GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
Ni sahihi kuchimba kisima cha maji kipindi cha mvua?
Sikuwa na mpango wa kukichimba muda huu, lakini mtu anayelihudumia shamba langu kwa sasa kaniambia anaweza kukichimba kwa bei nafuu hadi ayakute maji. Nilipomwambia kuwa visima vianvyochimbwa nyakati za mvua zinaweza kuishiwa maji wakati wa kiangazi, kajibu kuwa hilo likitokea, atakifukua tena hadi ayakute maji.
Kwa wenye uzoefu, nini ushauri wenu?
1. Ni kweli kuwa kisima kichimbwacho kwa mikono nyakati za mvua zina uwezekano wa kuishiwa maji wakati wa kiangazi?
2. Ikiwa kisima kitakaukiwa maji wakati wa kiangazi, kuna uwezekano wa kupata maji endapo kitafukuliwa zaidi kwenda chini?
Asanteni🙏🙏🙏