujazo tunaoujadili hakuwezi kukugharimu kama kuchimba.
Ni kweli mkuu. Swali lingine najiuliza nyumba kubwa moja inatosha kukijaza kisima cha ujazo unaosema wewe huo wa lita 120,000?
 
Ni kweli mkuu. Swali lingine najiuliza nyumba kubwa moja inatosha kukijaza kisima cha ujazo unaosema wewe huo wa lita 120,000?
Kisima cha 120,000L sio mchezo ni kikubwa mno na gharama yake itakuwa kubwa sana hadi kimalizike, na nyumba lazima iwe kubwa ili kuweza kukijaza. 50,000L zinatosha sana, height=5m, diameter=3.6m unapata roughly 50,000L ambazo zinatosha sana kwa matumizi ya nyumbani.
 
Asante tena Eli79
 
Ni kweli mkuu. Swali lingine najiuliza nyumba kubwa moja inatosha kukijaza kisima cha ujazo unaosema wewe huo wa lita 120,000?
Mvua zote za masika zinajaza na zaidi.

Ushawahi kushuhudia mvua1 inajaza maji kiasi gani?

Unatakiwa kuudhibiti upenu wote wa nyumba yako kwa magata na maji yote yaelekezwe tankini.

Kwanza zile mvua kubwa za kukesha,waweza kustaajabu kulijaza kwa muda mfupi usivyotegemea.
 
Mkuu umepigia hesabu gharama za tofari, nondo, gharama za fundi kuchimba shimo na kujenga pamoja na wire mesh kisha uka conclude?

Na je ulishaonana na wachimba visima virefu wakakueleza gharama zao?

Me nilienda kuwaona kwa shida kama hiyo wakanipatia ghara zao, kuanzia safari ya kuwatoa ofisini hadi site, kuservey na kuanza kuchumba.

Kwa aridhi ilipo site walinikadiria kuyapata maji kuanzia 50 mtrs deep na kuendelea.

Sasa ukichukua hiyo mita 50×60,000, viunganishio hadi pump, m.10 ni ya kufikia!

Je hiyo reserve tank yenye ujazo wa unit 120, waweza ijenga zaidi ya m.7?

Embu weka kikokotoo ili tukitathimini kama hautajali.
 
Mvua zote za masika zinajaza na zaidi.

Ushawahi kushuhudia mvua1 inajaza maji kiasi gani?

Unatakiwa kuudhibiti upenu wote wa nyumba yako kwa magata na maji yote yaelekezwe tankini.

Kwanza zile mvua kubwa za kukesha,waweza kustaajabu kulijaza kwa muda mfupi usivyotegemea.
Sawa mkuu asante kunitoa wasiwasi. Ni kweli kuna mvua inakesha unakuta siku 3 mfululizo. Sasa vipi kuhusu gharama ya hicho cha lita 120,000 haiwezi kuwa sawa tu na griling?. Griling kawaida kwa huku haizidi milioni 8
 
Ndugu ushauri uliopewa Ni nzuri lakini hicho kisima kama unataka kutumia maji ya Mvua kwa Muda mrefu yakutane na maji ya Mvua msimu ujao, nakushauri usije ku- supply kwenye mabomba nyumba nzima hata miezi 8 hayawezi kufika. Ukitaka hayo maji yakufikishe na Mvua nyingine mchote kwenye kisima kwa kutumia ndoo au dumu hapo yatafika.

Ukichota maji kwenye ndoo ndogo unaoga vizuri tena kwa bajeti. Uweke Bomba la Mvua watu wengi wanaoga ndoo 2 badala ya moja.

Maji ya kufungua kwenye koki Yana rahaa Yake yanatumika mengi kuliko kuchota kwenye kisima.

Kama unataka ku- supply kwenye system nzima ya mabomba ndani nyumba nakushauri chimba kisima cha drilling
Kuchota kwenye kisima nafikiri haitawezekana mkuu. Ksbb kisima hakitakiwi kiingize mwanga kabisa,kufuatana na ushauri wa watalaam
 
Back
Top Bottom