Kisa Maji, Madiwani Ilemela Mwanza, wahofia kukosa Kura Uchaguzi mkuu Ujao

Torra Siabba

Senior Member
Jul 24, 2016
105
102
Swala la Ukosefu wa Maji katika halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza imekuwa sugu kiasi kwamba wananchi wanakosa walalamike kwa nani kutokana na kero ya ukosefu huo wa maji safi na Salama.

Kijografia Ilemela imezungukwa na Ziwa Victoria lakini upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi sio wa Ilemela imekuwa changamoto kubwa ambayo imewashinda wengi kutatua, Inaelezwa kwamba maji katika wilaya hiyo hutoka kwa muda usiozidi mara mbili kwa mwezi na wakati mwingine hutoka usiku wa Manane na kuwalazimu wananchi kuamka usiku ili kukinga maji.

Leo Agosti 11 Kimefanyika kikao cha baraza la Madiwani Wilayani humo ikaibuka hoja ya ukosefu wa maji safi na salama, Diwani wa kata ya Nyakato Jonathan Mkumba akasema Mamlaka ya maji safi na maji taka mkoani Mwanza wanafanya uzembe mkubwa kwa kutotimiza wajibu wao jambo ambalo amedai kuwa Litawanyima kura Wagombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Katika uchaguzi mkuu ujao kwakua Wao kama Viongozi wa kata Ilemela wameshasema Uongo kwa wananchi kwamba Maji yatapatikana lakini imekuwa kama hadithi za Abunuasi.
 
Dah yaani wanazidiwa hadi na Dodoma kwenye upatikanaji wa maji wakati wamezungukwa na Ziwa Victoria.
 
Waziri wa Maji Juma Aweso tunaambiwa 'anapiga kazi sana' na ni miongoni mwa vipenzi vya Rais Mama Samia. Hata mkewe mmoja ambaye ni DC wa Pangani ameamua kumchora tatoo kifuani kwake kama 'appreciation'. (uzi uko humu)
 
Mamlaka.ya maji safi Mwanza ndio Wazembe Aweso anahusika kuweka msukumo tu maana hata miradi ikiwa tayari Mnufaika ni Mwauwasa sio Aweso
 
Waziri wa Maji Juma Aweso tunaambiwa 'anapiga kazi sana' na ni miongoni mwa vipenzi vya Rais Mama Samia. Hata mkewe mmoja ambaye ni DC wa Pangani ameamua kumchora tatoo kifuani kwake kama 'appreciation'. (uzi uko humu)
Huyo Bibi kazi yake ni kusifia mitala.

Ukiona Bibi tozo anamsifia mtu chunguza
 
Back
Top Bottom