Kisima cha kutunzia maji ya mvua

Kisima cha kutunzia maji ya mvua

[emoji23][emoji23] sikujua hili, 9.5L/min nadhani ni nyingi mno mkuu. Elevation ya tank hapo ni mita ngapi, kwa sababu hydraulic pressure itategemea sana tank lilipo. Tank/sink lenye options ni zuri zaidi, ukikojoa unabofya inatoka 2L, ukikaa ndio 5L zinakwagika.[emoji23]
Sisi waswahili bwana.. Kama hatujachuchuma Bado hujafanya yako...halafu na choo kikishaanza kula vilaki laki tunaghairi.. [emoji16]

Kweli nyumba ni choo ila ndio bei yake ilingane na kitanda!?[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mwanga wa jua una athari gani kwenye maji
mwanga wa jua unaipa nafasi micro organism kukua .wakikua wanakuwa wadudu hatari kwa afya pia wakifa wnaoza na kuchafua maji ndipo unakuta maji yananuka .Pia hawa wadudu hujisaidia pia
 
Naomba namba yako niko tayari kulipa consultation fee , tayari nimechimba kisima, na Tower tumejenga 8 mtr high base ya 3 m diameter matofali ya kulaza kila 2m bean nondo 4 na katikati sbb ni msaraba katikati kuna column ya nondo 4 toka chini.

Swali langu mnara huu unaweza beba tank la ujazo gani wa maji maximum ?
Swali la pili tofauti ya cost ya container per ltr kwa haya matank yafuatayo mfano wa 30,000 ltrs
1. Tank la kujenga chini ya ardhi moja au 2
2. Tank la kujenga juu ya ardhi 1,2 hata 3
3. Tank la plastic kwa maeneo nilipo 10,000L ni sh 2,400,000 site
2,400,000x3 =7,200,000 /30000 = Tsh 240 per lita maji
4. Tank plastic 3000L ni sh 520,000 site
650,000 x 10 = 6,500,000 /30,000 = Tsh 216 per lita

naomba msaada makadirio ya gharama namba 1 na 2 tafadhali
Kujenga tank underground au on ground ni gharama...
Kama umejenga mnara wa 8m na umejenga kwa tofali imara na umeweka Msingi imara...na then ukaweka kitako strong pale juu, then unaweza kuweka simtank la Lita elfu 5 au 10... Na ukawa ukafunga motor pump ya umeme kwenye kisima chako... Then ukafanya plumbing nzuri kwa house yako.. Unaweza kuinjoi Maji vizuri... Kwa familia Maji hayo yanatosha kabisa...

For consultation check me kwa debe... I can send you a simple BOQ. And a simple sketch..
 
Maji ya mvua yana vumbi sana. Aidha, huwa yananuka sana yakikaa muda mrefu. Hivyo, ushauri wangu ni kuchimba kisima.
Hapa uko sahihi na huwa yanatoa ute mlaini na kuteleza. Sio safi kwa ustawi wa afya hasa yakikaa kwa muda mrefu, hata yakiwekwa usalama bado yana athari.
 
Maji ya mvua ukiyahifadhi vizuri, Yanakaa hata mwaka na yanakuwa vilevile kama umeyakinga leo. Cha msingi ni yahifadhiwe semehu ambayo mwanga wa jua hauyafikii

Mwanga wa jua una athari gani kwa maji ya mvua?
 
mwanga wa jua unaipa nafasi micro organism kukua .wakikua wanakuwa wadudu hatari kwa afya pia wakifa wnaoza na kuchafua maji ndipo unakuta maji yananuka .Pia hawa wadudu hujisaidia pia
Hapa uko sahihi na huwa yanatoa ute mlaini na kuteleza. Sio safi kwa ustawi wa afya hasa yakikaa kwa muda mrefu, hata yakiwekwa usalama bado yana athari.
Mwanga wa jua una athari gani kwa maji ya mvua?
@Rodrigo Moreno amejibu vema.

Maji ya mvua ni salama.. miji Kama handeni ambako maji Ni shida watu wengi wanatumia maji haya kwa shughuli zote na hakuna waterborne diseases. Miaka yote

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ubarikiwe sana
Maji ya kisima pia ni mazuri maana ni ya kudumu hasa ukipata maji mapole. Tatizo hizo bei, naona ziko juu sana.

Utaweka ya mvua ni sawa kabisa, hivi wawezaje wote wanaokuzunguka hawana maji wewe uko ndani na familia yako na maji yako, hakika mimi siwezi.

Namkumbuka mtu mmoja alijiwekea matanki makubwa na akawa anapata maji ya mwaka mzima ila kwake husogei maana siyo mageiti hayo. Bahati mbaya sana mume na mke wametangulia, ule mjumba upo hakuna hata anayeishi, maisha bana.

Hapa kwetu tulikuwa na shida sana ya maji chini pia wapimaji miaka ya nyuma walisema maji hakuna, ila nilipochimba nilipata maji ya kisima na ikabidi nichimbe visima viwili changu na cha raia. Yaani wanachota for no cost maana nami ni kama Mungu alinipa maji kwa sababu tu japo nilitumia gharama sana.

Angalia jipime na moyo wako na mazingira ya watu wako ufanye litakalokupendeza.
 
Nashauri chimba kisima... Matumizi yatakuwa makubwa zaidi. Nahayo madawa yoote yakuhifadhi maji hayatakuwepo.

Chimba kisima mkuy
 
Naomba msada wa vipimo vya tank la chini lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki moja.
 
Naomba msada wa vipimo vya tank la chini lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita laki moja.
1) Lita laki moja ni sawa na Cubic meter 100 (100,000 /1000=100m³)

2) Ukichimba mita 4 (4m) x mita 5( 5m ) x mita 4(4m) yani (urefu mara upana mara kimo) =100m³ sawa na Lita 100,000

Hivyo ni vipimo vya ndani kwa ndani
 
Ahsante sana
 
Sio kweli ndugu

Mi natumia haya kwa miaka 10 sasa, sijaona shida yake, natumia kwa kila kitu kunywa na kupikia na kupikia.
Kabisa mkuu mwenyewe wakati naanza kazi nilipewa nyumba na taasisi iliyokua ina kisima cha maji ya mvua yalikua safi kabisa kiasi ukiyakuta usipoambiwa ni maji ya mvua huwezi kujua
 
Mwanga wa jua una athari gani kwa maji ya mvua?
Hata mi napenda kujua hili

Halafu mnawezaje kutumia maji yaliyokaa muda mrefu hivyo?? Bora kuchimba kisima cha kawaida tu
 
Hii kitu nimetengeneza kwangu hapa Dar. Ninavuna kama lita 200,000 kwa mwaka. Ni gharama sana kujenga ila ukimaliza ni Maisha murua sana. Maji utunzaji wake siyo mgumu maana nachanganya na maji ya dawasco lita elf tatu tu kwa mwaka.
 
Wana JF wote nawasalimia kwa umoja wetu. Bila kupoteza muda naombeni ushauri.

Home kijijini kwetu kuna hali ya uhaba wa maji,nilikuwa nina mpango wa kuchimba kisima cha drilling. Sasa jana kuna mtaalam amekuja akanishauri ili kupunguza hizo gharama za kisima cha drilling zinazofikia milioni 8 mpaka 9,akanishauri tuchimbe kisima futi 20,kijengelewe vizuri kifungwe juu.

Gharama ya hii ni usiyozidi milioni 3,then niwe navuna maji ya mvua lita zisizopungua 60,000 kwa mwaka. Tunayatia dawa,water gud.Nayavuta kupandisha juu kwenye tank then tunaya-saplay nyumba nzima kwa matumizi ya kupikia na kufulia na kuoga. Sasa nauliza mwenye uzoefu vipi kuhusu hayo maji na huo mpango?
Ni kweli mie nimelipa gharama za bill Dawasco 84000 kwa kipindi cha miaka 4. Miss mwingi maji ya kuvuna
 
Hii kitu nimetengeneza kwangu hapa Dar. Ninavuna kama lita 200,000 kwa mwaka. Ni gharama sana kujenga ila ukimaliza ni Maisha murua sana. Maji utunzaji wake siyo mgumu maana nachanganya na maji ya dawasco lita elf tatu tu kwa mwaka.
This was an overkill for domestic use lkn!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom